A
Anonymous
Guest
Umoja wa Watoa Huduma Sekta ya Binafsi APHTA, Mashirika ya Dini (CSSC), na Bakwata wanapenda kutaarifu umma kuwa mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika baina ya umoja huo na Wizara ya Afya. Kamati ya Waziri na NHIF yameshindwa kupata muafaka katika suala zima la kitita cha bei mpya zilizopendekezwa na Wizara kupitia kamati iliyoundwa na Waziri.
Kwa kuwa Wizara pamoja na NHIF wameamua kudharau maagizo yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya namna bora ya kumaliza suala hilo na kuamua kutangaza kitita hicho bila maridhiano, basi umma unatangaziwa kuwa vituo binafsi vya huduma za afya vitashindwa kutoa huduma hizo kwa wanachama wa Mfuko huo kuanzia tarehe 1 mwezi Machi 2024.
Ili kuepuka usumbufu, wanachama wa NHIF wanaombwa kuwasiliana na Mfuko wapi wataweza kupata huduma hizo.
Suala la hili limekuja baada ya Wizara ya Afya kutoa barua ya kuendelea na vifurushi vyao kwenye barua iliyoandikwa 27/02/2024.
Barua ilisema "Hivyo, Mfuko unapenda kukufahamisha kuwa utatumia Kitita cha Mafao cha Mwaka 2023 kuanzia tarehe 01.03.2024. Vilevile, unafamishwa kuwa, orodha ya huduma na bei katika Kitita hicho zinapatikana katika ofisi zote za Mfuko, tovuti ya Mfuko na kupitia mfumo wa Service Porta/. Aidha, Mfuko utaendelea kupokea maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa wanufaika wake na kuendelea kuishauri Serikali ipasavyo."
Pia soma - APHFTA: Tutasitisha huduma za NHIF kuanzia saa sita usiku, wagonjwa mahututi tutawaongezea saa 48