Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Here is what I don't understand,wakati unawateua hawa viongozi wanaapa kuwa watiifu katika kulitumikia taifa then wanapovunja uaminifu wao why is so hard for you to take the action against them ni viapo vyao wewe kama rais unafanya kazi yako kwa uadilifu then why you have to think twice,huruma!!!.wao hawakukuhurumia then respond the same way.

If Sahiba become a president the corrupt leaders will hate him but the population will love him to death.I think I won't last for four years.

SAHIBA.
 
- Unajua mkuu Bubu, maneno yako ni sawa sawa, lakini ni lazima sasa Tanzania tukubali kwamba ya kubadili cabinet na kujizulu viongozi wa chini hayajatusadia sana so far as a nation, wakati umefika sasa kwenda mbele zaidi na uwajibikaji, majuzi kwenye kikao chake cha siri na baadhi ya mawaziri, Muungwana ameambiwa wazi kwamba wamejiuzulu wengi na wengi kuondolewa lakini bado kivuli kipo pale pale, hapa kinacho-miss ni kimoja tu nacho ni huenda ni wakati muafaka wa yeye mwenyewe mkulu wa kaya kujiuzulu au viongozi mafisadi waende mahakamani na wafungwe wakipatikana na makosa.

Maneno murua hayo , kama pamoja na kubadilisha baraza la mawaziri mara tatu sasa na Watanzania kutoona utendaji wowote ule unaoturidhisha, basi mwenye tatizo ni huyo anayewateua hao mawaziri labda hayuko makini na anawateua watu wasio na sifa wala uwezo za kuingia kwenye baraza la mawaziri

-- Lakini huwezi kuwa na utawala wa kuheshimu sheria, kwamba mawaziri wa zamani wako rumande huku nyuma wanatokea mawaziri wako wewe mwenyewe rais kuwatafutia mawakili, sasa tutabadili cabinet mpaka lini na mauza uza kama haya? unaaanza kufikia mahali sasa tuanze kufikiria mbele zaidi ya mawaziri na uwajibikaji!

Naam kama mawaziri wanavurunda kila kukicha na anayewateua haonyeshi kutoridhishwa kwake kwa kuvurunda kwa hao mawaziri wake, basi wa kuwajibika hapa ni Kikwete, ndiyo maana nimewahi kusema hapa jamvini kwetu kwamba ahadi alizotuahidi Watanzania wakati wa kampeni za 2005 hakuna hata moja aliyoitimiza na huu ni mwaka wa nne sasa tangu aingie madarakani.

Kwa maoni yangu kazi imemshinda na CCM inastahili kabisa kuteua mgombea mwingine wa Urais katika uchaguzi wa 2010. Hii dhana ya Rais ni lazima akae madarakani awamu mbili hata kama kuna ushahidi wa kutosha kwamba kazi imemshinda, imepitwa na wakati.
 
Mama Siti Mwinyi alikamatwa na Mrema pale Dar Airport akitokea Z'bar na madini . Kama tujuavyo Z'bar hakuna madini yoyote ana likuwa anayasafirisha nje ya nchi ili akachangamke na kuyauza. Hiyo si siri, pia kulikuwa na ufisadi mwingi tu wakati wa awamu ya pili hiyo si siri. Sasa kudai wakati wa enzi za Nyerere kulikuwa na kunguni wengi na kusahau kunguni waliokuwamo ndani ya awamu ya pili, ya tatu na ya nne ni unafiki wa hali ya juu.

Anamsifia Kikwete kafanya mazuri, sijui mazuri gani aliyoyafanya, maana katika ahadi zake wakati wa kampeni hakuna hata moja aliyoitimiza.

Sasa kwanini ulishindwa kusema yote hayo wakati una-introduce mada na badala yake ume-copy na ku-paste.
 
Wako watu wanalima mchicha, kufunga ng'ombe wa maziwa n.k. hawa wanaishi kwa kipato halali siyo kama wanaotaka uongozi ili wakaitumie Ikulu kufanya uharamia wao na kuwafisadi Watanzania na kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka.

Sasa wewe unaofanya kazi ya Plagiarism hapa una tofauti gani nao ??? Nina uhakika ukipewa nafasi na wewe utafanya kama wafanyavyo.
 
Sasa kwanini ulishindwa kusema yote hayo wakati una-introduce mada na badala yake ume-copy na ku-paste.

Kwani kufanya hivyo ni dhambi!? Tangu lini? Unaweza ukatuma habari toka popote pale na ikawa ni kichocheo cha mjadala kama huu unauona hapa. Halijaharibika neno pamoja na kucopy na kupaste.
 
Kwani kufanya hivyo ni dhambi!? Tangu lini? Unaweza ukatuma habari toka popote pale na ikawa ni kichocheo cha mjadala kama huu unauona hapa. Halijaharibika neno pamoja na kucopy na kupaste.

Hiyo ni dhambi kwa sababu unavunja haki miliki za watu. Mtu anaye-poach habari kutoka website zingine ana tofauti gani na fisadi. Mwandishi ametumia siku nzima kuandaa kazi yake. Na akisha-publish haichukui dakika tano wewe kuivuta. That's not so cool.
 
Hivi unafikiri hao wenye magazeti yao Tanzania hawazioni articles zao mbali mbali zikitumwa hapa jamvini!? Wengine wanaona ufahari mkubwa kuona articles zao zimeanzisha mjadala mkubwa hapa jamvini na huthubutu hata kuchungulia kuona kama articles zao zimeshatundikwa hapa jamvini.

Provided situmii hizo articles zao kuziuza ili kujinufaisha basi hakuna lalam na kama kungekuwa na malamiko basi tungeshayasikia miaka mingi iliyopita maana wanajua lengo la kuweka articles zao hapa ni kujenga na siyo kubomoa. Na siku zote huwa nahakikisha articles zote nazoziweka hapa naonyesha zimetoka katika magazeti gani ya Tanzania.
 
Mwinyi kama kawaida yake analeta hadithi nyingi na viswahili vingi bila ya kuwa na umakini wowote, matamshi yake yanaleta maswali mengi zaidi ya majibu.

Huyo Spika naye katika kutaka muungano wa kulazimishwa miongoni mwa wapinzani anaitukanisha dhana nzima ya demokrasia.Unataka wapinzani waungane hata kama hawana sera zinazofanana? Hata wakiungana na kuishinda CCM kutakuwa na mgongano katika kutawala.

Tumeshazoea kuwa na standards ndogo katika pub lic discourse, ama sivyo waandishi wa habari wangewatafuna Mwinyi na Sitta.
 
Hiyo ni dhambi kwa sababu unavunja haki miliki za watu. Mtu anaye-poach habari kutoka website zingine ana tofauti gani na fisadi. Mwandishi ametumia siku nzima kuandaa kazi yake. Na akisha-publish haichukui dakika tano wewe kuivuta. That's not so cool.

Zakumi unaweza kuipa nguvu hoja yako kwa kuweka vifungu vya hakimiliki kutoka magazeti haya?

Bubu un aweza kuweka links za habari hizi? Waandishi wengi ukiweka link inakuwa unawaongezea traffic kwenye sites zao, that's the least you can do while opy pasting.
 
Hivi unafikiri hao wenye magazeti yao Tanzania hawazioni articles zao mbali mbali zikitumwa hapa jamvini!? Wengine wanaona ufahari mkubwa kuona articles zao zimeanzisha mjadala mkubwa hapa jamvini na huthubutu hata kuchungulia kuona kama articles zao zimeshatundikwa hapa jamvini.

Provided situmii hizo articles zao kuziuza ili kujinufaisha basi hakuna lalam na kama kungekuwa na malamiko basi tungeshayasikia miaka mingi iliyopita maana wanajua lengo la kuweka articles zao hapa ni kujenga na siyo kubomoa. Na sikun zote huwa nahakikisha articles zote nazoziweka hapa naonyesha zimetoka katika magazeti gani ya Tanzania.

