Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba: Naagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye, achukuliwe hatua

Yes ...kila mtu atimize wajibu kwa mujibu wa sheria ....leo ukicheka yanamtokea Nape jiulize wewe usiyejulikana hata nyumba ya pili watakufanya nini ....Mwigulu umefanya vyema
Tatizo hatutajua kitacho fanyika. Hapo ndo mwisho Wa story kaka
 
Najaribu kuwaza na kukumbuka nyuma, kipindi kile ambacho mabomu ya likuwa yanarindima kwenye mikutano ya CHADEMA. Police walikuwa wamefanya mikutano ya CHADEMA kama ndio vituo vyao vya kazi.
Leo hii Nape kaonyeshwa BASTOLA tu imekuwa ndio issue kubwa.
Najaribu kuwaza tu je CHADEMA wamesahau yote haya mpaka wamekaa kimya. Nilitegemea sana wao ndio wangekuwa wakwanza kusema kuwa "Nape tulia hayo ni mambo ya kawaida", au ndio ile Mkuki kwa nguruwe............................
Nawaza tu.
 
Lakini daudi bashite asifanywe lolote...ila linda kibarua chako tu mkuu hamna namna kuna watu ukiwagusa utayapata ya nape
 
Sasa mbn ya uyo jamaa imekua haraka kutoa tamko?ya wale wa clouds mlikaa kimya tu,au urafiki time?
 
Hongera sana Mwigulu Nchemba. Angalau umenena. Tulikuwa tunajihoji ukimya wako kwa jambo hili. Hivi ni kweli huyu Nape tunayemfahamu ndo anatolewa bastola hadharani! Nadhani aliyumwa kuua kabisa.

Hivi mwigulu unaamani ya moyo kabisa au ni utamu wa madaraka tu? Mbona mnamwacha mwenzenu mikononi mwa Simba peke yake? Ina maana ninyi mawaziri hamna umoja? Kila mtu afe kivyake? Hata watoto wa shule ya msingi mwenzao akigongwa na bodaboda au gari huandamana kutaka matuta yajengwe. Ninyi hamtaki haki itendeka kwa mwenzetu? Shame on You!
 
View attachment 485970
Mwigulu Nchemba(Kushoto) akizungumza na Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma 10/15/2014(Maktaba)

Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.

Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.
======

View attachment 486002
Katika ccm vijana hodari ninao wajua ni wewe Mwigulu, Nape, Januari, na Bashe!!! Tupo pamoja
 
Hujui Mtoto wa Baba katoa instruction,na yeye anafuata Mkondo wa Maji sasa hivi.Alichelewa kwenye Clouds,hakuwaona kama Clouds ni Watanzania??Je hakuwaona kama Lissu,Lema na wapinzani wengine wakishikiwa Bunduki na Polisi kama kumi hivi,duh,Mwigulu acha double standard anza upya

Kila jambo na wakati wake hata vitani sio busara kufyatua risasi zote, Hii sinema haitaki papara
 
Kweli huyu askari lazima atafutwe na ahojiwe kwa sababu NAPE alitaka kitabulisho yeye akatoa bastola harafu mbaya zaidi alikoki na kuanza kurukaruka sasa ingefyatuka gafla na kumpata NAPE, nakwambia BASHITE nyumba yako ingechomwa moto na wewe lazima tungekatakata hicho kinye..... kinanachowazingua watu mpaka wanaamua Kibashitebashite
 
Jamani huyu Daudi bashite zero mbona amepanda watu kichwani yani amekuwa untouchable kabisa hivi wale waandishi wasingekuwepo si angeweza kuua jamani. Kweli fa fa fa ni mbaya mno

Mambo.. Bashite hakamatiki, ni kama ana mamlaka kama ya Rais, ukimgusa Bashite au maslahi yake umemgusa Faru John, yaan Faru John yuko ndani ya Bashite na Bashite yu ndani yake.

