Elections 2010 Wengi hawajui Nguvu ya Maaskofu

Status
Not open for further replies.
Wana haki ya kutoa mawazo yao kama ambavyo nao waislamu wametoa tamko lao. .


Na mimi na wewe tunahaki ya kutoa maoni yetu, tofauti yake mimi na wewe tukisema hata kama tumechemsha impact yake ni ndogo. Don't forget that freedom of speech can also be abused...remember, freedom of speech is your right but responsible speech is your duty
 
Askofu wa Arusha ni mwana Arusha. Kiongozi wa Kiroho, ni kiongozi mwa mwili unautunza roho pia. Huwezi ukaona mwizi akitokea ofisi ya Chama fulani ukakaa kimya eti kwa sababu wewe Askofu au Shekhe utaonekana mwanasiasa. Maskheh na maaskofu wanapaswaa kukemea maovu yote bila kujali nani anayatenda.

HONGERENI MAASKOFU, NAWAPO MOYO SANA....
 
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Yule Askofu Lebulu mpaka ameamua kusema hivyo kuna tatizo kubwa. Na kwa kuwa maaskofu wengi hawana nia ya kushindana na awaye yoyote kwenye kusimamia ukweli, wanaoendelea kuwabeza waendelee tu. Kuna siku kutakuwa hakuna mlango wowote wa kugonga zaidi ya milango ya maaskofu hawa wanaodharaulika endapo amani hii iliyopo itatoweka.
Watawala tusijidanganye kama amani ni kitu ambacho ati serikali iliyopo ama chama tawala ndio vinaitengeneza. Amani iliyopo inatengenezwa na watanzania wote kwa kufuata sheria na taratibu kadri inavyotakiwa. Cama tawala na serikali yake walianza kuzichezea sheria na taratibu za kiutendaji za kuongoza nchi, iposiku madaraka waliyonayo watanyang'anywa na kupewa watu wengine. Wasiwasi wangu ni kuwa siku hiyo inawezekana kabisa ikatokea bila kuwepo amani kama uropokaji, kukosa heshima na maadili ya hovyo ya viongozi yataendelea hivi yalivyo.
 
Hivi Chatanda hakumsikia yule mzee Wasira alivyo sema kule Mwanza kwenye sherehe ya kumsimika askofu mkuu? Aliwaambia maaskofu wasisite kuikemea serikali kama matendo yake yanataka kuvuruga amani. Wazee wenye busara kama Wasira na Malecela wameanza kuliona hilo, lakini wale bongo lala kama Makamba na nduguye Tambwe na kundi lingine kama wakina Chatanda bado wako gizani,hawalioni hilo.
 
Umesema vizuri sana. Kwani huyo Chitanda ni dhehebu gani? Na kwanini yeye na familia yake wasitengwe na kanisa kwa kukosa adabu hadi hapo atakapo tubu dhambi zake?

hapo umenena! Atengwe kabisa huyu FISADi kwani hadi sasa inaonesha yeye ni chakula cha wakubwa!
 
Wewe una akili sana. You are very INTELLIGENT! (siyo intelijensia ya Side Good). Uko sahihi kabisaaaa!
 
Umesema jambo la maana sana,Viongozi wengi wa CCM hawajui mambo muhimu ambayo taasisi za dini zinafanya kwa maendeleo ya jamii.
 
AFRICAN MOVEMENT FOR THE RESTORATION OF THE TEN COMMANDMENDS CHURCH..BABA ASKOFU JOSEPH KIBWETERE, kwa imani bwana yesu amefanya mauaji ya kinyama sana zaidi ya watu 1000 walikufa ikiwamo miili ya watoto 11 iliyoungua na moto kutokana na tukio hilo, uchunguzì wa polisi wa uganda wamegundua baadhi wamepewa sumu wengine walikuwa wemenyongwa na wengi walikuwa na alama za kuchomwa na vitu vya ncha kali, mafuvu yalikuwa yamepasuka na na kutupwa kwenye visima na vyoo vya mashimo.NGUVU ZA MASKOFU
 
AFRICAN MOVEMENT FOR THE RESTORATION OF THE TEN COMMANDMENDS CHURCH..BABA ASKOFU JOSEPH KIBWETERE, kwa imani bwana yesu amefanya mauaji ya kinyama sana zaidi ya watu 1000 walikufa ikiwamo miili ya watoto 11 iliyoungua na moto kutokana na tukio hilo, uchunguzì wa polisi wa uganda wamegundua baadhi wamepewa sumu wengine walikuwa wemenyongwa na wengi walikuwa na alama za kuchomwa na vitu vya ncha kali, mafuvu yalikuwa yamepasuka na na kutupwa kwenye visima na vyoo vya mashimo.NGUVU ZA MASKOFU
Majani!!
 
