Wewe ni mfugaji? Uliza swali lolote la kitaalam nikusaidie

Nimekuwa nikifuga sana kuku wa kienyeji na kuwapa madawa lakini wanakufa sana na sipati faida Naomba unisadie kwa hilo asante

Katika ufugaji wa kuku kunahitaji umakini sana maana kuku ni wepesi sana wa kupata magonjwa na magonjwa hayo mengi yao yanakua makali sana hivyo mkulima unashauriwa kutoa chanjo kwa kila kuku kwa yale magonjwa ambayo ni common katika eneo ulilopo pia hakikisha unawalisha vizuri pamoja na usafi wa banda, hakika ukifanya hivyo utanufaika sana.

Pia unaweza chukua mzoga wa kuku alie kufa ukampelekea mtaalamu uliopo karibu nawe
kuona ni maradhi gani haswa yanawapata kuku wako ili hata dawa utakazotumia ziwe sahihi pale endapo wataugua tena.
 
shukrani sana kwa kujitolea
eti unaweza kunifafanulia huu ufugaji wa kuku wa mayai kwa kutumia battery cages
kuanzia kuku wanapokua vifaranga hadi wanapoanza kutaga na gharama za kuwalisha wakiwa wanataga na mapato yake kwa wastani
idadi ya kuku ni 500
 
Nishauri juu ya aina bora ya mbuzi kwa ajili ya nyama,wenye kukua haraka na kilo nyingi,na wapi ntawapata
 
Kwanza nitoe shukran kwa kushare nasi taalum yako kwa kuruhusu maswali.

Ningelipenda kujua,ninatarajia kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji ,vitu gan mhm vya kuanza navyo ukiachana na banda? atleast nianze na kuku wangapi?

Hapa nilipo ugonjwa wa kuku unaosumbua sana ni wa kuku kunya kinyes cheupe pee,na kutoa udenda mdomon mara ukimshika kichwa chin miguu juu.

kwa vifaranga huwa vinakohoa na kujenga kibanda yaan anakuwa kama mtu anayehis barid.

utakuwa umenisaidia san ukinitoa umande juu ya hili,
Natanguliza shukran.
 
shukrani sana kwa kujitolea
eti unaweza kunifafanulia huu ufugaji wa kuku wa mayai kwa kutumia battery cages
kuanzia kuku wanapokua vifaranga hadi wanapoanza kutaga na gharama za kuwalisha wakiwa wanataga na mapato yake kwa wastani
idadi ya kuku ni 500

ufugaji wa kuku kwa kutumia battery cagez unafaida kama inakuitaji uwe na eneo dogo haina ulazima wa eneo kubwa pia ugawaji wa chakula ni rahisi na kwa kuku wanaotaga uwa rahisi kukusanya mayai hivyo nakushauli kuendelea kutumia hii njia na pia kuhusu chakula hakikisha kila kuku anakula gram 130 yenye mchanganyo uliokamilika na maji kila muda

nazan utakua umeelewa lakin kama bhado ujalizika tuwasiliane kwa namba 0753160392
 
Kwanza nitoe shukran kwa kushare nasi taalum yako kwa kuruhusu maswali.

Ningelipenda kujua,ninatarajia kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji ,vitu gan mhm vya kuanza navyo ukiachana na banda? atleast nianze na kuku wangapi?

Hapa nilipo ugonjwa wa kuku unaosumbua sana ni wa kuku kunya kinyes cheupe pee,na kutoa udenda mdomon mara ukimshika kichwa chin miguu juu.

kwa vifaranga huwa vinakohoa na kujenga kibanda yaan anakuwa kama mtu anayehis barid.

utakuwa umenisaidia san ukinitoa umande juu ya hili,
Natanguliza shukran.

kuku wakuanzia inategenea na mtaji ulio nao ni upi na pia katika ufugaji wa kuku gharama zaidi zipo katika chakula hivyo nakushaur angalia mtaji ulionao zen tuwasiliane #O753160392
 
Kwanza nitoe shukran kwa kushare nasi taalum yako kwa kuruhusu maswali.

Ningelipenda kujua,ninatarajia kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji ,vitu gan mhm vya kuanza navyo ukiachana na banda? atleast nianze na kuku wangapi?

Hapa nilipo ugonjwa wa kuku unaosumbua sana ni wa kuku kunya kinyes cheupe pee,na kutoa udenda mdomon mara ukimshika kichwa chin miguu juu.

kwa vifaranga huwa vinakohoa na kujenga kibanda yaan anakuwa kama mtu anayehis barid.

utakuwa umenisaidia san ukinitoa umande juu ya hili,
Natanguliza shukran.

kuhusu huo ugonjwa jitaid saana kuwachanja kuku wako maana niugonjwa hatar kwa kuku;
mtafute mtaalamu aliopo karibu na ww kukuelekeza namna yakuchanja na chanjo yenyewe ni ugonjwa unaiitwa gumboro pia kwa hao vifaranga nakushaur pia mtafute mtaalamu aliopo karibu nawee ili kuutibu na kuuzuia katika banda lako
 
  • Thanks
Reactions: Php
Nina kuku 30 na vifaranga 23 walikuwa wanarandaranda kujitafutia chakula wenyewe na chakula ni kingi tu kwani kuna mashine za unga hapo hapo,
Sasa nimeamua kuwafungia kwenye banda na kuwapa chakula humo humo Je ni idea nzuri?

Swali lingine Je naweza kuongeza mitetea ingawa naogopa maradhi yao
 
ni idea nzur sio mbaya hakikisha unawaangalia kila mara kutazama maendeleo yao pia kuhusu kuchanganya aina tofauti za kuku binafsi sikushaur ufanye hivo kwamaana unaweza sababisha mlipuko wamagonjwa na kama ukiitaji kuwachanganya fanya hivyoo bhas anza kuwachanganya wakiwa wadogo saana
 
Nataka kuwa na large scale goat farming.

Niambie nifanye nini ili nifanikiwe?
 
ufugaji wa kuku kwa kutumia battery cagez unafaida kama inakuitaji uwe na eneo dogo haina ulazima wa eneo kubwa pia ugawaji wa chakula ni rahisi na kwa kuku wanaotaga uwa rahisi kukusanya mayai hivyo nakushauli kuendelea kutumia hii njia na pia kuhusu chakula hakikisha kila kuku anakula gram 130 yenye mchanganyo uliokamilika na maji kila muda

nazan utakua umeelewa lakin kama bhado ujalizika tuwasiliane kwa namba 0753160392
battery cage inafaa kwa kuku wa kinyeji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom