Wazungu wachanganyikiwa, wahaha kuokoa dili na Afrika Kusini

Nchi za Africa zinaongozwa na madikteta ndio maana tuzo ya MO Ibrahim ina hang coz hakuna mwenye sifa sasa leo tunafurahi kujiondoa ICC du kweli hili bara limelaanika
Kwahy wa Africa hamuwezi kufanya jambo mpk muwashirikishe ma masters wenu

Africa tutaendelea kutawaliwa miaka mingi ase ,kila kitu ni dependent ..bado tuna fikra ya kutawaliwa tawaliwa tu
 
mkuu kwahiyo jambo jema hatuwez kushiriki mpaka hizo nchi ulizozitaja zishiriki? alaf kwann viongoz wetu wajitoe kipind cha matatizo ktk vipindi ambavyo wanaanza kustakiwa, kwann wasijitoe ktk kipind cha amani muda ambao viongoz wetu wanapendwa na kushabikiwa na wananchi wao? hao viongoz wanaotaka kujitoa walijiunga wenyewe huko icc ambayo wew unaiita upuuz, lkn kuna mdau mmoja kachangia vzr tukijitoa bas tusiache vacuum tuanzishe ya kwetu africa ambayo itawashtak kama icc.. japo napata ukakas kama kweli tunaweza kuanzisha na kustaki viongoz wetu kama icc kama sio kulindana kama tunavyoona sasa kwa AU. kimsingi viongoz wetu hawana jeuri ya kupelekana mahakamani wenyewe kwa wenyewe. lkn kitu kizur kat ya viongoz wote waliopelekwa icc hakuna hata mmoja ambae ameonewa au kusingiziwa ingekua vinginevyo hata mimi ningekua shabiki wa kujitoa,, kwa sasa tuendelee tu kwa lengo lile lile wkt tunasaini hiyo mikataba
Hakuna jibu ulilo toa hapo...!!!

Na kama hizo Nchi zingekuwepo kwenye huo mkataba wa Rome ICC unazani hayo mauwaji yanayo tokea ktk kama Libya, Palestina, Yemen, Syria, Afghanistan, Iraq Ukraine nk.
Hizo Nchi zisinge tokea mauaji ya kutisha namna hiyo.

Ila tuu western na paka Wao Marekani ndio chanzo cha machafuko ktk Nchi mbali mbali Duniani.

Je hao watafikishwa ktk Mahakama ipi japo Wao wauwaji wakuu na waharibifu ktk miundo mbinu ktk Nchi za watu. .....???
 
Mugabe kwenye speech yake ya kuaga uwenyekiti wa AU mwezi February nilimuelewa sana

Alisema kwann hakuna nchi ya Africa kwenye UN security council ,kuna haja gani ya wa Africa kuhudhuria ikiwa kazi yao ni kusema yes kwenye kila jambo na hawana usemi wowote na hawaruhusiwi kuchangia ,alitishia kuondoa japo kuna watu hawakumwelewa

Kwann mataifa walioanzisha hyo mahakama hawajajiunga?

Africans bado tupo utumwani kuanzia UN,ICC nk nk

AU ianzishe mahakama yke ambayo ita deal na matatizo ya wa Africa kama kuna kiongozi ambaye ameenda kinyume na maadili atatengwa na kuchukuliwa hatua

Ni ujinga kutegemea ICC mahakama isiyo kuwa na haki wao wakifanya maujinga hawashitakiwi ila wa Africa fasta wakamatwe

Sitetei ma dictator lkn sipendi utumwa ukiendelea kwann kila jambo la ss wa Africa tuwapeleke ma master watuamulie ?? Halafu wao wala hawapo huko ICC

Ni time ya wa Africa kusimama na kufanya maamuzi..AU ipo waanzishe sheria na mahakama zao

UN watuendeshe na huku pia watuendeshe

Aaah
 
UK ilijitoa EU kwa kufuata matakwa ya wananchi yaliyofikiwa kupitia kura.

