#COVID19 Wimbi la tatu la COVID 19: Tusimame pamoja na maono ya Jemedari mpya

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,074
28,272
Habari za jioni wanaJF!
Mimi ni muumini wa kumsikiliza kiongozi katika mapambano yoyote.

Upo muda wa taharuki,kutoaminiana, kuchallange, kujadili na hatimaye kuchukua upande na uelekeo.

Mwaka 2020 tulikuwa na Jemedari wa vita dhidi ya covid 19 na alituvusha salama with acceptable number of fatalities.

Mwaka huu tunaye Jemedari mpya aliyejifunza uzoefu wa vita hivi lakini pia Jemedari huyu anaikuta vita katika hali ya mabadiliko.

Kwa namna yoyote ile kila Jemedari ana mbinu zake ambazo anaziamini ni sahihi na kila subordinate ni lazima na muhimu kuzifuata kwa afya ya mfumo.

Naweka bandiko hili kujaribu kuelezea ni kwa nini sasa tukubali kuchanjwa kama sehemu ya afua zinazobadilika mara kwa mara katika mpambano huu.

Sio jambo geni kubadilika katkati ya mapambano ,tufanye hivyo sasa na tuujenge umoja wetu.

Kwa sasa afua ya chanjo imeonekana (with all doubts and uncertainities) kuwa ndio afua bora.

Sasa tuungane rasmi ,tuikubali chanjo tuendelee kuielewa na baadhi yetu lazima tujitoe muhanga.

Kuna mdau anasema ni bora tuwe zombies kuliko kufa,isitoshe kama dunia yote tunaamua kuwa zombies basi hatuna budi kugeuka zombies wenye character(genes) za kitanzania.

#Kazi iendelee na tusameheane wotekwani wapingaji na waungaji mkono wote wana sababu za msingi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Marehemu huko aliko anageuka kaburini!

Ujumbe wangu:Wenzetu wana misimamo,ukiona hukubaliani na mkuu wa nchi basi unaachia ngazi!Leo hii kuna viongozi wamegeuka kituko!Kile walichokiamini walikikanyaga kwa maslahi yao binafsi ya madaraka!

Tujifunze kusimamia tunachokiamini,hata kama ni kwa gharama za nafasi zetu!
 
Jemedari mpya sio Gwajima, anayeendeleza falsafa za kujitegemea na kukataa chanjo za mabeberu ? 🤣🤸🐒
Anayo haki ya kuhoji na kuexpress alternatives.
Kwa mfano ukiniuliza ushauri wangu kwa sasa ni kuhakikisha tunakuja na uzalishaji wa chanjo yetu haraka kama kamati ilivyoshauri.
 
Anayo haki ya kuhoji na kuexpress alternatives.
Kwa mfano ukiniuliza ushauri wangu kwa sasa ni kuhakikisha tunakuja na uzalishaji wa chanjo yetu haraka kama kamati ilivyoshauri.
Hiyo haraka itachukua muda gani ?

Investment ya kujenga kiwanda cha kuzalisha chanjo itachukua miaka mingapi ?

Wataalamu tunao wa kutosha ?

Tuliambiwa chanjo ili itengenezwe inahitaji sijui miaka zaidi ya 10, tunauhakika wakuweza kutoa funding ya research kama hiyo kwa miaka 10++ ?

Kamati iliandika siasa ambayo haiwezekani kwa mazingira yetu unless tunpartner na hao hao mabeberu watuletee teknolojia sisi tuwe na waatalamu wanaofanya routine production lakini patent zote na teknolojia yote ibaki kwao.
 
Hakuna cha wimbi la tatu wala nini! Ni mwendo wa kujaribu kutowakwaza mabeberu tu! Hata mabeberu wenyewe wanajua!! Hili ni wimbi la kufikirika! Ukitaka kujua wimbi halisi linavyofanana waulize India, Italia, Hispania, marekani nk
 
Unafikri chanjo inazalishwa kama NIMCRAF, BUPIJI au COVIDOL hadi na nyie mzalishe kwa haraka
Anayo haki ya kuhoji na kuexpress alternatives.
Kwa mfano ukiniuliza ushauri wangu kwa sasa ni kuhakikisha tunakuja na uzalishaji wa chanjo yetu haraka kama kamati ilivyoshauri.
 
Ukiona kiongozi anafanya maamuzi bila kuwa na taarifa ujue hapo mmepigwa.
Rais anadai eti yeye ni bibi hivyo hawezi kudhamiria kujiua ataliza vijukuu.
Yaani hoja ya kijinga hivyo Rais anatumia kulizamisha taifa zima.
Tanzania tulikua na nafasi ya kipekee kabisa kulishinda gonjwa hili mzee wetu Magufuli amekubali kufa ili kuliokoa taifa yeye anakuja kuliuza kama nyanya mbovu.
UBINAFSI ni laana kwetu waafrika

Samaki mtungoni alijisemea mwana fasihi.
 
Back
Top Bottom