Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

Hakuna lolote ni ghiliba za kisiasa kuwanyima wanafunzi fursa ya kufanya maamuzi wanayoyataka.Kwa jimbo kama la Ubungo lenye upinzani mkubwa sana kwa C.C.M inawalazimu kusogeza mbele tarehe ya kufungua maana wanafunzi wakiwepo ni dhahiri watashindwa tu.Hivyo hii yote ni mikakati ya kufanya hila kwenye maeneo wanayoona wana upinzani mkubwa.
 
ni ushenzi ulio tukuka
sijawahi ona hii maishani,hivi hawa watu wana akili kweli?
maamuzi gani haya ya ki*&&@:>> namna hii,kwahiyo unanyima wanafunzi haki ya kupiga kura ki namna hii kweli?

niliposikia hii news nikajikuta tu naongea peke yangu,sikuamini maskio
 
sababu ya kizembe sana hii uyu maghembe!!
aisee hili ni kosa la jinai,sasa watu si wamekosa kupiga kura?
maana ata raia wa kawaida wapo waliojiandikisha pale (majority wanafunzi)
 
Huu ni Use***&^^%&**(% e hapa ningekuwa na bastola ningemmaliza maghembe use&&^%*())))(&%$£"%^*&*(( wake
 
MKuu huu ni maongo wa CCM kuzoofisha Upinzani, 2005 nilikuwa na watoto wangu pale UDSM but hawakupiga kula mana waliambiwa majina yao hayapo kwenye daftari la wapiga kura.

CCM imeona Mnyika wa Ubungo atashinda lakini hapa wanatengenezea mizengwe hili akose kula za UDSM. 2005 80% ya wanachuo walikuwa namusupport JOhn Mnyika


NB: JOHN MNYIKA KUWA MAKINI KWA HILI KURA ZAKO ZINAPOTEA

Hili tatizo sio kwa Dar es salaam tu. Dodoma nako, Iringa, Mwanza, Morogoro na kwingineko ni tatizo kubwa kwa ccm kushinda. Kizazi kipya kinaamini katika mabadiliko. Siku hizi ccm wanaringia vijijini kuliko na wananchi wengi wasiokuwa na uelewa mpana. Matokeo yake wakivifunga hivi vyuo vyenye wapiga kura zaidi ya 20,000 kila kimoja itapunguza sana makali ya upinzani na kuzuia umma wa Watanzania kufanya mabadiliko kwa umoja wao.
Hili haliwezi kukubalika hata kidogo, lazima vyuo vyote vifunguliwe kwa wakati ili wanachuo waweze kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wao.

Chiligati Busanda aliwahi kusema: Magazeti na TV havifiki kijijijini na hata vikifika hakuna mwenye uwezo wa kununa hayo magazeti, na huko vijijini hakuna umeme ili watu waweze kuyaona yanayoendelea kwenye TV. Kwa maana hiyo, ccm hapa inatumia mbinu ya kuwarudisha wasomi huko vijijini kusikokuwa na magazeti wala umeme hadi watakapokuwa wamejihakikishia ushindi. Hili halikubaliki hata kidogo
 
twende mbele turudi nyuma
1.sheria inasemaje kuhusu haki ya mtu kupiga kura?
2.na je hili tangazo la uyu meghembe limetoka muda upi hasa?
3.maana athari ni kubwa ya kunyima "kimakusudi"watu maelfu kupiga kura katika kituo walichojiandikisha,
4.maana daftari la kujiandikisha lishafungwa nchi zima except dar 2 days-marudio
5.naamini watakaoathirika majority ni wasomi wa elimu za juu ambao sheria wanaijua na wanauwezo wa kufatilia ili wapate haki yao ya msingi(kumbuka hawatapiga kura sehemu yoyote ile)
6.je hii ni kesi ya mahakama na je ina uwezo wa kuzuia agizo hili la waziri uchwara?
7.ivi unawezaje kiongozi mzima unasimama na weak sentences za kusogeza mwaka wa masomo nchi zima kihivi?bila sababu ya msingi au NJIA MBADALA YA HAWA WATU WAPIGE KURA WAPI SASA??
8.rais najua hatuna wala maamuzi amgumu kama suala hili lililokaa,hawezi ongelea zaidi ya kukomaa na mishahara/kura za wafanyakazi laki 3
9.NAAMINI SERIKALI ZA WANAFUNZI VYUONI WATACHUKUA HATUA,PIA WAHADHIRI WAO
10.nimemaliza chuo ila ningekuwepo,KUNJI LA NGUVU LA WANAFUNZI LINGETOKEA KIELEWEKE

