Willy Muga is no more!!!!!

Kwa nini hii serikali isipeleke jeshi huko???hawa watakuwa Intarahamwe tu....polisi haiwawezi hawa.Wanajeshi wapo hapo mijini wana vitambi???AIBU!!!
RIP wote walofariki kwenye tukio hilo.
 
je huyu jamaa yupo au ameuawa?

therad inanichanganya

shem...aliyekufa ni bwana anaitwa Willy Muga......aliyeripoti hii habari ya kuvamiwa kwa hilo basi asubuhi anaitwa Mu-Sir ni member wa JF....umeelewa sasa?
 
shem...aliyekufa ni bwana anaitwa Willy Muga......aliyeripoti hii habari ya kuvamiwa kwa hilo basi asubuhi anaitwa Mu-Sir ni member wa JF....umeelewa sasa?
nimeelewa shem, aikamae
 
habari iliyotangazwa saa mbili na ITV inasema majeruhi wapo 20 na hali zao ni mbaya kutokana na majeraha ya risasi, na aliyekufa ni mtu mmoja....tuzidi kuwaombea majeruhi wapone haraka
Kwa mujibu wa walionusurika na watu waliokuwa eneo la tukio waliokufa ni wawili.
Taarifa nilizozipata hivi punde zinasema Wilfred Muga Katibu wa CCM vijana Musoma Mjini ameuawa na majambazi leo asubuhi kwa kupigwa risasi akiwa njiani kutoka Kigoma Kuelekea Mwanza.
Mwenye taarifa za kina naomba atusaidie. Nlichosikia kuwa kuna watu wengine wawili pia wameuawa kwenye tukio hilo

Basi hilo la Kampuni ya China ya Golden Intercity Express lenye namba za usajili T 457 ARC lilikuwa limebeba abiria 51 lilitekwa na Majambazi hayo katika eneo la Mkugwa wilayani Kibondo, inasemekana majambazi hao walipiga sana Risasi, akielezea Mkasa huo kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, mmoja wa Wasafiri aliyekuwa ndani ya Basi hilo kutoka Kigoma kwenda Mwanza, Sophia Nasibu alieleza kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi ambapo alishuhudia Majambazi yakipiga risasi ovyo kwenye Basi hilo na hivyo Dereva kulazimika kusimama porini hapo.


Ameeleza kuwa majambazi hao yalikuwa yakipiga kelele kuwaamrisha Askari wawili wanaosindikiza Basi letu wasalimishe Bunduki zao, na baada ya muda mrefu huku yakitupiga risasi kutoboa toboa basi ndipo Askari hao wanaosindikiza Basi waliogopa na kuamua kusalimisha Bunduki zote mbili walizokuwa nazo, walizitupa mlangoni na Majambazi yakazichukua.
Majambazi hayo baada ya kuchukua Bunduki za Askari hao yalipoanza kuwapora Abiria fedha walizokuwa nazo huku wakiwachapa viboko baadhi ya waliokuwa wakorofi na ambao walionekana kukaidi.Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, George Mayunga alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kwamba amepata taarifa lakini bado anasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Kamanda wa Polisi wilayani Kibondo (OCD) Innocent ili aweze kuandaa taarifa rasmi.
 
Kwa nini hii serikali isipeleke jeshi huko???hawa watakuwa Intarahamwe tu....polisi haiwawezi hawa.Wanajeshi wapo hapo mijini wana vitambi???AIBU!!!
RIP wote walofariki kwenye tukio hilo.
Hukusia Hotuba ya JK??? Hakuna uhalifu.....na akawapongeza Polisi.... then wanajeshi wataongezewa marupurupu.....na sure wapo hapa mjini na kwenye makambi mengine kibao nchi nzima...............


KG ndo home...kila kitu shida, Maji, Umeme, barabara, reli, Shule, Hospitali (maweni) taaabu.....bado ukienda Majambazi......Emugabho????
 
Basi hilo la Kampuni ya China ya Golden Intercity Express lenye namba za usajili T 457 ARC lilikuwa limebeba abiria 51 lilitekwa na Majambazi hayo katika eneo la Mkugwa wilayani Kibondo, inasemekana majambazi hao walipiga sana Risasi, akielezea Mkasa huo kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, mmoja wa Wasafiri aliyekuwa ndani ya Basi hilo kutoka Kigoma kwenda Mwanza, Sophia Nasibu alieleza kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi ambapo alishuhudia Majambazi yakipiga risasi ovyo kwenye Basi hilo na hivyo Dereva kulazimika kusimama porini hapo.

Uwekezaji mweingine kweli ni ule unaoatufanya tuwe maskini zaidi kama hata mabasi yanakuwa ya wawekezaji. Nina wasiwasi sana kuwa dereva, tanoboi, na konda wa basi hilo analipwa kama yule wa daladala tu.
 
Huyo member wa JF aliyepuuzia taarifa ya dharura bado ana exist? m-delete kabisa kama vile hajawahi ku-exist!
 
Kweli bwana Wlfred Muga amekufa baada ya kupigwa risasi na majambazi.
Yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kufa, alifia eneo la tukio.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amin
 
RIP. poleni sana waathirikA, serikali should do smething on this. please!!
 
Majambazi yateka basi na kuua

Yapora polisi silaha na kupora abiria
Mtu mmoja ameuawa na wengine 23 wamejeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wenye silaha za kivita baada ya kuteka na kushambulia basi la abiria lililokuwa likitoka mjini Kigoma kuelekea Mwanza.
Katika tukio hilo lililotokea jana, abiria wameporwa mali mbalimbali pamoja na bunduki mbili za jeshi la polisi walizokuwa nazo askari waliolisindikiza basi hilo.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Mukugwa wilayani Kibondo mkoani Kigoma, takriban kilomita 30 kabla ya kufika mjini Kibondo, ambapo majambazi hayo yalilishambulia basi la kampuni ya Golden Inter City Express lenye namba za usajili T457 ACR linalofanya safari kutoka Kigoma kwenda Mwanza.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kibondo, Dan Makanga ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, majambazi hayo hayakuweka kizuizi chochote na kwamba waliibuka kutoka porini na kuanza kurusha risasi mfululizo na kuharibu vibaya basi hilo.
"Majambazi wanne wakiwa na silaha nzito walijitokeza barabarani na kuanza kurusha risasi hali iliyomlazimu dereva wa basi hilo Bw. Method Chang'a kulisimamisha, majambazi hao wakatoa amri kwa askari polisi waliokuwemo ndani ya basi hilo kusalimisha silaha na kadri walivyochelewa kufanya hivyo ndivyo majambazi hao walivyozidi kupiga risasi sehemu mbali mbali na kusababisha abiria wengi kujeruhiwa na risasi hizo", alisema Dan Makanga, Mkuu wa wilaya ya Kibondo
Imeelezwa kuwa kutokana na kuendelea kupigwa kwa risasi hizo kwa fujo huku askari polisi nao wakijaribu kujihami na kuwahami abiria bila mafanikio, walilazimika kuzirusha nje ya basi bunduki zao kitendo kilichowapa fursa majambazi kuziteka na kuanza kupora abiria mmoja mmoja.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kibondo, Florian Ntinuga amebainisha kuwa abiria aliyeuawa ni katibu wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM Musoma vijijini mkoani Mara.
Wilfred Peter Muga na abiria 23 wamejeruhiwa na kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo na watatu kati yao hali zao ni mbaya na wanasafirishwa kwenda Bugando kwa matibabu zaidi.
Majambazi hao ambao hawakuwa wameficha sura zao walifanikiwa kutokomea porini bila kukamatwa huku wakiondoka na silaha mbili aina ya SMG zikiwa na magazine nne mali za jeshi la polisi na imetajwa kuwa msako mkali katika pori hilo unaendelea ili kuwatia mbaroni majambazi hayo.
Eneo la Mkugwa lilipotokea tukio hilo lilikuwa kambi ya wakimbizi mchanganyiko kabla ya kufungwa na wakimbizi hao kuhamishiwa wilayani Kasulu na eneo hilo kufunguliwa shule ya sekondari ya juu ya wasichana.
Hili ni tukio la pili kutokea eneo hilo, katika kipindi cha miezi minne iliyopita ambapo majambazi yalilitega gari dogo la abiria na kumuua mwalimu Deo Kato ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Parokia ya kanisa katoliki Kibondo akiwa njiani kutoka Kasulu kwenda Kibondo.
Juhudi za kumpata mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma ACP George Mayunga hazikufanikiwa kutokana na simu yake kuwa katika matumizi kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani Kibondo, Innocent Rwelamira amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa askari wawili waliokuwa na silaha aina ya SMG wakisindikiza basi hilo wameporwa silaha zao na mmoja kujeruhiwa
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom