Wazungu wachanganyikiwa, wahaha kuokoa dili na Afrika Kusini

Tunawauliza kama ni upuuzi nani kaonewa...nani ambaye kapelekwa kubakiwa makosa?

Nakuuliza tena......

Nipe sababu ya haya Mataifa kutojiunga Ama wanaogopa nini kujiunga na hicho kichaka kinacho itwa ICC.....???

Marekani
Israel
China
Urusi nk.
 
Hii ya kujitoa ikiendelea wengine tutakosa hoja ya kuwaambia watu wetu pale mambo yanapokuwa magumu. Maana huko ndio kulikuwa kwa kujiliwazia...ha ha haaa umenikumbusha Uchaguzi 2015
 
Kama haina faida vipi kunafada

1. Nkrunziza anavofanya....?

2. Kunafaida yoyote maafa ya Daful

3. Kunafaida yoyote katiba inasema kabila hana sifa kuendelea kuongoza DRC

Nin mtazamo wako kuepukana na matatizo ya watawala wa kidikiteta kama wapo au kama watakuwepo.....watashughulikiwaje?

Ni ajabu sana Afrika ina nchi zaidi ya 50 lkn ulizozitaja hata 5 hazifiki lkn unataka kufanya kama vile Afrika yetu ina matatizo ya kipekee hapa Duniani wkt siyo kweli, tuna matatizo ndiyo lkn wapi hakuna ?
 
Waafrika tumeanza kujielewa,n ingependeza gaddafi angekuwa hai
Wanaoshabikia kujitoa ICC ni viongozi, tena wakati mwingine bila hata kushirikisha wananchi wao kupitia bunge au referendum. Swali ni kwa nini viongozi hawa washabikia kujitoa kwenye hii mahakama? Jibu ni rahisi ili kusiwe na chombo cha kuwabana wanapofanya uhalifu kwenye nchi zao...
 
Kwani ni nchi gani Dunia hii ambapo wananchi huamua badala ya Viongozi?
 
Nchi za Africa zinaongozwa na madikteta ndio maana tuzo ya MO Ibrahim ina hang coz hakuna mwenye sifa sasa leo tunafurahi kujiondoa ICC du kweli hili bara limelaanika
 
Siwezi kuwa 1 kati ya wale 4 ambamo utafiti unasema ukichaa

Am off in this thread.
 
Hakina faida kwetu na ndiyo maana tunajitoa!
Mnajitoa ili muendelee kukandamiza na kuuwa wanyonge, kuharibu chaguzi na kupora ushindi, kuiba fedha za umma na kuzificha ulaya, kuendeleza rushwa na vitendo vya kifisadi bila kuulizwa au kuingiliwa na chombo chochote, maana mahakama zenu na vyombo vya dola mmeviweka kwenye mifuko yenu mipana. Hii ndiyo sababu kubwa kwa nchi za Africa zinazojidai kujitoa.
 
Uamuzi wa Afrika Kusini kuondoka ICC haujafikiwa leo ni wa muda mrefu.

Afrika Kusini walisaini mkataba wa Rome Statute of the ICC mwaka 1998.

Halafu ikaufanya kuwa sheria nchini humo iloitwa Implementation of the Rome Statute of the International Criminal Court Act 27 mwaka 2002, na baadae ikaja kuwa sheria kamili August 16, mwaka 2002.

Inabidi kufanya taratibu za kurekebisha hizi sheria mbili ya ndani ambayo pia ilishindwa kuifuata khasa pale waliposhindwa kumkamata rais Bashir wa Sudan ili apelekwe ICC.

Nionavyo mimi, Afrika inatakiwa iwe na kitengo cha mahakama ya Afrika pale AU ili kuweza kushughulika na mambo ya Afrika ndani ya Afrika.

Afrika wana fedha kama hawana watafute waanzishe mahakama hii na ionekane inafanya kazi.

Lakini ICC kuanza ku-pinpoint nani wa kuleta kule The hague ni kama kitendo cha kuita mbwa kwa mluzi au "dog whistling"

ICC ni kwa wahalifu wa nchi za magharibi na USA ambazo zenyewe hazikujiunga tangu mwanzo.
Ahsante Mkuu nimeipata na nimekuelewa.....

Tumeona Raia wengi wakifa kutokana na mapigano yalitokea na yanayo endelea huko...
Iraq
libya
Syria
Afghanistan
Ukraine
Yemen Na Palestina...

Na wahusika wanajulikana na hivi vichaka vinavyo inatwa ICC na UN haina vichwa wala meno wala mguu zaidi kuwakodolea macho tuu.

Huu ndio mda wa Africa kuanza kumka ila kuna viongozi wachache ni wanafki ambao hawana msimamo.
 
Mnajitoa ili muendelee kukandamiza na kuuwa wanyonge, kuharibu chaguzi na kupora ushindi, kuiba fedha za umma na kuzificha ulaya, kuendeleza rushwa na vitendo vya kifisadi bila kuulizwa au kuingiliwa na chombo chochote, maana mahakama zenu na vyombo vya dola mmeviweka kwenye mifuko yenu mipana. Hii ndiyo sababu kubwa kwa nchi za Africa zinazojidai kujitoa.

Ni mawazo yako una haki pia ya kufikiria hivyo!
 
Wanaoshabikia kujitoa ICC ni viongozi, tena wakati mwingine bila hata kushirikisha wananchi wao kupitia bunge au referendum. Swali ni kwa nini viongozi hawa washabikia kujitoa kwenye hii mahakama? Jibu ni rahisi ili kusiwe na chombo cha kuwabana wanapofanya uhalifu kwenye nchi zao...
Nitajie Nchi ambayo aliyotaka kujiondoa ktk hiyo Mahakama ya ICC bila kupelekwa Muswada Bungeni.....??
 
Uamuzi wa Afrika Kusini kuondoka ICC haujafikiwa leo ni wa muda mrefu.

Afrika Kusini walisaini mkataba wa Rome Statute of the ICC mwaka 1998.

Halafu ikaufanya kuwa sheria nchini humo iloitwa Implementation of the Rome Statute of the International Criminal Court Act 27 mwaka 2002, na baadae ikaja kuwa sheria kamili August 16, mwaka 2002.

Inabidi kufanya taratibu za kurekebisha hizi sheria mbili ya ndani ambayo pia ilishindwa kuifuata khasa pale waliposhindwa kumkamata rais Bashir wa Sudan ili apelekwe ICC.

Nionavyo mimi, Afrika inatakiwa iwe na kitengo cha mahakama ya Afrika pale AU ili kuweza kushughulika na mambo ya Afrika ndani ya Afrika.

Afrika wana fedha kama hawana watafute waanzishe mahakama hii na ionekane inafanya kazi.

Lakini ICC kuanza ku-pinpoint nani wa kuleta kule The hague ni kama kitendo cha kuita mbwa kwa mluzi au "dog whistling"

ICC ni kwa wahalifu wa nchi za magharibi na USA ambazo zenyewe hazikujiunga tangu mwanzo.
... Hivi AU bado ipo kwa maana ya kutimiza malengo yake makuu au imebaki tu kama kijiwe cha viongozi kukutana na kuteteana?
 
Kwani ni nchi gani Dunia hii ambapo wananchi huamua badala ya Viongozi?
Viongozi wanatakiwa wapate ridhaa ya wananchi wanawaongoza kupitia vyombo vyao vya uwakilishi au kura za maoni. Viongozi wabinafsi ndio wanaokimbilia kuamua mambo bila ku involve wananchi wao. Jambo la kushangaza ni kwamba kama unaendesha nchi yako kwa kufuata misingi yote ya utawala bora, na wananchi wako wakukubali, why worry about ICC? Woote Wanaoshabikia kujitoa wana wasi wasi na utawala wao mfano Burundi, Kenya etc
 
Marekani, Urusi, China, Israel, India na Nchi kibao tuu hawajajiunga na upuuzi huu unaitwa ICC.

Nataka utuambie sababu ya Wao kutojiunga au wanaogopa nini kujiunga na hicho kichaka Chao kinacho itwa ICC.......????

Naomba utuambie Mkuu alafu ndio utajua kwanini sisi Waafrika tusianza kujiondoa.

mkuu kwahiyo jambo jema hatuwez kushiriki mpaka hizo nchi ulizozitaja zishiriki? alaf kwann viongoz wetu wajitoe kipind cha matatizo ktk vipindi ambavyo wanaanza kustakiwa, kwann wasijitoe ktk kipind cha amani muda ambao viongoz wetu wanapendwa na kushabikiwa na wananchi wao? hao viongoz wanaotaka kujitoa walijiunga wenyewe huko icc ambayo wew unaiita upuuz, lkn kuna mdau mmoja kachangia vzr tukijitoa bas tusiache vacuum tuanzishe ya kwetu africa ambayo itawashtak kama icc.. japo napata ukakas kama kweli tunaweza kuanzisha na kustaki viongoz wetu kama icc kama sio kulindana kama tunavyoona sasa kwa AU. kimsingi viongoz wetu hawana jeuri ya kupelekana mahakamani wenyewe kwa wenyewe. lkn kitu kizur kat ya viongoz wote waliopelekwa icc hakuna hata mmoja ambae ameonewa au kusingiziwa ingekua vinginevyo hata mimi ningekua shabiki wa kujitoa,, kwa sasa tuendelee tu kwa lengo lile lile wkt tunasaini hiyo mikataba
 
Baada ya nchi ya AK kuamua kuachana na ICC sasa Wazungu wanahaha huku na kule kujaribu kuzuia hili gharika wamekwenda mbali na kuwataka AK waseme wanachotaka kiwe reformed na kwamba AK watapewa special treatment lkn AK wamegoma!

Kinachowagopesha Wazungu ni umuhimu wa nchi hiyo Afrika na kwamba wimbi la nchi za Kiafrika litafwatia na Wazungu kupoteza sehemu pekee ambayo walikuwa na uwezo wa kumiliki binadamu!

Ikumbukwe kwamba kwa nchi nyingine zote Duniani uanachama wa ICC ni hiari na wapo waliojiunga na kujitoa na wapo waliogoma kabisa kujiunga lkn kwa Afrika siyo hiari bali ni lazima na ndiyo maana Dunia nzima inajadili kujitoa kwa AK lkn haijadili kukataa kwa USA kujiunga na Mahakama hiyo!
Na cha ajabu labda klk vyote USA ambaye amekataa kujiunga na amesema kamwe raia wake hatopelekwa kushitakiwa nje ya USA ndiyo wanaowagomea AK kujitoa na ICC sasa kwa nini wao hawataki kujiunga nayo?

Baadhi ya nchi nyingine zilizogoma kujiunga au kujitoa ni Israeli, India, China, Indonesia lkn hakuna hata anayejua kama hizi ni Wanachama wa ICC au la, lkn kwa Afrika Dunia nzima inajadili kujitoa kwa AK, swali linakuja ni kwa nini?

Sasa kwa kuwa J. Zuma kaamua kumwaga Mboga, ajitayarishe na civil unrest, AK itakumbwa na maandamano makubwa siajabu hayajawahi kutokea ambayo yanaweza yakaleta Mapinduzi AK na ANC kuondolewa madarakani, na kuwekwa puppet Government, stay tuned!
Wazungu hawawezi kukubali kuipoteza Afrika kirahisi, Afrika ni mtoto wa Mzungu!

Mbona Burundi umewasahau?

South Africa & Burundi Move to Pull Out of International Criminal Court
October 21, 2016
Headlines
South Africa has begun the formal process to withdraw from the International Criminal Court. The news comes just two days after another African nation, Burundi, became the first country to ever pull out of the court. Over the years, the court has been accused of disproportionately targeting African leaders. Human Rights Watch criticized South Africa’s move. The group said, "South Africa’s proposed withdrawal from the International Criminal Court shows startling disregard for justice from a country long seen as a global leader on accountability for victims of the gravest crimes.”

Source:
 
China akitutawala nrio tutajua kwamba tumeruka mkojo na kukanyaga mav!
China ni mshirika mzuri asiye na masharti ya kipuuzi ambaye hana makuu tofauti na hao Wamagharibi wanataka tuunge ndoa za jinsia moja na ukigaidi basi vikwazo vinakunyemela.
 
Back
Top Bottom