Wenye wanaume walokole tukutane hapa

Veronica7598

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
361
408
Aman iwe kwenu wapendwa,

Leo nataka nizungumze na wanawake wenzangu ambao wameolewa na wanaume washika dini (walokole) sjui kwa waislam wanaitwaje.

Binafsi namshukuru Mungu nimeolewa na mwanaume mshika dini tena mwenye hofu ya Mungu. Nimekua na maisha yenye furaha maana mimi na hubby wangu wote tunahofu ya Mungu.

Kwakweli tangia niingie kwenye ndoa sijawahi kujuta na tumekua waaminifu sana japo wanasema usimwamini mwanaume lakini huyu wa kwangu. Namshukuru Mungu si mpenda anasa tena muwazi kwa kila kitu. Pesa yake ya kwangu, changu ni chake.

Japo changamoto ni nyingi ukiangalia bado sisi ni vijana Mungu ni mwema tutazishinda.

Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu ambao hamjaolewa tulieni. Acheni kuchagua sna mwanaume wa kuoa wewe weka sharti awe mcha Mungu. Mambo mengine atatafuta baadae sio mnakimbilia mwanaume mwenye pesa, sijui alie soma.

Mkitaka ndoa yenye amani na upendo daima, wote muwe mnahofu ya Mungu.

Ahsante
 
Back
Top Bottom