Wewe unataka kutetea mazoea yako ya kifisadi. Nenda kwenye therapy.

Hata wananchi wa Tanzania wanaona ufahari kwa kuwachagua viongozi wanaowapa pilau zinazotokana na ufisadi.
 
Zakumi unaweza kuipa nguvu hoja yako kwa kuweka vifungu vya hakimiliki kutoka magazeti haya?

Bubu un aweza kuweka links za habari hizi? Waandishi wengi ukiweka link inakuwa unawaongezea traffic kwenye sites zao, that's the least you can do while opy pasting.

Traffic zinaongeza hits ambazo zinaongeza matangazo ya biashara katika site hizo na mapato.

Hivyo kutoka katika business na innovation point of views bubu anawarudisha watu nyuma.
 
Traffic zinaongeza hits ambazo zinaongeza matangazo ya biashara katika site hizo na mapato.

Hivyo kutoka katika business na innovation point of views bubu anawarudisha watu nyuma.

Nadhani wenyewe wanaweza pia kulalamika maana hapa JF is where we dare to talk openly kama waandishi wa magazeti mbali mbali ya Tanzania wakilalamika kwamba kwa kuweka articles zao hapa jamvini ninawarudisha nyuma basi nitaacha mara moja kufanya hivyo. Wamo waandishi wengi hapa wanaosoma mijadala moto moto inayoendelea hapa ukumbini, tunawaomba msinyamaze.
 
Traffic zinaongeza hits ambazo zinaongeza matangazo ya biashara katika site hizo na mapato.

Hivyo kutoka katika business na innovation point of views bubu anawarudisha watu nyuma.

Kwa kifupi unasema umeshindwa kuipa nguvu hoja yako kwa kutupa vifungu mahsusi vya hakimiliki kutoka magazeti hayo vinavyokataza copy paste.Kuna kitu kinaitwa copyleft na open source movement, ambapo mtu mwenye kuanzisha jambo/ kuprogram software/ kuandika article anatoa ruhusa kwa watu wengine kutumia article/ software etc ili mradi wasiitumie kibiashara.

Unaweza kutuhakikishia kuwa wanahabari hawa hawako katika mfumo kama huu kwa kutuletea vifungu vya sera zao kuhusu hakimiliki?

Kwa umakini zaidi inabidi tuende na ushahidi pamoja na documents, sio kwa kufikiri fikiri tu.
 
Mzee Mwinyi ni kunguni mwingine tu aliyetafuna taifa. Yeye na mkewe ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha biashara Ikulu, wakituuzia Stella Artois na majenereta ya umeme. Sasa anasema nini kuhusu kunguni? It takes one to know one.

...dah,

...nikikumbukia miaka ile, bora Mzee Ruksa aliyeanzisha biashara ikulu. kwa hali ilivyokuwa, ilibidi huyu mzee anywe nao chai ikulu kuwarudishia imani wafanyabiashara badala ya zile enzi tulivyokuwa tuna tafuna mpaka dola moja ya mmarekani tusijekamatwa ulanguzi uchumi!

...maisha gani yale ya kujivunia, eti mtu akitoka safari zawadi kuuubwa ni sabuni ya Lifebuoy, Lux, Imperial leather au Colgate? ...tuliokogea sabuni za 'magwanji' cha moto tulikiona kwa muasho.

...Basi mpaka nyembe ya Topaz nayo ilikuwa ngumu kuipata? maduka yamejaa vibiriti na majani ya chai tu?...

...yaani ilifikia hata shuleni, watoto wanavaa katambuga na mashati ya 'maradufu'? umasikini gani ule? Ukibahatika kuvaa shati la tetroni basi usipite karibu na moto.

...Kwa waliopitia boarding school nadhani mtakumbuka full-suit, ...enhe ule ugali wa yanga na dengu! huchelewi kutoka povu kinywani ukiufakamia!

...kuletwa Stella Artois angalau basi watu walipata vionjo vipya badala ya Pilsner, Safari, Ndovu na Kilimanjaro wakati huo, maana hang-over za hizo beer ukiamka umeze tembe.

...angalau basi hayo majenereta ya umeme yalikuja'tufaa majumbani badala ya mishumaa ambayo pia ilikuwa kimeo! ajabu yenyewe hata sukari ya nchini ilikuwa kimeo kuipata, wananchi tukalazimika kunywa chai na sukari guru.

...sioni tofauti ya Tanzania ya wakati ule na yanayowakumba wazimbabwe huko nchini kwao sasa.

...acheni nyie bwana, Mzee Ruksa pamoja na mapungufu yake (yalokuwa nje ya uwezo wake), ametukomboa!
 
Last edited:
Hivi DDT au Expel. or Doom haziu kunguni? si mzee Ruksa angewapulizia hiyo dawa kunguni wangekufa. ( kwanini hakuchukua hatua za kuwa maliza kunguni?)
 
Hivi DDT au Expel. or Doom haziu kunguni? si mzee Ruksa angewapulizia hiyo dawa kunguni wangekufa. ( kwanini hakuchukua hatua za kuwa maliza kunguni?)

Ha ha ha!

Hawa walikuwa wengi mno!

Na isitoshe hawakusikia dawa hata walipopuliziwa!
 
Alisema wapinzani sio maadui, na kwamba Watanzania walikubali wenyewe mfumo wa vyama vingi, yeye akiwa mwasisi wa mfumo huo, licha ya kwamba asilimia 80 walikuwa wameukataa maoni ya asilimia 20 ya watu waliohojiwa yalikubaliwa.

Lakini rais huyo mstaafu tangu mwaka 1995, aliwatupia wapinzani dongo la kushindwa kwao kukua: "tangu wakati huo wamebaki na asilimia 20 zao na CCM imebaki na ushindi wake wa asilimia 80," alisema.
Kwanza amekosea kusema Watanzania wenyewe walikubali mfumo wa vyama vingi.. sii kweli ukisoma maelezo baada ya maneno hayo..amesema asilimia 80 walikuwa against vyama vingi huwezi kusema Watanzania wenyewe walikubali..

Na ikiwa asilmia 80 ya wananchi walikataa vyama vingi, na asilimia 20 tu ndio waliokubali inaonyesha wazi kwamba wananchi walitaka kuona CCM ikiendelea kutawala na matokeo ya sasa hivi ni kithibitisho cha wananchi wengi kukataa mfumo wa vyama vyingi kwa asilimia hiyo hiyo... ndio maana wanakichagua chama chao CCM...
Bahati mbaya, hiyo asilimia 20 ndio wenye elimu na mwamko kuhusiana na vyama vingi wakati asilimia 80 ya wananchi ni kabuntas bado wanaamini hakuna chama zaidi ya CCM..

Kazi kweli kweli kufika huko tunakokusudia!
 
Wewe unataka kutetea mazoea yako ya kifisadi. Nenda kwenye therapy.

Hata wananchi wa Tanzania wanaona ufahari kwa kuwachagua viongozi wanaowapa pilau zinazotokana na ufisadi.

LOL!...kuna ufisadi kweli ambao mtu hafaidiki kwa chochote....:) ha ha ha ha!
 
Mkuu hebu tutajie biashara alizomiliki Mwinyi akiwa ikulu na anazomiliki sasa baada ya kuondoka ikulu.Repoti ya Warioba ilishindwa kutaja zaidi ya kuorodhesha kuwa Mwinyi aligawa viwanja bure kwa jamaa zake au hiyo ndio biashara ?

Anayo ardhi kubwa sana kule Kingoruhira, Morogoro. Aliipata akiwa Ikuru,hivyo aliipata kwa kutumia kofia ya jumba hilo. Ni ardhi kubwa isiyotumika ambayo wangepewa wawekezaji ikalimwa na kutatua tatizo la njaa nchini.

Back
Top Bottom