Weka aya/ mstari kutoka kitabu cha dini yako unaoona umeandikwa kwa ustadi, weledi na hekima ya hali ya juu

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,820
11,553
Ukisoma vitabu vya watu mashuhuri kama shakespeare, kuna ile unakuta mwandishi ameandika kwa ustadi wa hali ya juu...yani ametumia maneno vizuri, yani maneno ameyatumia kama rangi vile kuchora picha nzuri sana inayovutia kutazama machoni.

Bila stori nyingi au maelezo mengi, weka fungu la kitabu chako cha dini ambalo unaona limeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Naanza mimi:

Warumi 8:31

Tuseme nini basi kuhusu haya yote? Ikiwa Mungu yuko upande wetu ni nani atakayetupinga?....Ni nani atawashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo? Ni shida? Au taabu? Au mateso? Au njaa? Au umaskini? Au hatari? Au Kifo?

Hapana. Lakini katika mambo yote haya sisi ni washindi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda. Kwa maana nina hakika kuwa, si kifo wala uzima; si malaika wala mashetani; si mambo ya sasa wala mambo yajayo au mamlaka nyingineyo yote; si mambo yaliyo juu wala yaliyo chini sana; wala hakuna kitu kingine cho chote kati ya vitu vyote alivyoumba Mungu kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.
 
2Thimotheo 3:16-17

16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
 
1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Likewise, ye husbands, dwell with them according to knowledge, giving honour unto the wife, as unto the weaker vessel, and as being heirs together of the grace of life; that your prayers be not hindered.
 
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
2 Timotheo 3:16

17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
2 Timotheo 3:17
Nice
 
Ufunuo wa Yohana14:13
13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Screenshot_2017-08-13-23-50-22.png

Hapa muandishi aliandika kwa busara na utulivu wa hali ya juu sana
 
Isaya 4:1

Isaya 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
 
Isaya 4:1

Isaya 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
Dah.. Naisubiri sana hii
 
1 wakorinto 1: 27

27 Lakini Mungu alichagua vitu ambavyo huhesabiwa kuwa vya kijinga ulimwen guni ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alichagua vitu vidhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wenye nguvu.
 
Mithali 21:9
Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.

Mithali 21:19
Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.

Mithali 27:4
Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom