rama bendu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 310
- 220
Ukishatambua diamond ana exposure kuliko darasa utafunga bakuli lako.Hahahahahahahahaha jamani najaribu kufwatilia kwa mbali na kwa karibu hizi hit track mbili yani kokoro ya mavoko na muziki ya darasa, sasa kuna kitu kinanishangaza kokoro imetumia siku 10 kufika 1 milioni view wakati mpaka sasa muziki ina siku 15 lakini haijafikisha 1 milioni view.
Pia hizi nyimbo zinapisha siku moja kutoka yani moja ilitoka tarehe 22 nov na ingine tarehe 23.
Uchawi upo jamani, nyimbo ya Darasa imekuwa namba moja katika trending music tz you tube zaidi ya wiki moja, lakini kokoro hata top teni ya trend haipo lakini inamkimbiza view muziki wa darasa,
jibu ni moja tu nyimbo ya mavoko inaangaliwa sana na sehemu mbalimbali duniani ila nyimbo ya mziki inaangaliwa sana tanzania, so kiufupi watanzania wengi wanaiangalia sana muziki ya darasa kuliko wanavoiangalia kokoro ya mavoko conversely Dunia inaiangalia sana kokoro kuliko inavoiangali muziki ya darasa.
All in all , Hizi track zote ni kali, japo moja ndo imeingiza pesa nyingi kuliko ingine yani kokoro imeuza sana.
Nataka maoni ya watu kwanini nyimbo inatrend lakini inashindwa kuipita view nyimbo ambayo haitrend. Au you tube wanaupendeleo, kwani you tube ni ya clouds, jamani tuchangangie maoni, mimi ni Team Tanzania