William Ngeleja - Waziri Anayetuhumiwa kwa Wizi!

MwanzoMugumu

Member
Jan 27, 2012
24
22
WanaJF baadaya kusoma maelezo na mapendekezo yenu katika "TOPIC" ya jana ilisomeka hii ndiyo hali halisi kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kumleta kwenu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam Mganga Ngereja aka Mr.Megawat.kuwa ndiye mmiliki wa nyumba ya ghorofa kama tano hivi make sijaingia. Nyumba hiyo inajengwa jijini Mwanza katika mtaa wa Rufiji, kwa kibali namba 5955 na Planning Consent No_21390. Project ni construction of Commercial Building Plot No. 7 Block O, ndani ya Mwanza city. Inasomeka kwamba client ni Jakandom Investment Co. Ltd,Box No_7528 Mwanza. Architect ni Mellow Architects wa jijini Mwanza, Quality surveyor ni A.M Quantity Surveying Consultancy na Main Contractor ni CF Builders Ltd wa Box No_ 1755 Mwanza.Kwa taarifa tu ni kwamba huyo client ni kupitia tu, huyo bwana ni mfanyabiashara wa samaki jijini mwanza wala hana hata uwezo wa kujenga jengo hilo. Ndugu zangu Waziri kujenga jengo kubwa kama hilo sio nongwa hata kidogo hoja hapa ni anapokuwa mtumishi wa umma tena katika wizara inayolalamikiwa na Watanzania walio wengi hapo ndipo maswali yanapoanzia. Tunamuomba Mhe Waziri ajitokeze hadharani kulitolea ufafanuzi jambo hili la sivyo patakuwa hapatoshi. Kwa kumbukumbu tu jengo hili limeanza kujengwa mwaka jana tu yaani linaota kama uyoga. NALETA KWENU WAUNGWANA
 
aiseeh! Hii inatakiwa itolewe na gazetini maana humu JF hawa wakubwa hawawezi kushtuka kabisa.
 
Huyu Mr Megawati mwaka jana tu alipigwa kiwanja cha mtu hapa Boko kauziwa na rafiki yake kumbe kiwanja cha mtu kaja na hati feki ya kiwanja mpaka sasa sijamuona hapa kaingia mitini.
 
Haya. Mwenye taarifa za siri za wakina Nundu, Mkulo, Mponda, Nkya, Nyalandu na Chami atuwekee. Hapa hatuangalii chunusi wala makunyanzi.
 
Wivu tu!, nyie kinawauma nini Mr.megawati kujenga gorofa?. Mbona mshahara wake na posho anazopewa spika zinatosha kujenga hata gorofa kumi?. sembuse hizo tano!.
 
WanaJF baadaya kusoma maelezo na mapendekezo yenu katika "TOPIC" ya jana ilisomeka hii ndiyo hali halisi kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kumleta kwenu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam Mganga Ngereja aka Mr.Megawat.kuwa ndiye mmiliki wa nyumba ya ghorofa kama tano hivi make sijaingia. Nyumba hiyo inajengwa jijini Mwanza katika mtaa wa Rufiji, kwa kibali namba 5955 na Planning Consent No_21390. Project ni construction of Commercial Building Plot No. 7 Block O, ndani ya Mwanza city. Inasomeka kwamba client ni Jakandom Investment Co. Ltd,Box No_7528 Mwanza. Architect ni Mellow Architects wa jijini Mwanza, Quality surveyor ni A.M Quantity Surveying Consultancy na Main Contractor ni CF Builders Ltd wa Box No_ 1755 Mwanza.Kwa taarifa tu ni kwamba huyo client ni kupitia tu, huyo bwana ni mfanyabiashara wa samaki jijini mwanza wala hana hata uwezo wa kujenga jengo hilo. Ndugu zangu Waziri kujenga jengo kubwa kama hilo sio nongwa hata kidogo hoja hapa ni anapokuwa mtumishi wa umma tena katika wizara inayolalamikiwa na Watanzania walio wengi hapo ndipo maswali yanapoanzia. Tunamuomba Mhe Waziri ajitokeze hadharani kulitolea ufafanuzi jambo hili la sivyo patakuwa hapatoshi. Kwa kumbukumbu tu jengo hili limeanza kujengwa mwaka jana tu yaani linaota kama uyoga. NALETA KWENU WAUNGWANA

Hao ndio mawaziri wetu....!!! Hawaguswi hao....!!! PCCB iko wapi, zaidi wanakamata vidagaa tu...!!!:doh:
 
He is not sure what tomorrow holds.....

anachukua chake mapema, shamba la bibi:crying::A S shade:
 
huo ni ujasiri wa kuleta details hapa bado picha sasa
weka picha kabisa na ikiwezekana fuatilia uhalali wa huyo mtajwa mmiliki kama anatumiwa na ngeleja
 
Hao ndio mawaziri wetu....!!! Hawaguswi hao....!!! PCCB iko wapi, zaidi wanakamata vidagaa tu...!!!:doh:
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?
 
Mimi siku zote napenda kuingia hivi!! Kama ifuatavyo
HII TZ MIMI NA IFANANISHA NA FRASH,MEMORYCARD NA EXTERNAL ZINGNE AMBAZO ZIMEJAA MA VIRUS
SASA IMEKUWA KILA SIKU NI KUDELETE TU! HAYA MATROJAN(kujivua gamba) MIMI NIONAVYO BORA KU FORMAT KULIKO KUSCAN NA MA ANT-VIRUS AMBAYO NI NOT UPDATED!!!! Sh***@@##zy kabisa
BORA KUIFORMAT KWA MGOMO NCHI NZIMA
TUANZE KUINGIZA FILES UPYA!
yaani nipo moto acha tu!
 
Kila kamba atakula kwa urefu wa Mbuzi wake !
uko sawa kabisa!!!!!!!!!!!!!!
ila sio kwa kuiba. Kelele zilizopo ni kuwa hawa wanaiba , kwa hiyo hawafanyi hayo kwa vipato vyao halisi. kumbuka fedha haramu ndizo pia zinasababisha mfumko wa bei, maana watu wezi wanaogopa kuweka pesa benki kwa hofu ya kuulizwa wametoa wapi, matokeo yake wananunua vitu kwa bei yoyote ile ili mradi pesa iishe na kumbuka kwa 7bu ni wizi hawana uchungu nayo.

Hivi hamjiulizi kwa utajiri gani walionao WATZ eti wanauziana kiwanja cha kujenga nyumba milioni moja, mbili, tatu, nne, kumi mpaka milioni mia tano. Pesa wametoa wapi kama sio za wizi wanataka watumie haraka haraka ziishe. Na kibaya zaidi hawa wezi hawawafaidishi WATZ, ila wengine wanapeleka mabenki ya ulaya halafu serikali ya TZ inaenda kukopa pesa hizohizo kule ulaya...zikifika bongo wanazirudisha ulaya badala ya kujenga viwanda bongo

NAOMBA WALE MLIO IBA PESA YA UMMA NA HAMJAKAMATWA, BASI JENGENI VIWANDA MTUAJILI WATZ WENZENU NA NINYI MUWE MATAJIRI ZAIDI VINGINEVYO MTAKUFA MASKINI NA MAPESA YENU YATALIWA NA NONDO, TUNUNTU na MCHWA

Back
Top Bottom