well Chitanda alisema wajihusishe na kukemea maovu TUUUUUUUUUUU! Hivi unajiuliza, uuaji wa raia namna ya Arusha si uovu huo? Na viongozi wasikemee hilo pia?

tatizo hivi vyeo vya kupeana mahotelini bila kujua upeo wa mhusika unayempa hicho cheo..ndiyo haya ya kina Kitanda..hauhitaji elimu ya chuo kikuu kujua umuhimu wa viongozi wa dini ktk maendeleo ya sehemu husika:love::love:
 

Nimeshangazwa na kauli za baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Dini fulani mkoani Arusha kupinga tamko la Maaskofu walilolitoa baada ya kotokea vurugu mkoani Arusha. Pamoja na shutuma nyingi, maaskofu hao wametakiwa kujitenga na mambo ya kisiasa badala yake wajihusishe tu na Mambo ya kiroho na si vinginevyo!

Ni rahisi sana kutoa tamko la namna hiyo kama huna muda wa kutafakari na kujihoji wewe mwenyewe kujua sababu za maana zilizosababisha Maaskofu kutoka kwenye makanisa yao na kuingilia moja kwa moja mambo ya kisiasa hususan sakata la Meya wa Arusha.

Maaskofu hawa walikuwa na sababu za msingi kabisa kumpinga Meya wa mji wa Arusha kutokana na sababu kadha wa kadha. Zaidi ya Asilimila 70 za huduma za kijamii kama Hospitali, shule achilia mbali miradi ya maji n.k Mkoani Arusha tu zinamilikiwa na kanisa. Kanisa limekuwa halina ubaguzi wa Kidini katika utoaji wa huduma zake hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi na serikali. Kwa miaka mingi tumeshuhudia kanisa likifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na tabu zisizo za lazima kwa kujihusisha moja kwa moja na shida za jamii. Kanisa la Tanzania limekuwa likithubutu hata kushawishi nchi mbalimbali kama Ujerumani, Uingereza n.k kuziomba zitusamehe madeni, yote hayo ni katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Tanzania anapata nafuu bila kujali chama, dini au rangi. Hivi harakati zote hizi nilizotaja sio siasa hizi? Iweje suala dogo la kumpinga meya liwaondoe wanaharakati hawa katika siasa?

Nimeamua kuyaweka maelezo hayo machache ili nikufikirishe utambue umuhimu wa kanisa katika Nchi hii. Kimsingi MEYA wa jiji la Arusha hawezi kujitenga na kanisa kwa namna yote ile kwani kwa kiasi kikubwa kanisa linategemea kiongozi wa kisiasa ambaye kwa pamoja watashirikiana bega kwa bega ili kuendeleza zile juhudi kubwa zilizofikiwa na ambazo ni changamoto kwa maendeleo ya wanachi wa Mkoani humo. Huwezi kumtoa Askofu katika siasa, maana kwa upana wake siasa inagusa maisha ya kila siku kwa kila mtu, Askofu anahitaji Amani, maendeleo pamoja na huduma muhimu.aidha ieleweke wazi kuwa kazi ya kanisa si kutoa mapepo na kuombea wagonjwa tu, bali pamoja na hayo ni kuhakikisha kuwa maisha ya kawaida kwa maana ya mahitaji ya kimwili yanaguswa kwa namna mbalimbali.

Unapomwambia Askofu ajitenge na na siasa ni kwamba Wavunje Hospitali zao za Rufaa? Shule zao zinazofanya vizuri na kuzalisha watu wenye akili? Wavunje vyuo vyao ambavyo ni vingi kushinda vya serikali? Wasihoji vile visima vyao vya maji na miradi ya umwagiliaji? Hapana!!!. Nafikiri kuna maeneo ambayo Viongozi hawa inabidi wahoji na kukosoa wanasiasa ili vile ambavyo walibuni na kuhakikisha kuwa vinawasaidia wananchi wakiwamo waumini wao havisimamiwi na viongozi wabovu au viongozi ambao kwa nia moja au nyingine wanania mbadala na isiokubalika kwa wananchi wa Tanzania. Viongozi wa Kanisa kamwe hawatakuwa mishumaa ya kuwamulikia watu waovu wakati wao wanateketea. Linapokuja swala la Maaskofu kujiingiza katika siasa Nguvu yao ipo katika Huduma na mambo ya msingi ambayo kama wataamua kumwachia Mungu watu waovu wanaweza kuifikisha Tanzania yetu mahali ambako sio salama. Kiongozi wa kidini ambaye haoni sababu za kujiingiza na kuhoji mambo ya siasa ujue hana cha kupoteza!!!!!!!!!

