William Ngeleja - Waziri Anayetuhumiwa kwa Wizi!

WanaJF baadaya kusoma maelezo na mapendekezo yenu katika "TOPIC" ya jana ilisomeka hii ndiyo hali halisi kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kumleta kwenu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam Mganga Ngereja aka Mr.Megawat.kuwa ndiye mmiliki wa nyumba ya ghorofa kama tano hivi make sijaingia. Nyumba hiyo inajengwa jijini Mwanza katika mtaa wa Rufiji, kwa kibali namba 5955 na Planning Consent No_21390. Project ni construction of Commercial Building Plot No. 7 Block O, ndani ya Mwanza city. Inasomeka kwamba client ni Jakandom Investment Co. Ltd,Box No_7528 Mwanza.

Architect ni Mellow Architects wa jijini Mwanza, Quality surveyor ni A.M Quantity Surveying Consultancy na Main Contractor ni CF Builders Ltd wa Box No_ 1755 Mwanza.Kwa taarifa tu ni kwamba huyo client ni kupitia tu, huyo bwana ni mfanyabiashara wa samaki jijini mwanza wala hana hata uwezo wa kujenga jengo hilo. Ndugu zangu Waziri kujenga jengo kubwa kama hilo sio nongwa hata kidogo hoja hapa ni anapokuwa mtumishi wa umma tena katika wizara inayolalamikiwa na Watanzania walio wengi hapo ndipo maswali yanapoanzia. Tunamuomba Mhe Waziri ajitokeze hadharani kulitolea ufafanuzi jambo hili la sivyo patakuwa hapatoshi. Kwa kumbukumbu tu jengo hili limeanza kujengwa mwaka jana tu yaani linaota kama uyoga. NALETA KWENU WAUNGWANA

Jaman acheni kudanganya watu.jengo hili ni mali ya njiwa poli mvuvi bilionaire wa mza tatizo mnaacha kufanya utafiti mnaanza uzushi
 
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?

Waungwana kama nilivyotangulia kusema kujenga ghorofa sio hoja kwani ziko nyingi katika miji yetu. Hoja hapa ni kwamba Waziri ambaye wizara yake inalalamikiwa kila kukicha. Pili kama kuna uhalali ya nini kijenga kwa kupitia majina ya watu kwanini lisiwepo jina lake? Tatu, report ya CAG inaonesha wizi mkubwa wa takribani wizara zote na idara zilizo chini yake. Nne tunasema experience ni mwalimu mzuri aum mbaya experience yetu Tanzania inaonesha viongozi wengi wa umma kukwapua malim za umma. Wito kama yote haya yako sawa sawa Waziri ajitokeze aweke mambo sawa sawa then tusongembele. Hatuna maslahi binafsi katika hili. Wakati tunalaribia kusherekea miaka 50 ya uhuru, Waziri wa zamani kidogo Paul Kimiti alieleza wakati wa awamu ya kwanza alipokuwa akijenga nyumba yake Dodoma Mwl Nyerere alimuita kwamba Kimiti nasikia unajenga niambie umepata wapi pesa? Naye akaonesha vielelezo kwamba amekopa Bank Mwl akamwambia endelea. Haya ndiyo maswali yetu na hoja zetu asema kapata wapi basi.
 
Wivu tu!, nyie kinawauma nini Mr.megawati kujenga gorofa?. Mbona mshahara wake na posho anazopewa spika zinatosha kujenga hata gorofa kumi?. sembuse hizo tano!.

No, Mhe Madame Supika alitamka hadharani sio siku nyingi zilizopita kuwa pale DOM kuna umasikini wa kutupa. Sasa kama kuna umaskini wa kutupa basi wananchi tuna haki ya kuhoji waheshimiwa wanapata wapi mafeza ya kujenga maghorofa wakati hatujasikia wameondoka DOM kushughulikia biashara zao. Hakuna Mbongo asiyependa watawala wetu watajirike, lakini huo utajiri usitokanae na kutunyonga sisi. Mzee wa Vijisenti alibainika ameweka tubilioni twake mabaenki ya nje jambo ambalo hatuna shida nalo, lakini hadi leo hii TRA haijatuthibitishia hiyo biashara yake ameisajili wapi na amelipia kodi kiasi gani. Tusiogoe kuwahoji eti kwa sababu tutaambiwa tuna wivu wa kike - vinginevyo tutakuwa tunashiriki kufuga ufisadi.
 
