Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
hau machi ini madafu pa naiti?......givu mi ze toto pakeji inklusivu transipoti
Check the ROOM RATES!
Hizi Kwa Tanzania ziko Tatu yaani :
Grumeti Reserves: Sasakwa Lodge, Sabora Tended Camp na Faru Faru Lodge.
Hizo RATE ulizopewa hapo mbona ni ndogo sana? Angalia hizi ambazo ni za juu kabisa. Kumbuka kuwa hii ni Hotel ya Mtoto wa Mzee wa NASDAQ Stock Market, lile moja ya masoko makubwa duniani kama la Wallstreet ndani ya New York.
Sasakwa Lodge: ndiyo aghali sana: Bei inaanzia $1,600/- hadi $16,500 ukichukua Luxury Villa per night (4 bed room)
Singita Game Reserves > Rates for Singita Sasakwa Lodge
Sabora Tended Camp: ina nafuu kwa walala hoi wenye hela zao na wameamua kuwashau ndugu na jamaa zao:
Luxury Tents double: $1 045.00 per person per night sharing
Singita Game Reserves > Rates for Singita Sabora Tented Camp
Faru Faru Lodge: Rate zake ndiyo hizo juu uliwekewa.........
Singita Game Reserves > Rates for Singita Faru Faru Lodge
Hivyo basi Sasakwa Lodge ni kwa Watanzania kama Hashimu Thabeet na wengine wachache sana. Vinginevyo wanabaki Wahindi, Waarabu na wazungu wanaoishi Tanzania. Wengine wote watumiaji wanabaki kama alivyosema Mkuu Jasusi, watu wa Hollywood maana yule badala ya kulipa, yeye analipwa ili atangaze soko....... Hapo ndiyo wanaingia watoto wa Mamilionea na Bilionea wa dunia hii kuja kula goodtime mbaali kabisa na PAPARAZI.
Unayeuliza Price OFF (Gaijin):
Hizi ni zile Hotel ambazo mtu haulizi bei. Nashangaa hata wameweka bei. Ni za watu ambao akitaka kununua gari, haulizi Bei wala linakula mafuta kiasi gani, yeye anataka tu kujua atapata nini ndani ya lile gari na wangapi wanalo. Ukianza kuuliza bei, basi ile si hotel yako.