The Following 26 Users Say Thank You to Anold For This Useful Post:
3D. (10th January 2011), Babasean (Yesterday), Candid Scope (Today), Eeka Mangi (10th January 2011), hilbajojo2009 (10th January 2011), Jile79 (10th January 2011), Konakali (Yesterday), mageuzi1992 (10th January 2011), malipula (10th January 2011), mamakunda (10th January 2011), Mchwechwele (10th January 2011), Mfwatiliaji (10th January 2011), Mgalanjuka (10th January 2011), Mindi (10th January 2011), Mkeshahoi (10th January 2011), MVUMBUZI (10th January 2011), Mwikimbi (Yesterday), Mzee Mwanakijiji (Yesterday), Neema J Makene (10th January 2011), Ngalikihinja (10th January 2011), nzehe (10th January 2011), Shakazulu (10th January 2011), STEIN (10th January 2011), tarita (10th January 2011), tru rasta (10th January 2011), VSM (Yesterday)
 
mkuu anold haihitaji kuwa std 7 kujua akili ya huyo mama hajui power ya church ktk serikali aulize ROMAN EMPIRE!!!
 
Kwakweli CCM imelichoka kanisa matusi yao yalianzia Sumbawanga na sasa wamehamia Arusha, mi nahisi wakiendelea hivi wataifikisha hii nchi mahala pagumu sana...

Kwa kauli hizi mgawanyiko wa kidini utaanzia huku huko ndani ya CCM na mwishowe kuivunja vipande vipande, maana kuna viongozi na wanachama ambao ni waumini wazuri wasiopenda kuona viongozi wao wa kidini wakidharauliwa kiasi hiki...

Kadiri siku zinavyokwenda ule mstari wa kutofautisha dini na siasa unazidi kufutika ndani ya Tanganyika :pout:

Inasikitisha..
 
Ukiona chama kimeanza kuwa na watu kama Mkwere, Makamba, Chitanda, n.k. basi ujue kuwa huo ndo mwanzo wa kuwa mwisho wa kuwa chama tawala kwenye Taifa lenye watu wenye upeo kama Tanzania! Namshauri kikwete na hili kundi lake la wahuni wajiulize KANU na vyama vingine vilivyopoteza madaraka Afrika walikosea nini.

Nchi inabadilika, watanzania sasa wanaanza kuchambua pumba na mchele. Mara nyingi watu wastaarabu huwa inawachukua muda mrefu kujipatia uhakika wa lile linalofanyika au kutokea na kuchukua hatua baada ya kufanya maamuzi sahihi.

Busara na upeo wa viongozi wa CHADEMA sasa unaanza kueleweka vema kwa watanzania wapenda nchi yao. Sidhani kama mkwere na kundi lake la kinyang'anyi litapata tena fursa ya kuongoza taifa hili. Huu ndio mwisho wao, tunataka kurudisha nchi yetu iliyoanza kupoteza mwelekeo kutokana na viongozi wasio na uwezo, busara wala uchungu na nchi, bali wizi tamaa na ubinafsi mpaka hata kuua ili kulinda maslahi yao na familia zao.
 
Wapi iliandikwa kwamba maaskofu au wakuu wa dini wasijihusishe na siasa? Je, is religion operative outside this world? Je, hao wanaohudumiwa na maaskofu sio wanaoku-affected ya mambo ya kisiasa? Sasa wawaache tu waumie? Kazi ya kiongozi wa dini ni kuangalia maslahi yote ya mwanadamu ya kimwili, kiroho na kisaikologia; this includes pastoral care, counseling, nurturing people spiritually, advocacy in issues of justice....and speaking against all forms of evil...they are the prophets of today....and they have their civil rights ambayo haiondolewi na uaskofu wao...so hizo nonsense must stop
 
Mkuu Anold bahati nzuri sana watz ni wepesi sana kusahau askofu fulani alipata kusema as individual jk ni chaguo la Mungu, matusi na kejeli alizopata kutoka kwa wana jf ni tofauti kabisa na hao hao wanaounga mkono kauli ya maaskofu kutomtambua meya na kutompa ushirikiano ndio waliomtaka askofu huyo avue joho ajiunge ccm

Nirejee ktk mada yako, kwanza nikupe pongezi kwajinsi ulivyojitahidi kuiwasilisha hoja yako kwa umahiri mkubwa wenye kushawishi tuamini ulichoandika ni sahihi.
Ulichojaribu kukieleza hapo ni jinsi gani kanisa lilivyo wekeza ktk huduma mbali mbali za kijamii, na ukaenda mbali zaidi na kuita hii ni "siasa" na ukaona kuwa hii ndio "nguvu" ambayo watu hawaitambui nguvu hii ya maaskofu kama ulivyoainisha ktk heading ya topic yako.

Umeniacha hoi kabisa uliposema kama wanataka maaskofu wasiingilie siasa basi wavunje huduma zao zote maana kwako wewe hii ndio siasa na unashangaa kwanini iwe ajabu wao kuingilia jambo "dogo" kama la meya wa arusha.

