Welcome to the Grumeti Reserves...!

hau machi ini madafu pa naiti?......givu mi ze toto pakeji inklusivu transipoti

Check the ROOM RATES!

Hizi Kwa Tanzania ziko Tatu yaani :
Grumeti Reserves: Sasakwa Lodge, Sabora Tended Camp na Faru Faru Lodge.

Hizo RATE ulizopewa hapo mbona ni ndogo sana? Angalia hizi ambazo ni za juu kabisa. Kumbuka kuwa hii ni Hotel ya Mtoto wa Mzee wa NASDAQ Stock Market, lile moja ya masoko makubwa duniani kama la Wallstreet ndani ya New York.

Sasakwa Lodge: ndiyo aghali sana: Bei inaanzia $1,600/- hadi $16,500 ukichukua Luxury Villa per night (4 bed room)
Singita Game Reserves > Rates for Singita Sasakwa Lodge

Sabora Tended Camp: ina nafuu kwa walala hoi wenye hela zao na wameamua kuwashau ndugu na jamaa zao:
Luxury Tents double: $1 045.00 per person per night sharing
Singita Game Reserves > Rates for Singita Sabora Tented Camp

Faru Faru Lodge: Rate zake ndiyo hizo juu uliwekewa.........
Singita Game Reserves > Rates for Singita Faru Faru Lodge

Hivyo basi Sasakwa Lodge ni kwa Watanzania kama Hashimu Thabeet na wengine wachache sana. Vinginevyo wanabaki Wahindi, Waarabu na wazungu wanaoishi Tanzania. Wengine wote watumiaji wanabaki kama alivyosema Mkuu Jasusi, watu wa Hollywood maana yule badala ya kulipa, yeye analipwa ili atangaze soko....... Hapo ndiyo wanaingia watoto wa Mamilionea na Bilionea wa dunia hii kuja kula goodtime mbaali kabisa na PAPARAZI.

Unayeuliza Price OFF (Gaijin):
Hizi ni zile Hotel ambazo mtu haulizi bei. Nashangaa hata wameweka bei. Ni za watu ambao akitaka kununua gari, haulizi Bei wala linakula mafuta kiasi gani, yeye anataka tu kujua atapata nini ndani ya lile gari na wangapi wanalo. Ukianza kuuliza bei, basi ile si hotel yako.
 
ngoja nikwambie.....kwa nini mimi mtanzania nilipe sawa na mzungu wakati hii kitu ipo nchini kwangu.....ni tabia mbaya kwa serikali kuwaachia hawa wawekezaji kutunyanyasa ndani ya nchi yetu...ingetakiwa moja ya sharti la uwekezaji liwe kuwa na bei ya mzalendo ( naruhusu kusahihishwa)..nimewahi kufika hapo but hata huduma ya mswahili na mzungu ni tofauti kabisa pamoja na yule shoga yake Bilila...huyu yeye rate zake ni kwa euros....ni aibu sana kwa taifa lenye vivutio kama hivi lakini wananchi wake hatuvifaidi

Umesikika bibie. I strongly support you.
 
ni kweli kabisa unachoongea na ndio maana huwa wanalalamika utalii wa ndani haukui na kila siku tunasikia wanapanga mikakati ya kukuza utalii wa ndani, mikakati yenyewe inabaki kwenye makabati tu utekelezaji 0
 
Naruhusiwa kwenda na Eliza hapo? Hawakawii kusema mbona ana rangi mbili!
 
hakuna prices za off peak huko?

utalii wa ndani utashamiri ikiwa kutakuwa na bei maalum kwa ajili ya wakati wa off peak manake competition na mzungu hatujaiweza bado.

hiyo bei iliyowekwa hapo ni rack rate ambayo travel agent hawezi pewa hiyo na sisi watanzania kutumia agent bado kidogo...bei za off peak zitakuwepo lazima but sio nafuu kivile bado ni ghali na utatakiwa ulipe kwa dola, na isitoshe kwa upande ilipo hiyo lodge, off peak ni april,may and mid june, kunakuwa na mvua, nyasi ni ndefu huwezi kwenda off road utakwama, na burudani ya huko ni uone wanyama sana sana utaenjoy migration ya nyumbu....but its good to experience
 
Naruhusiwa kwenda na Eliza hapo? Hawakawii kusema mbona ana rangi mbili!

unaruhusiwa kwenda nae mradi ajue kuswitch on/off jacuzzi........halafu wewe.....hiyo avatar yako hiyo....embu njoo kwanza hapa calabash tuijadili
 
ngoja nikwambie.....kwa nini mimi mtanzania nilipe sawa na mzungu wakati hii kitu ipo nchini kwangu.....ni tabia mbaya kwa serikali kuwaachia hawa wawekezaji kutunyanyasa ndani ya nchi yetu...ingetakiwa moja ya sharti la uwekezaji liwe kuwa na bei ya mzalendo ( naruhusu kusahihishwa)..nimewahi kufika hapo but hata huduma ya mswahili na mzungu ni tofauti kabisa pamoja na yule shoga yake Bilila...huyu yeye rate zake ni kwa euros....ni aibu sana kwa taifa lenye vivutio kama hivi lakini wananchi wake hatuvifaidi

Duniani kote serikali makini huwashurutisha watoa huduma wa kila aina sio hoteli tu kuwa na viwango nafuu kwa ajili ya wakazi wa nchi husika na hii sio raia tu bali hata wakazi wakudumu.
 
JEMBE ni kwa WAKULIMAAAAAA!... na NYUNDO ni kwa WAFANYAKAZIIIII! KIDUUUUUMU CHAMA TAWALA! ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI!!! "Sasa tunapenda kuchukua fursa hii kumkaribisha msanii Maloooooo!!! Pamoja na VUVUZELA zake aje kutupa Shooo!!! By Captein Chiligati aka CHILL-SAUCE!!! ... IT SUCK...
 
Hivi vitu vingine tutabakia kutolea macho tu!!!!, $ 1,045 kuziunguza kwa usiku mmoja wakati mdogo wangu aliyepata nafasi ya chuo kikuu anasubiri kudeposit ada apate registration, wapi na wapi!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom