WanaJF baadaya kusoma maelezo na mapendekezo yenu katika "TOPIC" ya jana ilisomeka hii ndiyo hali halisi kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kumleta kwenu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam Mganga Ngereja aka Mr.Megawat.kuwa ndiye mmiliki wa nyumba ya ghorofa kama tano hivi make sijaingia. Nyumba hiyo inajengwa jijini Mwanza katika mtaa wa Rufiji, kwa kibali namba 5955 na Planning Consent No_21390. Project ni construction of Commercial Building Plot No. 7 Block O, ndani ya Mwanza city. Inasomeka kwamba client ni Jakandom Investment Co. Ltd,Box No_7528 Mwanza. Architect ni Mellow Architects wa jijini Mwanza, Quality surveyor ni A.M Quantity Surveying Consultancy na Main Contractor ni CF Builders Ltd wa Box No_ 1755 Mwanza.Kwa taarifa tu ni kwamba huyo client ni kupitia tu, huyo bwana ni mfanyabiashara wa samaki jijini mwanza wala hana hata uwezo wa kujenga jengo hilo. Ndugu zangu Waziri kujenga jengo kubwa kama hilo sio nongwa hata kidogo hoja hapa ni anapokuwa mtumishi wa umma tena katika wizara inayolalamikiwa na Watanzania walio wengi hapo ndipo maswali yanapoanzia. Tunamuomba Mhe Waziri ajitokeze hadharani kulitolea ufafanuzi jambo hili la sivyo patakuwa hapatoshi. Kwa kumbukumbu tu jengo hili limeanza kujengwa mwaka jana tu yaani linaota kama uyoga. NALETA KWENU WAUNGWANA
huyu jamaa anauchafu mwingi sana kanda ya ziwa, kajaza ukoo mzima geita gold mining mpaka darasa la nne, ununua magazeti yote mwanza mjini nyenye taarifa yake mbaya yasivuke jimboni kwake (je pesa hii anatoa wapi?) n.k na sasa swahiba wake mr tabasamu(diwani) wenye siri nying za huyu bwana ameamia CDM.... kwisha Mr william mganga ngeleja, mungu unajibu maombi asante.
tujaribu kufikiria sana kwa mapana hasa kwenye hali halisi ya uchumu wetu huyu jamaa aelleze amepata wapi hii hela
Tatizo TAKUKURU wamelala, hii taarifa inawahusu sana!
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?
Tatizo TAKUKURU wamelala, hii taarifa inawahusu sana!
Avatar hazidanganyi hata kidogo.....Siungi mkono hoja yako. Kwa sababu nina amini katika taratibu za kiungwana (sheria na kanuni bora kwa wote)Tumechoka sasa! Atakayemwona alipo Mr Megawati niambieni. Potelea mbali!
Mhuuu! Polepole ndugu.