Wana haki ya kutoa mawazo yao kama ambavyo nao waislamu wametoa tamko lao. .
Umesema vizuri sana. Kwani huyo Chitanda ni dhehebu gani? Na kwanini yeye na familia yake wasitengwe na kanisa kwa kukosa adabu hadi hapo atakapo tubu dhambi zake?
Majani!!AFRICAN MOVEMENT FOR THE RESTORATION OF THE TEN COMMANDMENDS CHURCH..BABA ASKOFU JOSEPH KIBWETERE, kwa imani bwana yesu amefanya mauaji ya kinyama sana zaidi ya watu 1000 walikufa ikiwamo miili ya watoto 11 iliyoungua na moto kutokana na tukio hilo, uchunguzì wa polisi wa uganda wamegundua baadhi wamepewa sumu wengine walikuwa wemenyongwa na wengi walikuwa na alama za kuchomwa na vitu vya ncha kali, mafuvu yalikuwa yamepasuka na na kutupwa kwenye visima na vyoo vya mashimo.NGUVU ZA MASKOFU
well Chitanda alisema wajihusishe na kukemea maovu TUUUUUUUUUUU! Hivi unajiuliza, uuaji wa raia namna ya Arusha si uovu huo? Na viongozi wasikemee hilo pia?
Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Dini fulani mkoani Arusha kupinga tamko la Maaskofu walilolitoa baada ya kotokea vurugu mkoani Arusha. Pamoja na shutuma nyingi, maaskofu hao wametakiwa kujitenga na mambo ya kisiasa badala yake wajihusishe tu na Mambo ya kiroho na si vinginevyo!
Ni rahisi sana kutoa tamko la namna hiyo kama huna muda wa kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe kujua sababu za maana zilizosababisha Maaskofu kutoka kwenye makanisa yao na kuingilia moja kwa moja mambo ya kisiasa hususan sakata la Meya wa Arusha.
Maaskofu hawa walikuwa na sababu za msingi kabisa kumpinga Meya wa mji wa Arusha kutokana na sababu kadha wa kadha. Zaidi ya Asilimila 70 za huduma za kijamii kama Hospitali, shule achilia mbali miradi ya maji n.k Mkoani Arusha tu zinamilikiwa na kanisa. Kanisa limekuwa halina ubaguzi wa Kidini katika utoaji wa huduma zake hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi na serikali. Kwa miaka mingi tumeshuhudia kanisa likifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na tabu zisizo za lazima kwa kujihusisha moja kwa moja na shida za jamii. Kanisa la Tanzania limekuwa likithubutu hata kushawishi nchi mbalimbali kama Ujerumani, Uingereza n.k kuziomba zitusamehe madeni, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Tanzania anapata nafuu bila kujali chama, dini au rangi. Hivi harakati zote hizi nilizotaja sio siasa hizi? Iweje suala dogo la kumpinga meya liwaondoe wanaharakati hawa katika siasa?
Nimeamua kuyaweka maelezo hayo machache ili nikufikirishe utambue umuhimu wa kanisa katika Nchi hii. Kimsingi MEYA wa jiji la Arusha hawezi kujitenga na kanisa kwa namna yote ile kwani kwa kiasi kikubwa kanisa linategemea kiongozi wa kisiasa ambaye kwa pamoja watashirikiana bega kwa bega ili kuendeleza zile juhudi kubwa zilizofikiwa na ambazo ni changamoto kwa maendeleo ya wanachi wa Mkoani humo. Huwezi kumtoa Askofu katika siasa, maana kwa upana wake siasa inagusa maisha ya kila siku kwa kila mtu, Askofu anahitaji Amani, maendeleo pamoja na huduma muhimu.aidha ieleweke wazi kuwa kazi ya kanisa si kutoa mapepo na kuombea wagonjwa tu, bali pamoja na hayo ni kuhakikisha kuwa maisha ya kawaida kwa maana ya mahitaji ya kimwili yanaguswa kwa namna mbalimbali.
Unapomwambia Askofu ajitenge na na siasa ni kwamba Wavunje Hospitali zao za Rufaa? Shule zao zinazofanya vizuri na kuzalisha watu wenye akili? Wavunje vyuo vyao ambavyo ni vingi kushinda vya serikali? Wasihoji vile visima vyao vya maji na miradi ya umwagiliaji? Hapana!!!. Nafikiri kuna maeneo ambayo Viongozi hawa inabidi wahoji na kukosoa wanasiasa ili vile ambavyo walibuni na kuhakikisha kuwa vinawasaidia wananchi wakiwamo waumini wao havisimamiwi na viongozi wabovu au viongozi ambao kwa nia moja au nyingine wanania mbadala na isiokubalika kwa wananchi wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa kamwe hawatakuwa mishumaa ya kuwamulikia watu waovu wakati wao wanateketea. Linapokuja swala la Maaskofu kujiingiza katika siasa Nguvu yao ipo katika Huduma na mambo ya msingi ambayo kama wataamua kumwachia Mungu watu waovu wanaweza kuifikisha Tanzania yetu mahali ambako sio salama. Kiongozi wa kidini ambaye haoni sababu za kujiingiza na kuhoji mambo ya siasa ujue hana cha kupoteza!!!!!!!!!
Anold, umenikumbusha kitu muhimu sana kuhusu kazi za Kanisa na uhusiano na uchumi wa eneo. Miaka ya 1970 na 1980, Padri mmoja mzee kule Maua Moshi alianza kuona chemichemi alimokuwa ametegeshia pump za maji kwa ajili ya shule ya seminari na majirani zilikuwa zinaanza kukaukia. Akagundua tatizo ni ukataji wa misitu millimani ambako ndiyo chanzo cha maji. Basi akaamua kuanza kuotesha msitu na amini usiamini kwa kushirikiana na wanafunzi na watu wachache walioajiriwa na kanisa aliotesha msitu wa zaidi ya kilomita mraba 6. Msitu ukakua na vyanzo vya maji vikawa vimeanza kushiba maji.
Mwaka 2004, akiwa anatembea kwenye tafakari maeneo ya seminari yake, aliona malori makubwa makubwa yamebeba miti. Kumbe Afisa Msitu alitoa kibali cha kuvunwa ule msitu aliootesha yule Mzee. Alikimbiza magari yale kwa miguu na kupayuka, akitaka kujua imekuwaje wanavuna msitu! Alikwenda Idara ya Msitu, na wale watendaji wakamshangaa, kwanza yeye ni mzungu halafu anazungumzia uvunaji wa raslimali za kikwetu. Baadaye ilijulikana kuwa ni viongozi wa serikali za mtaa kwa kushirikiana na watendaji waliridhiana kuvuna ule msitu. Katika hali hii kweli watu wa Kanisa au Msikiti wasijali aina ya uongozi tunaokuwa nao kwa manufaa yao na wananchi wao.
Bila shaka kauli za Katibu wa CCM Mkoa Arusha zimejikita zaidi kwenye ubinafsi kwani yeye ndiye kitovu cha vurugu zote za Arusha.