Yaan ni ngumu sana kuwatenganisha hawa wasukuma wawili. Tushaambiwa tulie tugaregare hamna kitakachobadilika. Bashite hata akimuua mtu leo, kelele zitapigwa sana tu ila ataambiwa aendelee na kazi na watu wachape kazi waache kupoteza mda.

Tanzania bado sana.
 
Kati ya mawaziri siwapendi ni huyu. Muuza ngada halafu anafanya kazi kwa kutaka sifa. aende chadema aone kama ccm itakufa. sijawah mpenda hata. ubishoo tu
 
Lakini Bwana waziri swali la kujiuliza ni je, kama jambo la awali, ni nani aliyezuia Nape kuongea na waandishi habari ilhali ni haki yake ya msingi kujieleza na kutoa maoni yake? Kuna mambo matatu ambayo ni jukumu la kila kiongozi mwenye dhamana kuyapigania kwa nguvu zake zote: utawala wa sheria, mgawanyo wa madaraka ya dola na kuwepo kwa 'checks and balances' katika uendeshaji wa nchi. Kama rais anaonyesha dalili zozote za kutokuzingatia haya mambo, ni jukumu lenu kama wasaidizi wake kumueleza 'blatantly' kwamba hii ndio njia sahihi; kinyume chake ni nchi kufuata nyayo za Somalia.

Kuhusu askari aliyemyooshea Nape bunduki, kwa mtu yeyote aliyepata mafunzo ya kijeshi hatapata taabu kuelewa hayo mazingira. Siku zote askari anatenda (react) kulingana na aina ya amri aliyopewa. Nauliza tena, ni nani aliyetoa amri ya kuzuia mkutano wa Nape na waandishi wa habari?
 
Ki u halisia ,Ma waziri wote hawana Nguvu awamu hii naona wanasubiri order nini cha kufanya,
Na wenda ndo njia ya kuji tumbua wenyewe maana wamesoma Alama ,kubwa ni kwamba si ndo hawa waliisifia hii Nchi sasa yakiwakuta wanalia .
MUNGU kazini anapitia kila File
 
Hongera mkuu kwa uamuzi sahihi. Kwa aina hii ya uongozi itafanya na wengine watambue kuwa kuna mipaka ya utendaji na ufuataji wa sheria. Nape alikemea na wewe unakemea na wengine watafuata. Najua utakuwa na simanzi kuona mpiganaji mwenzio ameondolewa kizandiki.Nakumbuka niliona ukifanya kampeni katika kijiji ambacho mtu wa kawaida asingefikiria kama unaweza kwenda, na nadhani Nape alifanya kama hivyo.Kazi njema ila jitahidi kudhibiti matumizi yaliyopitiliza na ya nguvu ya Jeshi letu la Polisi.

cc Mwigulu Nchemba
 
Mambo.. Bashite hakamatiki, ni kama ana mamlaka kama ya Rais, ukimgusa Bashite au maslahi yake umemgusa Faru John, yaan Faru John yuko ndani ya Bashite na Bashite yu ndani yake.

Yaan ni ngumu sana kuwatenganisha hawa wasukuma wawili. Tushaambiwa tulie tugaregare hamna kitakachobadilika. Bashite hata akimuua mtu leo, kelele zitapigwa sana tu ila ataambiwa aendelee na kazi na watu wachape kazi waache kupoteza mda.

Tanzania bado sana.
Kweli bashite naye kawa Raisi kivuli analindwa ka mboni ya jicho. Awamu twafaaa ni mwendo wa kutumia minguvu tu ukiwa mbishi unapotezwa ka Ben Saanane.
 
Mhemishiwa Mwigulu umejipanga lakini? Inaonyesha amri ilitoka kwa RC kumzuia Nape asiongee, siku hizi liko wazi akinena RC wa Dar kanena mkuu wa magogoni.
 
Mafuriko.jpg


BAO LA MKONO, MATOKEO YAKE NI HAYA.​
 
Back
Top Bottom