In short hiyo uliyoita "nguvu ya maaskofu" kwa mujibu wako ndio inayowapa uhalali wa kuingilia maswala ya kisiasa tena kwa kutoa matamko mazito ya maamuzi ya mamlaka nyingine ya kisheria.
Ni matamko kama kukemea ufisadi na kutaka maadili yazingatiwe ndio matamko yanayotarajiwa toka kwa viongozi wa dini.
Kwa hili la kupingana na maamuzi ambayo vyombo husika vimelipitisha kwa taratibu husika na kisha chama fulani kikagoma kwa hisia zao za kuonewa au iwe wameonewa kweli kisha maaskofu wanakurupuka na kusema hatumtambui hii si sahihi kabisa, ya kaisari aachiwe kaisari.
Je ikithibitika kisheria ilikuwa ni halali nini itakuwa credibility ya maaskofu?
Kanisa kuwa na vyuo au hosipitali(ikumbukwe ni misamaha ya kodi) sio kibali cha kuingilia maswala ya siasa.
Ninacho kuhakikishia hapa ni kuwa siasa zitaanza kuhubiriwa madhabahuni na misikitini kwa msingi huo wa kipuuzi unaotushawishi tuamini kuwa huwezi kuwaepusha maaskofu na siasa.
Ni mpumbavu pekee asiyeweza kuona hatari inayotunyemelea kwa kuacha viongozi wa dini wawe wanatoa matamko hovyo tu, hawa ni binadamu na wanautashi wao binafsi kama binadamu yeyote.

Pia ujue dini ni imani kali yenye kugusa hisia anachotamka askofu sikuzote ni sahihi mbele ya muumini no matter kiweje, mimi ni mkristo safi lakini kwahili ntasimamia hapana

Watu wengi wamekupa thanx na kuunga mkono hoja yako sababu tu wamesikia kile wanapenda kusikia bila kujali kina mantiki gani. watu wanashindwa kuona mbali sababu tu for this time wao ndio wanabenefit na tamko hilo la maaskofu

Mwisho nawaheshimu sana maaskofu lakini kwa hili wanakwenda mbali sana maana kwa mwendo huu watakuja kutoa tamko tubaki midomo wazi tusiamini masikio yetu.
 
Anold, umenikumbusha kitu muhimu sana kuhusu kazi za Kanisa na uhusiano na uchumi wa eneo. Miaka ya 1970 na 1980, Padri mmoja mzee kule Maua Moshi alianza kuona chemichemi alimokuwa ametegeshia pump za maji kwa ajili ya shule ya seminari na majirani zilikuwa zinaanza kukaukia. Akagundua tatizo ni ukataji wa misitu millimani ambako ndiyo chanzo cha maji. Basi akaamua kuanza kuotesha msitu na amini usiamini kwa kushirikiana na wanafunzi na watu wachache walioajiriwa na kanisa aliotesha msitu wa zaidi ya kilomita mraba 6. Msitu ukakua na vyanzo vya maji vikawa vimeanza kushiba maji.

Mwaka 2004, akiwa anatembea kwenye tafakari maeneo ya seminari yake, aliona malori makubwa makubwa yamebeba miti. Kumbe Afisa Msitu alitoa kibali cha kuvunwa ule msitu aliootesha yule Mzee. Alikimbiza magari yale kwa miguu na kupayuka, akitaka kujua imekuwaje wanavuna msitu! Alikwenda Idara ya Msitu, na wale watendaji wakamshangaa, kwanza yeye ni mzungu halafu anazungumzia uvunaji wa raslimali za kikwetu. Baadaye ilijulikana kuwa ni viongozi wa serikali za mtaa kwa kushirikiana na watendaji waliridhiana kuvuna ule msitu. Katika hali hii kweli watu wa Kanisa au Msikiti wasijali aina ya uongozi tunaokuwa nao kwa manufaa yao na wananchi wao.

Bila shaka kauli za Katibu wa CCM Mkoa Arusha zimejikita zaidi kwenye ubinafsi kwani yeye ndiye kitovu cha vurugu zote za Arusha.

Hata mimi ni mdau wa msitu huo kule Maua kijiji cha Rua. Tulikuwa na mpango wa kufanya documentary kuhusu uvunaji wa huo msitu maana hata mimi nilishiriki nilipokuwa hapo Maua 1982-1988. Sasa hivi huyo Fr Ladislaus ni mzee na anajisikia vibaya kuona viongozi wenye njaa wanavuna msitu ambao ni chanzo cha maji na huku serikali ikipigia debe utunzaji wa vyanzo vya maji. Tutajitahidi kuweka wazi kwenye hiyo documentary majina ya viongozi wote walioshiriki kuuvuna huo msitu - ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom