Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Mchungaji mbona umeshajijibu mwenyewe. Mawazo ya Mwalimu Nyerere ni matokeo ya kile ambacho Profesa Ali Mazrui anakiita 'Africa - A Triple Heritage', yaani 'Urithi wa Afrika Kutoka Sehemu Tatu' sehemu hizi ni Afrika-Asilia, Asia-Arabuni na Uropa-Amerika. Hivyo basi, ni sahihi kabisa kusema kuwa Mwalimu alichanganya madesa yote matatu ndio maana kale kajitabu kake kwa mwaka 1962 kanakoitwa 'Ujamaa - The Basis of African Socialism', yaani 'Ujamaa- Msingi wa Usoshalisti wa Kiafrika', kanaonesha mambo tuliyoyarithi katika jamii ya Kiafrika/Kitanzania yanavyoweza kutumia ufahamu/teknolojia kutoka ...
Nyerere alichanganya madawa tu. Vitabu na falsafa yake ilitokana na mtazamo wake bila kufanya utafiti wa kutosha.
Angefanya utafiti wa kutosha asingeandika ujamaa. Kwa sababu hakuna kitu kinachoitwa ushoshalisti wa Kiafrika. Kuna ushoshalisti tu.
Na misingi aliyotumia kuandika au kujenga ujamaa sio misingi unique kwa Afrika peke yake. Hile ni misingi ya primitive life style. Hata wazungu walipokuwa katika primitive life style walisaidiana katika masuala mengi.
Hivyo basi ukiona waafrika wanasaidiana kuombana chumvi basi isifikiriwe kuwa wanaweza kutumia ushirikiano wao wa kuombana chumvi kutengeneza space ship rocket.