SoC03 Wema wako ulibadili maisha yangu

Stories of Change - 2023 Competition

LEZIMA

New Member
Jun 1, 2023
3
4
Siku moja Heri akiwa katika kutembea alimkuta mwanaume wa makamo akiwa ameketi Kando ya barabara. Mwanaume yule kwa muonekano tu na vile alivyokuwa amekaa pale chini hata wewe ungejua kabisa kuwa mwanaume yule alikuwa ni ombaomba.

Alikuwa amechafuka sana, nywele zake na ndevu zake zilikuwa ni ndefu sana, pia zilikaa ovyo. Kiufupi ni kwamba hakuwa katika muonekano mzuri hata kidogo. Hali ya hewa ilikuwa ni baridi kali sana, yeye alikuwa amevaa shati jepesi tu tena lililochanikachanika.

Heri alimwangalia kwa makini mwanaume yule, kisha baada ya kumwangalia kwa muda mrefu alimuonea huruma. Aliamua kusogea karibu yake na kumsalimia. Lakini, mwanaume yule hakujari Ile salamu Bali akazidi kutazama mbele yake Kama ambaye hajaongeleshwa wala kusemeshwa chochote.

Heri alifungua begi lake alipokuwa amelibeba, akatoa koti na kumkabidhi mwanaume yule. Alimsihi alivae like koti ili ajikinge na baridi lakini mwanaume yule hakukubali. Alimuuliza Kama alikuwa amekula lakini Bwana yule hakutaka Heri aendelee kumuumiza maswali yake. Hii ni kwasababu alikuwa amechoshwa na maneno ya kejeli ambayo wapita njia wengi walikuwa wakimwambia pindi wamuonapo pale njiani.

Kwa hasira alimwambia Heri "tafadhari binti nakuomba uondoke hapa kwangu Kama umekuja kunidhihaki". Pamoja na kuwa mzee yule aliongea akiwa amekasirika, Heri hakuondoka bali alipiga magoti na kumsihi bwana yule akisema "najua una njaa, tena unapigwa na baridi, siwezi kuiacha hapa wakati ninajua kuwa una shida na mimi uwezo wa kukisaidia ninao". Bwana yule alikuwa no mkali sana lakini alipoona Heri hataki kuondoka aliamua likubali. Alivaa koti lile na kumwambia Heri kuwa ni kweli ana njaa.

Heri alimsihi Bwana yule aongozane naye mpaka kwenye mgahawa mkubwa kidogo uliokuwepo mtaani pale. Walipofika pale Heri alimweleza yule Bwana akae kwenye huduma, kiti hicho walikuwa wanakalia watu maalumu au wale wageni wakubwa waliokuwa wamealikwa na bosi.

Mhudumu mmoja aliyekuwa akiwatazama alipiga kelele akisema "wewewe!!! Unawezaje kumruhusu kichaa kuingia hapa ndani tena ukamwambia akae kwenye kiti cha watu wazito? Kwamba wewe no nani, maana huenda hata wewe ukawa una matatizo!"

Heri aliuachia tabasamu hafifu usoni lake ambalo kama mtu angekuwa makini katika kumtazama, angegundua kuwa lilikuwa mi tabasamu lililoashiria dharau kubwa. Aliketi kimya akamuuliza "unamfahamu au uliwahi kumsikia Heri Gonzale?" Mhudumu yule akajibu bila kupoteza muda "ndio". Baadaye ya hapo Heri alitulia kudogo na kuuliza "unamfahamu vipi?" Mhudumu yule akasema "mtu huyo ndiye mmiliki wa huu mgahawa. Na leo atafika hapa ili kufanya kikao na sisi, nafikir Kama utaendelea kuwepo unaweza ukapata bahati ya kumuona.

Heri akamwambia "ooh! Sawa nimekwishafika, naomba ukampe taarifa meneja umwambie nimeshafika". Yule mhudumu alimwangalia kwa umakini kama ambaye hakuelewa alichokisema, akayakumbuka yale maneno aliyomtamkia anapofika mahali pale akifikiri labda no mmoja kati ya wateja wao. Alihisi aibu sana kisha akaondoka kwenda kumpa taarifa Meneja.

Wakubwa wamebaki wawili, Heri alimuuliza yule mzee "je, unanikumbuka Mimi?" Yule mzee alimtazama Heri na kumjibu "nahisi kama niliwahi kukuona Ila shida ni kwamba sikumbuki nilikuona wapi". Heri akamwambia "Mimi ni yule binti niliyekuja nyumbani kwako miaka sita kumi iliyopita nikiwa nimenyeshewa na mvua na baridi ikiwa imenipiga. Nilikuwa sina sweta pia nilikuwa na njaa sana. Nakumbuka ulinikaribisha jikoni niote moto, ulinipa sweta, na ukanipa chakula nika.. kabla hajamaliza Mzee yule aliuliza "vipi ulifanikiwa kufanya usaili siku ile?" Heri alijibu kwa furaha "ndio nilifanya na nikawa miongoni mwa waliochaguliwa".

Heri aliendelea kumweleza mzee yule "sasaivi namiliki mgahawa wangu mwenyewe na nimeajiri wafanyakazi. Nakushukuru sana bwana Henry kwa msaada wako, ijapokuwa ulikuwa hunifahamu lakini ulinisaidia. Na huu ni wakati wangu wa kumlipa fadhira, nitakujengea nyumba na kukuhudumia kama mzazi wangu.

Bwana Henry alifurahi sana, hakuwahi kukutana na mwanamke mwenye roho nzuri kama yule. Alitegemea kuwa mwanamke kama yule tena anayemiliki kampuni angeweza kuwa na roho mbaya kama wanawake walio wengi walivyo. Hiyo ni kwa sababu alizoea kuwaona watu wengi wenye pesa wakiwa wamejawa dharau na viburi. Tena isingewezekana kabisa kwa mtu Kama Heri kumsaidia mtu Kama Bwana Henry, lakini Heri alikuwa na moyo wa tofauti sana.

Siku zilisonga na miezi ikayoyoma huku Heri aliendelea kufanya kazi kwa bidii na kumhudumia Bwana Heri Kama mzazi wake. Bwana Heri alifurahi sana huku akizidi kusambaza habari kwa watu kuwa, "wapo matajiri wengi wenye pesa, lakini Heri amebarikiwa halafu ni mtu wa watu".

Bwana Henry hakuacha kumuombea Heri hata siku moja. Kila siku alikiwa alimuomba Mungu azidi kumlinda na kumtetea katika maisha yake.

Sio Bwana Henry tu aliyemuona Heri kuwa ni mtu mwema, bali hata wafanyakazi wake walimpenda Heri kutokana na uongozi wake nzuri. Hii ni kwa sababu Heri hakuwahi kumuonea mfanyakazi awaye yeyote yule. Alitenga haki katika kila kipengele huku akiwasisitiza watu wake wafanye kazi kwa bidii wakiiga mfano kwake.

Hata hivyo, hakuna binadamu anayependwa na watu wote. Hata Kama una mema mengi, ni lazima kuna watu watakuchukia. Hata Heri alichukiwa na wafanyakazi ambao wao walimpenda kuwa wavivu na kuwa kiherehere katika kudai mshahara. Lakini hayo hayakumfanya Heri ateteleke au arudi nyuma, aliyapuuza akazidi kufanya kazi na kuwaongoza watu wake.

Funzo
Kila Jambo unalolitenda kwenye hii dunia ni kama akiba, usishangae likaja kukurudia miaka kadhaa ijayo. Hii ni kwa sababu kila kazi ina malipo yake, tenda wema sasa ili ulipwe wema baadae. Lakin pia kumbuka kuwa juhudi haijawahi kumtupa mtu mkono, Kama ukifanya kazi kwa bidii ni lazima utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom