Binadamu alijipatia hekima ya uovu alipokula tunda

Ghost boss

Member
May 3, 2019
33
56
BINADAMU ALIPOTEZA KILA KITU ALIPO ASI

Binadamu alipoamua kuasi, alipoteza uwezo wote wa asili alio kuwanao, binadamu alikuwa mtawala wa kweli katika USO wa dunia, lakini alipoteza uweza wake kwa kuasi, ule Mti wa ujuzi wa mema na mabaya (kama unavyotajwa ujuzi) haukuwa mti wa kujipatia hekima Bali ni mti wa ujuzi wa uovu, binadamu kiasili alikuwa ni kiumbe chema kabisa kisicho na kasoro kwani Mungu alimuumba kwa wema kabisa, lakini udhaifu wa sasa wa binadamu unatokana na uasi wake mwenyewe, hii nipamoja na mateso na matatizo aliyonayo, matatizo aliyonayo binadamu ni kwasababu ya kuasi, yaani lengo kuu la Nyoka na shetani ilikuwa ni kumwondoa au kumpindua binadamu katika cheo chake na uweza wake.

Kwanza binadamu ndiye mwangalizi wa dunia na kwa upande mwingine ndiye mlinzi wa dunia, kama abinadamu ata pinduliwa basi mamlaka yote yatakuwa kwa yule aliye mpindua, basi nyoka na shetani walifanikiwa kumtoa binadamu katika mamlaka yake, sasa kama ilivyokwa mtawala yoyote huteseka kwa kuwekwa kizuizini na kwenye kifungo (yote umkuta baada ya kupinduliwa) basi binadamu Leo anateseka kwa sababu ya kupoteza uweza wake wakutawala mazingira, tatizo la kushindwa kutawala mazingira ndio msingi wa matatizo yote ya binadamu, hekima ya kutawala mazingira iliondolewa kwa binadamu kwa kuasi kwak.

Mungu alimpa uweza wa hali ya juu sana, lakini alitaka pamoja na binadamu kuwa nauweza huo alitaka utii kutoka kwa binadamu, utii wa binadamu ungemwezesha kukaa katika utawala wa kazi zote za Mungu duniani, lakini binadamu alipokataa kabisa kumtii Mungu alipoteza kabisa uweza wake wote, sasa binadamu anajua kutenda mabaya kama ujuzi alioupata kwa kula tunda la ujuzi wa mabaya, sasa ujuzi wa kutenda au kujua mabaya ndio hekima?, matekeo yake hawezi kutawala mazingira yake na anateseka, hivi kweli tunaweza kuamini binadamu hakuwa na hekima kabla ya kula tunda?

Jibu ni hapana kwasababu hakuna ambaye anaweza kuweka kazi yake yote isimamiwe na MTU asiye na akili kabisa, Mungu aliweka kazi yake yote chini ya binadamu mwenye akili, alitaka kila kitu kiwe salama na kwasababu hiyo alimpa hekima ya juu sana, sasa angalia Leo kuna kuyeyuka kwa barafu mabadiliko yenye athari kwa tabia ya nchi, angalia kuna mioto ya misituni, kuyeyuka kwa barafu na ongezeko la hewa ya carbon, uharibifu wa kila aina ya shughuli za kuihalibu dunia, je! uyu mwanadamu ndiye Mungu alitaka awe juu ya Mali yake?

Hapana uyu binadamu wa leo mwaribifu asiye na akili siyo Mungu alitaka aitawale dunia, tujiulize je hii ndio tunayoita hekima baada ya binadamu kula tunda la mti waujuzi wa mema na mabaya? matokeo yake binadamu hana uwezo wake waasili wa kuongea bila shida na Muumba wake, kumbuka Mungu alikuwa akimtembelea na kuongea na Adamu kila jioni, muda wa kupunga upepo, je! Mungu anaweza kuongea na kiumbe kisicho jielewa?!

Hapana ila sasa Mungu hawezi kuongea nasi hivyo maana hatuna akili mwishowe atatuangamiza kwa maneno yetu yasiyo na maana tu, kwani hatuna hekima ya kujua jinsi gani ya kuongea na muumba wetu, kinachotufanya ni kuomba na kusubili ila sio kuongea na Mungu, basi kwa Leo binadamu hawezi kuwa na hekima bila usaidizi wa Roho mtakatifu, ukweli ni kuwa katika historia ya binadamu, Yesu Kristo alipokuja duniani alikuja kumrudishia mwanadamu alichopoteza, kwa Ku mwamini yeye ndio mwanadamu anapata uweza alio poteza, utajiuliza kivipi?

