Wema Sepetu na Ommy Dimpoz katika mahaba, kimya kimya

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,417
upload_2016-5-14_15-8-43.png


LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa Wema amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika mapozi ya kimahaba huku wamevaa mavazi ya kulalia.

Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake.

Chanzo cha habari hii kinaeleza kuwa, picha hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani kwa Dimpoz, Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho kilipozikwapua na kuzituma kwa piblic.

“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya maana wenyewe hawataki kuanika mambo yao,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kuwa, kutokana na Diamond kufahamu kuwa, wawili hao wanaendeleza uhusiano, ndiyo maana tangu picha zao za awali zilipovuja mwaka jana wakiwa nchini Afrika Kusini, Diamond na Dimpoz haziivi na hata uswahiba haupo tena kama zamani zile.

“Diamond hataki hata kumsikia Dimpoz katika maisha yake, anamuona ni mtu ambaye hakufanya uungwana kuwa na mtu ambaye yeye tayari ameshatembea naye,” kilisema chanzo hicho.

Ommy Dimpoz alikiri kuwa picha hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.

“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua, Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna kitu kingine zaidi ya ushikaji.

Kuna mtu itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema Dimpoz.

upload_2016-5-14_15-9-16.png


Source: Tanzania Today
 
Mond mwenyewe ana mke wa mtu(Zari). Sioni tatizo Wema akitoka na Dimpoz kwani hata hawakuwa wameoana. Na nina uhakika Mond hakuwa wa kwanza wa Wema. Hata baada ya talaka watu uoa na kuolewa.
Let Wema and Dimpoz choose whoever they love not who people want them to love.
 
Aah hizo picha zinaonekana za muda wema alikuwa hajawa na tako kubwa ile mitako ingeonekana tu kwenye picha
 
Back
Top Bottom