AK inajitoa wananchi wanakasirika viongozi wanatia pamba maskioni, kwanini wasiitishe kura? Huu upuuzi wa viongozi kujiamulia na kusigina katiba ndiyo unafanya watu waone haipaswi kujitoa ICC ingekua uongozi unafuata katiba hata wananchi wasingeona shida wewe kujitoa.
Kuna mdau kasema AU kuwe na mahakama ya kuwajibisha nchi za Afrika, wasafi kidemokrasia Afrika wanahesabika nani atamshtaki mwenzie?
Hata huko kuna wachafu ndiyo lakini angalau wenzetu utamtukana raisi na itakua umeexercise freedom of speech huku kwetu either uandae milioni saba au kipigo.

Wadau tufikirie vizuri kabla hatujashabikia huku kujitoa.
 
Kujitoa baada ya kuona una sifa zote za kushtakiwa haileti maana. Ikiwezekana basi tuunde yetu na iwe na Nguvu, coz unyanyasaji ya hawa watawala wetu utazidi sana wakijua hawana pa kushtakiwa
 
Ikumbukwe kwamba kwa nchi nyingine zote Duniani uanachama wa ICC ni hiari na wapo waliojiunga na kujitoa na wapo waliogoma kabisa kujiunga lkn kwa Afrika siyo hiari bali ni lazima


Mkuu, sio sahihi kwamba African States zote ni lazima ziwe wanachama wa ICC. Hapana!

Since its establishment in July 1998 Rome-Italy, membership to the ICC is not compulsory, bali ni hiari ya nchi husika, worldwide. Na ndiyo maana mpaka leo hii, huko huko kwa wazungu kuna nchi ambazo ni wanachama wa ICC, na kuna nchi ambazo sio wanachama wa ICC.

Vile vile kwa hapa Africa, mpaka leo hii, African state parties to ICC ni nchi 34 TU! Lakini kumbuka kuwa bara lote la Africa lina nchi 54. That means, kuna nchi 20 (za Africa) bado sio wanachama wa ICC. Mfano wa karibu kabisa ni RWANDA. Mpaka dakika hii, Rwanda haitaki kabisa kuwa mwanachama wa ICC. SUDANI pia, n.k

The States Parties to the Rome Statute :
ICC.JPG


Hivyo basi, uanachama wa ICC sio lazima kwa nchi za Africa, bali ni hiari kwa nchi yoyote duniani pote. Na ndiyo maana Mkataba wa Roma (Rome Statute) ambao ndiyo Sheria ya ICC, unaruhusu member state yoyote kujitoa uanachama wakati wowote ule:

ICC2.JPG


Ila 'ujanja' waliotumia wazungu, ni kwenye hiyo 'Withdrawal' (kujitoa uanachama). Kwamba, hata kama nchi itajitoa uanachama, bado obligations zote za nchi hiyo to the ICC zita-remain intact. Kujitoa uanachama, haifuti 'wajibu' wa nchi hiyo kwenye ICC. Hapa ndo wazungu walicheza kama Pele ili kuwanyoosha 'watawala wa kiafrica' !

-Kaveli-
 
Nimehoji hapo juu

1. kama hakuna hata mmoja alionewa...hofu ya kujitoa knatoka wapi?

2. Mbona jana na kila siku unakula chakula hujasema huli mpaka mzungu ale ndo utakula (namaanisha unakula kwasababu ni busara na nijambo jema kula kilichochema na hujahitaji mzungu)

......
Hapo kwa namba moja umeuliza swali la msingi but la namba mbili liko illogical!! Cha kushangaza zaidi umesahau kuwa migogoro mingi inayosababisha vita na umwagaji damu na huko wanakokuita uhalifu wa kivita wanaochochea ni wao wazungu halafu mwisho wa cku wanawapelekeni ICC.
Wakati mwingine kabla hujaandika ufikirie kwa kina.
 
AU ipo na ndiyo chombo ch waafrika, hivyo tusikidharau.

...Chombo cha waafrika sawa, but kwa maslahi ya nani? Warundi majuzi walikuwa wanauwana hapa, AU imefanya nini? Huko DRC nako hali si swari, wamechukua hatua gani? As said earlier hicho ni kijiwe kwa maslahi ya wateule fulani...
 
...Chombo cha waafrika sawa, but kwa maslahi ya nani? Warundi majuzi walikuwa wanauwana hapa, AU imefanya nini? Huko DRC nako hali si swari, wamechukua hatua gani? As said earlier hicho ni kijiwe kwa maslahi ya wateule fulani...

ICC ni chombo cha nani na kwanini hakiwapeleki tha Hague viongozi wa Ulaya na Marekani wanaoua watu kwa mabomu?

Ni vizuri sasa huko tuendako kunaleta picha ya nchi mbalimbali kujikusanya kwa uhusiano ulio na manufaa zaidi kuliko kumsikiliza mtu ambae anafanya "double standards".

Huko DRC kuna nchi za magharibi ambazo wamegawana nchi hiyo (nadhani unafahamu hili).

Hali kadhalika Burundi nani anawauzia silaha waasi?
 
Daah!!
Kujitoa siyo jambo zuri saana.
Tutatakiwa kuishi kikorea korea dizaini
 
ICC ni chombo cha nani na kwanini hakiwapeleki tha Hague viongozi wa Ulaya na Marekani wanaoua watu kwa mabomu?

Ni vizuri sasa huko tuendako kunaleta picha ya nchi mbalimbali kujikusanya kwa uhusiano ulio na manufaa zaidi kuliko kumsikiliza mtu ambae anafanya "double standards".

Huko DRC kuna nchi za magharibi ambazo wamegawana nchi hiyo (nadhani unafahamu hili).

Hali kadhalika Burundi nani anawauzia silaha waasi?
Hadithi ile ile ya kila kitu kumlaumu mzungu... Ila Mkitaka kwenda kutanua, kuzungusha bakuli la kuomba misaada, kuficha fedha mlizotuibia na kununua mapangaboi Wazungu wanakuwa wadau wa Maendeleo na marafiki wakubwa..
 
Hadithi ile ile ya kila kitu kumlaumu mzungu... Ila Mkitaka kwenda kutanua, kuzungusha bakuli la kuomba misaada, kuficha fedha mlizotuibia na kununua mapangaboi Wazungu wanakuwa wadau wa Maendeleo na marafiki wakubwa..

Unachotetea wewe ni nini?

Kuna mambo mengine Afrika ni lazima ifanye kivyake kama wengine wanavyofanya, yaani kuwa na maamuzi ya kivyao ambayo hayahusiani na sera za mahusiano ya nje.

Lakini wakati mwingine yanaweza kuhusisha diplomasia na kuiingilia.

Mojawapo ni kuondoka ICC maana tangu kuanzishwa kwake kesi zake nyingi ni zile zinazowahusu waafrika.

Amka ndugu sasa, wakati umewadia wa kufikiri nje ya boksi.
 
Hiyo ICC ni Mahakama maalum kwa Third World countries.
Toka Vita vya pili ya dunia serikali ya Marekani imesababisha vifo vya watu million 20 kwa vita mbali mbali ilivyovileta na kuanzisha mbona hakuna hata kiongozi ama askari mmoja wa Marekani amefikishwa the ICC
 
Nimehoji hapo juu

1. kama hakuna hata mmoja alionewa...hofu ya kujitoa knatoka wapi?

2. Mbona jana na kila siku unakula chakula hujasema huli mpaka mzungu ale ndo utakula (namaanisha unakula kwasababu ni busara na nijambo jema kula kilichochema na hujahitaji mzungu)

......
Una akili timamu wewe?,kwan huo ugali tulipika wote na mzngu mpaka tule wote?. Hoja hapa tunashirikiana kuandaa ugali(ICC) ukiiva halafu yeye anasepa hataki kula anakuachia msosi wote tena tuliandaa ugali/ICC ya wote,kyeee na mimi naacha kula
 
Wajitoe wote waimarishe dictatorship Africa. Viongozi wa Afrika wanamiliki Nchi na vilivyomo ndani yake ndio maana wanajiamulia watakavyo bila kuwashirikisha wananchi. Madhara yake yatafuatia.
 
Back
Top Bottom