Au unasema kama wachungaji?! jibu hapana, siongei kama wachungaji Bali kama mwana wa Mungu, ni hivi,; Mara nyingi Yesu alijiita mwana wa Adamu akirejelea Adamu yule aliyeweza kutawala mazingira yake, hakuna mazingira yaliyomshinda Yesu, sio mazingira ya hali ya hewa, kifo, magonjwa, njaa na kila kitu juu ya uso wa dunia, Yesu Kristo alitawala mazingira yote akisema Yeye ni mwana wa Adamu, Yesu aliye Mungu alionyesha yote, akifundisha yote kwa binadamu.

Hata kufufuka kwake aliwafundisha binadamu, alifundisha kwanza binadamu ili aweze kutawala mazingira yake kwanza arudishe utii wake kwa Mungu, Yesu aliyekuwa katika umbo la MTU akionyesha binadamu mwenye nguvu katika utii kwa Baba yake (Mungu) alitaka binadamu tujifunze funzo, kumbuka alisema; Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani ameniweka wakfu niwaletee maskini habari njema. Amenituma niwatangazie mateka Uhuru wao, na vipofu watapata kuona tena, Amenituma niwakomboe wanaoonewa, nakutangaza mwaka wa neema ya Bwana.

kisoma kwa utulivu amesema Amenituma niwaletee mateka Uhuru wao, yeye Yesu hakuja kijeshi sasa mateka atakombolewaje?! na pia anasema awakomboe wanaoonewa, je yeye hakuwa na jeshi angewakomboaje?!, ukisoma kitabu cha ufunuo anasema; wewe unajisema Mimi ni tajiri, nimejitosheleza, sina haja na kitu chochote;' kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa, maskini, kipofu tena upo uchi.

Haya nayo hayo alisema, binadamu tulijiingiza kwenye hali mbaya sana pale tulipo asi, sasa Yesu alikuja kuturejeshea yote tuliyopoteza, kwanjia ya kumuamini yeye na kujirudisha utii kwa Mungu, kikawaida huku duniani tunajiona tumefanikiwa lakini kihalisi sisi ni masikini, kikawaida tunaambiwa adamu na Eva walipokula tunda macho yalifunguka ukweli ni kuwa macho Yale yanayoona yalifungwa, vazi la utukufu lilivuka, umasikini ulimvamia, unyonge ulimjia kwani alikuwa dhaifu mpaka Leo, binadamu hana namna yeyote ambayo anaweza akafanya kujiondoa kwenye hali hii isipokuwa kuonyesha utii kwa Mungu, Mungu anakuhitaji wewe na sio kikundi ndio maana anasema kwenye amri zake, usiue, usiibe, n.k anasema kwa nafasi ya MTU mmoja sio kwa kikundi amri azisemi msiibe, msizini, n.k Bali amri zinataka wewe peke yako usiibe n.k, huundio ufunguo wa kufungua na kupata kile tulichokipoteza.

Yesu alikuja kutuonyesha njia ya kurudisha hali tuliyopoteza, kama kila MTU akifanya mazoezi ya kurudisha alichopoteza basi itamfaa yeye vizuri, kama MTU anaanza kufanya mazoezi ya kuwa mwema, haimaanishi punde ulipoamua kuwa mwema utakuwa mwema, ni sawa na unapoanza kufunya mazoezi ya kupunguza mwili sio unapungua hapo hapo, ila angalau umeanza kuingia sehemu ya hali ya kale, hutaanza kuwa mwema ikitokea umekosea tena usikate tamaa, ukikosea jua ndio mwili unapungua, Fanya mazoezi taratibu, hata kwasiku ukitenda jema moja sio mbaya, kuna sehemu ya kale inakurudia, kesho ukitenda mawili ndivyo hali yako ya kale inavyokurudia, mwisho utakamilika kuwa yule adamu wa kale ambaye alikuwa na kila kitu, kama ni utajiri utakuwa nao na kama ni uzima utakuwa nao, kwani utaweza kutawala mazingira na kila kitu.

Wachawi ujifunza kwa shetani namna ya kutawala mazingira ndio maana wanaweza wakaifanya ardhi yako isizae sio kwamba kuna chaziada ila kufanya usifanikiwe tu, na kwa vile wewe huwezi kutawala mazingira basi unaishia kulaumu tu, lakini ukitenda mema na kuwa mtii kwa Mungu sio kwamba shetani hata kuroga na pia hata kusogelea kabisa kwani anajua wazi kuwa wewe umekuwa adamu wa kale mwenye nguvu hivyo atawanyoosha wengine lakini wewe utakuwa sawa, shetani hawezi kumsogelea MTU mwema, kwakuwa anajua huyu MTU anauwezo wa kutawala mazingira, nachochote atakacho amuru kitakuwa hivyo shetani anajua hataukiamuru yeye apate balaa nalo balaa litamfikia ndio maana lazima akukimbie, kwako shetani hatakuletea magonjwa, njaa wala umasikini kwani hawezi kufanya hivyo, ila atakuletea kila fursa ya dhambi iliutende uishiwe nguvu akunyooshe.

Shetani anajua hawezi kitu kwa MTU mwema sasa njia pekee ya kumshinda shetani na kuwa na misuli mikubwa ni kufanya mazoezi ya kutenda mema, anzataratibu mpaka kutenda mema iwe Tabia yako, Yesu alikuja kutuonyesha njia ya kufanya vizuri ilikumshinda shetani, shetani hashindwi kwa kusema ushindwe, au kusali sala ndefu, au kushinda kanisani, msikitini au kwenye mahekalu, shetani haogopi vikundi vya maombi ya kumkemea wala Yale maombi ya kufunga anga, bahari wala nchi kavu wala yakuzuia milimani, shetani hajali ukifunga bila kula hata usipoonja kitu mpaka ufe napo ajali na haogopi, kwani izo biashara ni kichekesho kwake, jiulize umefunga malangapi na umesali Mara ngapi lakini mambo bado, ni kwasababu hivyo vitu havitawali dunia na kuitiisha, ila utii kwa Mungu pekee vitakurudishia hali yako na kwa njia ya Yesu utapata kila unacho amuru, kumbuka Yesu alisema ukiwa na imani utauambia mti huu ng'oka ukajitupe baharini nao utakutii, imani huja kwa kusikia neno la Mungu, ukiamini na kutii utakuwa na kila kitu, utaitwa mchawi, utapanda shamba la wastani utavuna maradufu kwani unayo amri ya kufanya utakalo.

Je, Yesu sio alikuwa na mikate na visamaki vichache lakini alilisha watu elfu tano, je Elia hakula na mama mjane na mtoto unga kidogo na mafuta kidogo kwa muda wa miaka mitatu, je mke wa mwanafunzi wa unabii wa Elisha hakujaza vyombo vingi kwa mafuta machache kwenye chupa,?! kama inawezekana basi ili kupata unachotaka rudi kwanza kwa Mungu alafu mambo mengine yatakaa sawa, Yesu alisema tafuteni kwanza ufalme wa Mbinguni na Mengine mtazidishiwa.

Kupambana kwetu kuwe kwa wema nasio kupambania maisha, kama tutajiita tunapambana na maisha hatutashinda kila siku tutakuwa hatuna kwani shetani atakuzuia uendelee kupambana mpaka ufe, ila kama tutaelewa alichosema Yesu kuwa tutafute ufalme wa Mungu basi tutafanikiwa, kutafuta ufalme sio kwenda kanisani au kushinda msikitini kutwa nzima, Bali kutafuta ufalme ni kuamua kufanya mazoezi yakuwa mwema popote ulipo katika shughuli zako na katika maisha yako, utakapo onasasa kutenda mema imekuwa tabia basi jua umejaamisuli hata maisha yako yatabadilika kwani umasikini na magonjwa vitakimbia ila nafsi za dhambi zitakujia, kama unavyoangaika na maisha ukiwa mwema dhambi itakuwa inakuvizia ili shetani achukue nguvu za misuli yako na akurudishe kule, Yesu Kristo Bwana mkubwa wetu alituonyesha namna yakupata kila kitu, embu tufikirie kibiashara kama Yesu angetaka fedha, alipoongeza wale samaki na mikate kwa watu wale elfu tano kama angeuza angepata kiasi gani, vipi wale samaki baharini hadi mtumbwi au boti ya kina petro ilipotaka kupasuka kwa kujaa samaki je angekuwa na utajiri wa kiasi gani.

Haya je kwa Huduma ya pale harusini kana kwa kugeuza maji kuwa divai angelipwa kiasi gani?! kama angetaka angekuwa tajiri vipi umesahau alipomwambia petro akavue samaki na samaki wakwanza atakaye mvua atakuwa napesa mdomoni, je hapo napo anahitaji nini Yesu, hakika alikuwa tajiri na alitawala mazingira yake, Yesu hakuhitaji kitu ila Yeye alikula aliishi na kila alichotaka alipata, kumbuka hata punda mpya yule Yesu alipata, kwani alisema Mungu amempatia vyote, sasa alitutaka nasisi tuwe kama Yeye kwa kumwamini yeye na kumtii ili turudishe hali yetu tuliyoipoteza. binadamu alikuwa nauweza wakuiitisha dunia, yaani kutawala anga, upepo, bahari na kila kitu kilichopo mbele ya binadamu, ukisoma Zaburi ya 8 inasema; mtu ni nini, Ee Mungu, hata umfikirie, binadamu ni nini hata umjali? Umemfanya awe karibu kama mungu, umemvika fahari na heshima . ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote.

hapo mzaburi anasema binadamu amewekewa kazi zote za Mungu miguuni kwake, pia amefanywa awe karibu kama mungu (miungu) binadamu alipewa kuwa miungu yaani Mungu alimfanya binadamu atawale hata upepo, maji, na chochote kile, uweza wa binadamu ulikuwa niwakutisha mno, na hekima yake niyaajabu mno, wengi wamesoma kisa cha Eva na nyoka lakini wengi tumeacha kisa icho kama kilivyo, wengi tunafikiria kuwa nyoka aliyeongea na Eva alikuwa ni shetani aliyevaa umbo la nyoka, tunafikiri hivi kwasababu tunajua nyoka haongei, ukweli ni kuwa tunajidanganya wenyewe, kama aliyemdanganya Eva alikuwa ni shetani mwenye umbo la nyoka sasa tujiulize kwa nini Mungu alimuadhibu nyoka halisi, labda tufikirie, mwizi amechukua utambulisho wako na kumuibia mtu Fulani, je! wewe ndiye utakaye fungwa?, labda niseme msemo mwingine, mwizi amejidai nyumba yako ni yake na kumtapeli mtu, je! wewe utawajibika na matendo ya mwizi?

Kama ni hapana, sasa kwa nini nyoka apate adhabu Kali namna ile kwa kosa lisilo lake,?! ukweli ni kuwa hekima ya binadamu ilikuwa kubwa na kilicho mfanya binadamu aanguke dhambini ni kuwa na tamaa, Eva alitamani kuujua uovu, alikuwa anajua wazi wazi kabisa kula tunda ni kosa ila aliamua, na pia hata Mungu alipomwambia adamu kwamba uliamua kumsikiliza mkeo na wewe ukala tunda la mti niliokukataza usile, Mungu asinge muadhibu Eva kama angekuwa hana hatia, Eva naye aliamua kwa tamaa na kiburi kabisa kuasi ndio maana Mungu aliadhibu, Mungu sikuzote anaangalia moyo(nia) na akisha jua nia ya MTU hapo anatambulika ni mwema au mbaya,. binadamu alipoasi aligeuka, macho yakajifunga na alikuwa kiumbe dhaifu mpaka adamu mwenyewe aligundua mabadiliko makubwa, vazi la utukufu alilovikwa lika vuka, akaona haya na aliposikia Mungu akija alikimbia, kwa nini alikimbia wakati alijishonea vazi la miti?

Ni kwasababu alijua Mungu angeshangaa vazi bovu la miti alikolitoa, adamu alijua amechanganya mambo ndio maana alikimbia, ukitaka kujua kuwa binadamu alikuwa na uweza mkubwa, angalia Mungu alisema na nyoka na binadamu alisema na nyoka, Mungu alimwambia nyoka adhabu zake na binadamu hapa anaonekana Eva anasema na nyoka na wanakubaliana kula tunda na kumwasi Mungu, lengo la nyoka na shetani linatimia na adhabu za shetani Mungu anataja hapa kwenye ufunuo 18...." kisha nikasikia sauti nyingine ikitoka mbinguni ikisema, "watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake. kwa maana dhambi zake zimekuwa nyingi mno, zimerundikana mpaka mbinguni, na Mungu ameyakumbuka maovu yake.

Mtendeeni kama alivyo watendeeni nyinyi; mlipeni Mara mbili kwa Yale aliyoyatenda. mchanganyieni kikombeni mwake kinywaji kikali maradufu. mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake, kulingana na kuishi kwake kwa anasa.

Maana anajisemea moyoni: ' Ninaketi hapa; Mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!'
kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwa moto, maana Bwana Mungu mwenye kuhukumu ana nguvu."...itaendele
 
Back
Top Bottom