Waziri wa nishati na madini na mgawo wa umeme wa kimya kimya

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
987
Ni zaidi ya wiki sasa.mgawo wa umeme unaendelea lakini hakuna taarifa yoyote toka tanesco au mamlaka yoyote ya serikali. Hivi karibuni prof muhongo alikuja na mkwara na mbwembwe za hali ya juu na kutuaminisha kuwa sasa mgawo ni historia. Kazi imemshinda?ameshindwa kutembea kauli zake?ni jambo la dharura? Au ni tatizo lililo nje ya uwezo wake.
 
Ni zaidi ya wiki sasa.mgawo wa umeme unaendelea lakini hakuna taarifa yoyote toka tanesco au mamlaka yoyote ya serikali. Hivi karibuniprof muhongo alikuja na mkwara na mbwembwe za hali ya juu na kutuaminisha kuwa sasa mgawo ni historia. Kazi imemshinda?ameshindwa kutembea kauli zake?ni jambo la dharura? Au ni tatizo lililo nje ya uwezo wake.

Ooops!
 
Wanachokifanya waziri Muhongo na Tanesco ni diplomasia kali ya mgao. Umeme haupo wa kutosha, kwa hiyo visingizio
vya upungufu wa umeme vinatafutwa. Kwanza walikuja na gia ya kutengeneza nguzo mbovu ili kuepusha zisianguke pindi mvua zilizotabiriwa zitakapoanza. Walisema zoezi hili lingechukua wiki mbili kuanzia septemba 12. Kwa hiyo kukatikakatika kwa umeme kipindi hicho kilikuwa ni kwa ajili ya ukarabati wa nguzo. Baada ya muda huo kwisha, ikaundwa diplomasia nyingine kwa mikoa ya arusha, kilimanjaro na tanga: kwamba kuna kazi ya kutengeneza nguzo kwenye njia za msongo mkubwa. Kwa mikoa hiyo, umeme ulikatwa Jumamosi tarehe 6/10 na jumapili tarehe 7/10 kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa moja jioni. Hatujui jumatatu 8/10 itakuwaje. Huenda diplomasia hii ya mgawo ikaendelea na kuhusisha mikoa mingi zaidi.
Hayo ni mawazo yangu tu- nionavyo hali iliivyo ndani ya tanesco na wizarani - hawapendi kusema ukweli wa mambo!
 
Watasema tu we subiri kidogo
 
Dodoma si rahisi sana kuwa na migao ya umeme na ikiwapo huwa ni kwa muda mfupi sana tofauti na mikoa mingine, lakini naona mambo magumu. Karibu siku nzima YA JANA HAKUKUWA NA UMEME KABISA. Maji shingoni Prof Muhongo.
 
Nafikiri Prof Muhongo, Maswi na timu yao wanajitahidi sana kwa kadri ya uwezo wao.......!Tegemea watakumbana na kukatishwa tamaa na wale aliowazibia kamuhogo kao...!

Sasa hivi Tanesco wanachokiomba ni mvua inyeshe, kwani maji yanayotumika kusukuma mitambo yapo chini ya kiasi kinachotakiwa....hapa ni pamoja na kutumia mitambo yote ya dharura kutoa umeme uliopo kwa sasa. Watangulizi wao, nchi ingekuwa gizani kwa zaidi ya masaa 14 kwa hali hii....!

Kibanga Msese
 
tell people the truth, a lie is just a quick and short fix wont help you in the long run, mr profesa.
 
Mhh...! huku boko umeme wamekata kuanzia saa mbili asubuhi mpka saa nne na nusu usiku. Kweli tanesco kazi imewashnda.
 
Laiti wakubwa wangejua kuwa watanzania siyo rahisi kudanyanga namna hiyo. Matatizo ya sekta hii yanajulikana na mikakati ya kuitanzua ipo kama viongozi wangetumia wataalam wetu ambao wanaujuzi na ueledi wa kutosha. Badala ya kufanya hivyo wenye taaluma za mawe na stashahada za uhasibu wanaamini wanamajibu ya changamoto zilizopo. I thought most of technical problems have a technical solutions but to these guys a political solutions appeared to be better. Well lets not forget that it is always very funny how pride goes before a fall. Kwa bahati mbaya sana madhara ya kuchemsha kwa viongozi katika sekta hii yanaweza kuwa makubwa sana kwa uchumi wa nchi hii na hii inadhihirishwa na kauli ya hivi karibuni ya IMF ambao walishauri kuwa uchumi wa nchi bado ni mzuri isipokuwa upo wasi wasi mkubwa kwenye sekta ya umeme. Ni vyema ieleweke kuwa masuala ya kitaalamu hayahitaji ubabaishaji.
 
Huku Mbezi hakuna umeme kuanzia saa 8:00am mpaka sasa hivi nivyoandika hii post..

Vijana msikilize radio jamani mbona tanesco walishatoa taarifa kwamba mbezi yote hakutokua na umeme! Fuatilieni habari kwanza!!
 
nilimsikia kwa masikio yangu, meneja mmoja wa mkoa akilumbana na bosi wake kuwa megawat 15 alizopewa kama magao kwa mkoa wake hazitoshi, tena akasema kwa mkazo kwenye simu "haya mambo ya kudanganya wanachi yanatupa shida sana,...mwenzake akamwonya kuwa akisema siku nyingine hivyo atafukuzwa kazi
 
Back
Top Bottom