Indume
Member
- Apr 11, 2011
- 81
- 36
Nimekuwa nikiimba sana wimbo wa Taifa toka nikiwa mdogo ninasoma chekechea hadi sasa hivi. Kuna maneno ambayo katika wimbo huo nadhani unahitaji marekebisho. Pale panapoimbwa........" Wabariki Viongozi wote". Kwa jinsi ilivyo hata kama kiongozi ni Fisadi, ,mwizi, muuza madawa ya kulevya, mtoa rushwa, mbakaji kama yule mzee, tapeli, muuaji, ......basii eti hao viongozi "wabarikiwe na Mungu". Mi nasema hapana. Ni busara inahitajika kutumika ili sehemu ya wimbo huo usomeke na uimbwe " wabariki wazalendo wote".
Labda ndio maana nchi hii hali ya uchumi ni mbaya kwa kuwa hata waovu wanaimbiwa wabarikiwe, matokeo yake viongozi wa nchi hii inakuwa kuwa wamelaaniwa na kushindwa kuleta maendeleo thabiti.
Nawasilisha