:angry:
 
Mimi nafikiri hoja ni rahisi na serikali kamwe isitumie umasikini wa wanafunzi kuwanyima haki yao. Mimi napendekeza kuwa kama serikali itakuwa haiko tayari kutoa hizo fedha basi wanafunzi waambiwe tu kuwa waende vyuoni mapema lakini wajiandae kusubiri hayo malipo kwa muda. Watanzania tumezoea shida haitaathiri sana hasa wanafunzi wakijawa na moyo wa mapinduzi wa kukubali kuvumilia ili tu wahusike katika kuupatia upinzani nguvu zaidi. Wana mapinduzi wanakaa misituni, sembuse kucheleweshewa posho tu.

Watanzania tuamke, mapindizi ya kweli yanakuja kwa wachache kutoa kafara.
 
Ingekuwa ni kwa shule za msingi ingeeleweka kwa sababu walimu mara nyingi ndio wanakuwa wasimamizi wa kupiga kura sasa kwa vyuo vikuu inasikitisha sana.
 
Kutokana na waraka ambao unasemekana umesambazwa kwenye vyuo vya Elimu ya juu kuelekeza vyuo kufunguliwa baada ya Uchaguzi Mkuu wanachuo wengi wanaweza wasipige kura. Is this fair?

Habari kamili

Mnyika ahoji waraka wa serikali
 
Mnyika ahoji waraka wa serikali


na Lucy Ngowi


amka2.gif

MKURUGENZI wa Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameitaka serikali kueleza wazi sababu za kutoa waraka kwa vyuo vikuu kutofunguliwa wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Mnyika ambaye ametangaza nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Ubungo, alisema hatua hiyo ya serikali inaweza kuikosesha Jumuiya ya Vyuo Vikuu, fursa ya kupiga kura kama ilivyokuwa katika miaka mingine.

"Wakazi wa Mtaa wa Chuo Kikuu walinieleza kuwa wana taarifa kuwa serikali imetoa waraka kwa vyuo kutofunguliwa wakati wa Uchaguzi Mkuu, hali inayoweza kuwakosesha fursa ya kupiga kura Jimbo la Ubungo kama ilivyokuwa kwa miaka mingine," alisema Mnyika.

Alisema mbali na kero hiyo ya vyuo kufungwa, wakazi wa jimbo hilo, walieleza kero nyingine ni ya wakazi eneo la Ubungo Maziwa kaya 137 ambao nyumba zao ziko karibu na maeneo hatari ya mitambo ya gesi, bado hawajalipwa fidia zao tangu mwaka 2004. Alisema kutokana na kero hiyo, anaitaka serikali itoe tamko rasmi kwamba ni lini watalipwa fidia, kwani eneo hilo liliwahi kupata ajali ya kuwaka moto mitambo ya TANESCO mwaka 2003.
 
Taarifa za uhakika kutoka kwa wakuu wa vyuo vikuu zinaeleza kwamba, wametaarifiwa rasmi kwamba muhula ujao wa masomo utaanza mwishoni mwa mwezi Novemba 2010. Hiyo itakuwa ni baada ya siku ya kupiga kura.

Kisingizio ni bajeti lakini yaonekana ni kuogopa kupoteza majimbo yaliyoko ktk miji yenye vyuo, Dar, Mwanza, Morogoro, Dodoma. Kwa idadi kubwa ya wanafunzi walioko ktk vyuo hivyo, na kwa uelewa wa wanafunzi, inaonekana watawala wanaanza kuhofia uamuzi wa wanafunzi ktk miji hiyo.

Pamoja na hali hii ambayo watawala wataiita "ujanja", ni aibu kwamba bado tunategemea ujinga ili kupata madaraka badala ya ufahamu. Sasa siasa inazidi kuharibu mipango ya elimu.
 
Taarifa za uhakika kutoka kwa wakuu wa vyuo vikuu zinaeleza kwamba, wametaarifiwa rasmi kwamba muhula ujao wa masomo utaanza mwishoni mwa mwezi Novemba 2010. Hiyo itakuwa ni baada ya siku ya kupiga kura.

Kisingizio ni bajeti lakini yaonekana ni kuogopa kupoteza majimbo yaliyoko ktk miji yenye vyuo, Dar, Mwanza, Morogoro, Dodoma. Kwa idadi kubwa ya wanafunzi walioko ktk vyuo hivyo, na kwa uelewa wa wanafunzi, inaonekana watawala wanaanza kuhofia uamuzi wa wanafunzi ktk miji hiyo.

Pamoja na hali hii ambayo watawala wataiita "ujanja", ni aibu kwamba bado tunategemea ujinga ili kupata madaraka badala ya ufahamu. Sasa siasa inazidi kuharibu mipango ya elimu.

Kama hii ni kweli
Basi kweli huu ni ujinga uliopitiliza
 

Pamoja na hali hii ambayo watawala wataiita "ujanja", ni aibu kwamba bado tunategemea ujinga ili kupata madaraka badala ya ufahamu. Sasa siasa inazidi kuharibu mipango ya elimu.


Inasikitisha kweli kweli! Upande mwingine vijana mtakaporudi makwenu itangazeni habari njema ya ukombozi wa Tz kwamba bila kuing'oa madarakani serikali ya cc em hatuvuka ng'ambo ya yorodani! Wametuhakikishia hilo baada ya kushindwa kuleta maendeleo kwa zaidi ya miaka 50 waliokaa madarakani!
 
Hii ni kawaida kwa CCM wakiona kuna upinzani mkali. Mwaka 1995 walifanya hivyo kwa sababu walijua mzee ruksa alikuwa ameharibu na mrema alikuwa anawapeleka puta. Safari hii CCM na watawala wake wanaihofia CHADEMA ndiyo maana wanaamua kutofungua vyuo.

Katika raundi ya kwa za mwaka 1995 CCM ilipoteza viti vyote Dar lakini walipogundua hilo wakafuta matokeo na kurudia uchaguzi kitu kilicho wafanya baadhi ya wananchi wawe wametupa vikadi vya kupigia kura, japo hilo leo haliwezekani kwani kadi ni za kudumu.

CCM wanatumia mtaji wa ujinga wa wananchi ili watawale na ndiyo maana hawaoni aibu kuwalalza akina mama wazazi chini kwenye sakafu ktk mahospitali.
 
Kuna uthibitiisho kuwa mwaka huu vyuo vikuu vyote vitaanza mwaka wa masomo mpya mwezi wa kumi na moja soon after uchaguzi. wachambuzi wanasema hi ni janja ya CCM kuzuia wanachuo wasipige kura kwani wengi si wana CCM, na wengi wangepigia upinzani. wanajua fika wengi wamejiandikisha maeneo ya chuoni. jamani mbona wanawanyima watu haki ya kupiga kura? I hate being tanzanian and live here, am strugling to go and live abroad where life there make sense.
 
Remmy, ni kweli hiyo hata mimi nimeisikia, lakini ndugu yangu remmy kukimbia tatizo sio dawa ya kulitatua wewe unataka kukimbia TZ ! tunawahitaji watu kama ninyi hapa nyumbani ili tusaidiane kuuondoa uozo huu, sasa kila mmoja akikimbia TZ yenye asali na maziwa italetwa na nani? tunahitaji kuunganisha nguvu ndugu sio kukimbia!
 
Kuna uthibitiisho kuwa mwaka huu vyuo vikuu vyote vitaanza mwaka wa masomo mpya mwezi wa kumi na moja soon after uchaguzi. wachambuzi wanasema hi ni janja ya CCM kuzuia wanachuo wasipige kura kwani wengi si wana CCM, na wengi wangepigia upinzani. wanajua fika wengi wamejiandikisha maeneo ya chuoni. jamani mbona wanawanyima watu haki ya kupiga kura? I hate being tanzanian and live here, am strugling to go and live abroad where life there make sense.
Duu,

Mkuu ukimbie nchi yako kisa? Acha hizo bana.. Tanzania is a very beautiful country na ninawashangaa sana watanzania wanaoichukia nchi hii.

Hata kama nchi hii unaiona mbaya vipi lakini naamini uki-struggle vya kutosha utakuwa na masiha mazuri tu..Ni watanzania wangapi walioko hapa Tz wanamaisha mazuri na ni watanzania wangapi walioko nchi za watu wanaishi kwa shida pamoja na elimu zao nzuri?..

Nikirudi kwa suala la Serikali na kufunga vyuo kwa kweli hawatendi haki hata kidogo..Mimi ningeku

wa bado niko chuoni ningeoongoza mgomo wa kuitafuta hii haki ambayo wakati mwnigine serikali hii imekuwa ikisisitiza kuwa ni haki ya msingi ya kikatiba hivyo kila mtu ni muhimu akapiga kura..
 
Kilembwe, sometimes is better to run from a problem than speaking with a deaf, dictator like our government. na wakati mwingine unaona bwana mkubwa anapewa tuzo ya utawala bora tena from outside countries, nabaki nashangaa na kushindwa kushangaa
 
Back
Top Bottom