Wivu tu!, nyie kinawauma nini Mr.megawati kujenga gorofa?. Mbona mshahara wake na posho anazopewa spika zinatosha kujenga hata gorofa kumi?. sembuse hizo tano!.
Kila kukicha wajinga kama wewe wanazidi kujitokeza hapa,wewe unauona huu ni wivu sisi tunaumwa na kodi zetu walala hoi zinavyoliwa kinyemela na nyinyi mafisi, mbwa mwitu, manyang'au,bila huruma ya wenzenu wanavyoteseka,halafu yulisema mnasema ni wivu.
Hivi umesahau *Ghadafi aliwaita watu wake mende na matokeo yake uliyaona kilichompata?*Mubarak pale Egypt nae si unamuona anapelekwa mahakamani pingu mkononi huku akiwa kwenye machela!*Bingu wa mutharika alianguka chini ndani ya ikulu lakini hata walinzi wake hawakuwa na huruma nae na matokeo yake alipelekwa afrika kusini akiwa tayari kisha kufa saa nyingi!
Jifunze kufikiri maana upepo umekwisha badilika kaa chonjo!
 
kaka hawa ndo "ware ware"
 
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?

Tupe jina moja tu la waziri aliyejenga nyumba ya maorofa kama hayo enzi za Mwalimu

Tena huyu ana vimiradi vingi sana kwenye migodi ambavyo kaandikisha vijikampuni vyake kwa majina tofauti na ingekuwa TAKUKURU inafanya kazi basi wangesha mtoa hadharani
 
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?
Realistic ipi unayoitaka kutuaminisha kwa mtumishi wa umma kwa hesabu zinazoeleweka jengo kama hilo ni halipungui bil 2.5 imagine ameanza kazi 30 yrs ago means average salary kwake ni 2.5bil/30yrs=83mill/year kwa mtumishi wa umma mshahara wa namna hii haujawahi kutokea. hapo ina maana imeinvest mapato yake yote bila kula , kusomesha , kuuguza nk unless aprove genuine bussiness afanyayo otherwise ni wizi wa mchana.
 
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?

Kwa wastani Ngereja ana umri wa miaka 40. Tufanye ameanza kazi yenye kipato cha kueleweka akiwa na umri wa miaka 25. Hivyo basi, amekuwa ndani ya ajira yenye kipato cha kueleweka kwa kipindi cha miaka 15. Aidha, tufanye kwamba katika mshahara wake huo (kwa kipindi cha miaka 15) kila mwezi alikuwa na uwezo wa ku-save TZS 3,000,000/=, so kwa kipindi cha miaka 15 ame-save (3m*12*15= 540m). Tuseme amechukua personal loan bank, up to 80% ya bank balance aliyokuwa nayo kabla= [(540m*80/100)+540m=972m].
Hesabu hizo ambazo kwa makusudi nimezi-overapproximate zitamwacha Muhusika na kiasi cha Shilingi Milioni Mia Tisa Sabini na Mbili; TZS 972!
Hapa hakuna ushahidi kwamba nyumba hiyo ni Ngereja kweli. Hivyo, let’s assume kwamba hiyo nyumba inamilikiwa na mtu mwenye kipato sawa na hicho nilichoainisha hapo juu. The question is; Je, katikati ya Jiji la Mwanza mtu anaweza kujenga jengo la ghorofa tano kwa kiasi hicho cha fedha (TZS 972M)?!
Tupate makadirio toka kwa wataalamu ambao wamejaa humu JF! Kama haiwezekani, basi hapo kuna utata na lazima ifuatiliwe hiyo nyumba ni ya nani. Na kama kweli ni ya Ngereja, basi anatakiwa atoe maelezo ni vipi alifanikiwa kuanzisha ujenzi wenye gharama zisizofanana na kipato chake halali!

Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?

mkuu hebu ainisha kila kitu ili tuwape taarifa pccb.
 
Mimi siku zote napenda kuingia hivi!! Kama ifuatavyo
HII TZ MIMI NA IFANANISHA NA FRASH,MEMORYCARD NA EXTERNAL ZINGNE AMBAZO ZIMEJAA MA VIRUS
SASA IMEKUWA KILA SIKU NI KUDELETE TU! HAYA MATROJAN(kujivua gamba) MIMI NIONAVYO BORA KU FORMAT KULIKO KUSCAN NA MA ANT-VIRUS AMBAYO NI NOT UPDATED!!!! Sh***@@##zy kabisa
BORA KUIFORMAT KWA MGOMO NCHI NZIMA
TUANZE KUINGIZA FILES UPYA!
yaani nipo moto acha tu!

nimeipenda
 
CPU imecolapse sababu ya virus sio?
 
HIVYO JIZI KUU LA NCHI HII LINALOWABEBESHA MZIGO WATANZANIA HAMUMFAHAMU AU KWA KUWA ANAKUCHANGIENI KWENYE MATAMASHA, MAJIMBO, UNAPOFIKA NYAKATI ZA UCHAGUZI (CCM NA CDM) NA HATA MISIBA YENU, MBONA HAMUMTAJI ? KUDADADADEK... (wote nyie ndio haohao,ccm,cdm,cuf BABA MMOJA MAMA MMOJA. mmezidiana kete tu..) MNATUPUMBAZA..!!!!!!
Mnawaonea akina Mr Megawati, Nundu, Chami, Mponda, Mkuchika, Maige, Mkulo na Maghembe.
FUATILIENI, NI NANI ANAECHANGIA KTK HAYO NA ZITTO ANAMJUA.
LAKINI HATA SIKU MOJA HAWEZI KUMTAJA WALA KUSEMA LOLOTE KUHUSU HUYO JAMAA.
SI CAG, TAKUKURU WALA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA VINAVYOWEZA KUSEMA UKWELI JUU YA HUYO JAMAA.
Lakini sisi tunaefanya kazi hapa na kutumwa kwenda mara kwa mchina huyu, mara kwe Muhindi huyu na mara kwa Mwarabu huyu kuchukua samsing TUNAUMIA...
 
Lakini tuwe realistic, Ngeleja kawa waziri kwa miaka mingapi? Kwa mshahara na marupurupu ya waziri kweli atashindwa kujenga nyumba ya ghorofa tano? Ofisini kwetu sisi masecretary wanajenga nyumba zao wenyewe. Almost kila secretary ama ana nyumba au ana gari. Sasa itakuwa waziri jamani? Tena waziri ambaye amekaa madarakani kwa muda wa karibu miaka saba. Sasa mnataka hela anayopata afanyie nini? Ndiyo yale yale ya kumwita Sumaye fisadi kisa kanunua shamba la ekari arobaini. Au ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kufanya shughuli za maendeleo binafsi?

Mkuu.. Azimio la Arusha lilikuwa na miiko ya uongozi.. Na moja ya miiko hiyo ilikuwa inamzuia kiongozi wa chama na Serikali kumiliki biashara yeyote.. Iwe ni nyumba ya kulala wageni mpaka kwenye viwanda.. Maana kubwa ya Mwiko huu ilikuwa kuondoa conflict of interest kati ya kuwa kiongozi wa umma na mfanyabiashara.. Hiyo ilipelekea kwa viongozi kuwa vipato vinavyotokana na mishahara yao pamoja na masurufu mengine.. Hii ikaleta viongozi kuulizwa pale wanapoonekana kuwa na kipato au mali za ziada.. Aelezee mali ameipataje na kama ameipata kwa njia halali au la.. Leo Viongozi wanamiliki mali zinazozidi vipato vyao..! Kikubwa hapa kama ni kweli Ngeleja anamiliki hilo ghorofa anaweza litolea maelezo jinci alivyopata pesa za kununulia kiwanja na mwisho kulijenga hilo jengo..?
Nakumbuka Basil Mramba alivyokamatwa aliwakilisha mahakamani hati ya nyumba yenye jina lake yenye thamani ya TShs. bilioni moja na ushee hivi kwa ajili ya kupata dhamana.. Cha ajabu Katika mali zake (Mramba) zilizoorodheshwa serikalini nyumba ile haikuwapo..! Na hakuna aliekaa na kujiuliza alipata wapi uwezo wa kujenga nyumba hiyo..!
Kinacholeta utata hapa Mkuu watujuze tu uwezo waliupata wapi wa kuwa na uwezo huo ilihali ni watumishi wa serikali ambao ukiangalia katika mtiririko wa kawaida sio rahisi.. Inawezekana wamepata kihalali bt ndo watuambie ili tuache kuwawazia mabaya..
 
HIVYO JIZI KUU LA NCHI HII LINALOWABEBESHA MZIGO WATANZANIA HAMUMFAHAMU AU KWA KUWA ANAKUCHANGIENI KWENYE MATAMASHA, MAJIMBO, UNAPOFIKA NYAKATI ZA UCHAGUZI (CCM NA CDM) NA HATA MISIBA YENU, MBONA HAMUMTAJI ? KUDADADADEK... (wote nyie ndio haohao,ccm,cdm,cuf BABA MMOJA MAMA MMOJA. mmezidiana kete tu..) MNATUPUMBAZA..!!!!!!
Mnawaonea akina Mr Megawati, Nundu, Chami, Mponda, Mkuchika, Maige, Mkulo na Maghembe.
FUATILIENI, NI NANI ANAECHANGIA KTK HAYO NA ZITTO ANAMJUA.
LAKINI HATA SIKU MOJA HAWEZI KUMTAJA WALA KUSEMA LOLOTE KUHUSU HUYO JAMAA.
SI CAG, TAKUKURU WALA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA VINAVYOWEZA KUSEMA UKWELI JUU YA HUYO JAMAA.
Lakini sisi tunaefanya kazi hapa na kutumwa kwenda mara kwa mchina huyu, mara kwe Muhindi huyu na mara kwa Mwarabu huyu kuchukua samsing TUNAUMIA...
 
Kwa mshahara wa uwaziri hawezi jenga gorofa pasipo kuiba.
 
Back
Top Bottom