Tarakilishi
JF-Expert Member
- May 19, 2013
- 2,181
- 2,446
Umenena yaliyo ya haki, Yeye kama Waziri anapaswa kwenda mbali zaidi hayo maagizo aliyoyatoa. Haiwezekani mtu unaulizwa kitambulisho unatoa bastola unarudi nyuma kulenga shabaha!! Hili limetuhuzunisha wengi maana kama Nape ambaye karibu kila mtanzania anamfahamu anatendewe vile, je wananchi wa kawaida wana hali gani kutoka kwa vyombo hivi vya usalama?? Kimsingi, Yule mtu anatakiwa kupekekwa mahakamani kwa kutishia kuua. Najiuliza, hivi tangu lini bastola ikawa ni kitambulisho cha askari au mwana usalama??? Kwa nijuavyo mimi hata majambazi wana bastola, sasa sijui Yule bwana tumuweke kundi lipi kati ya ujambazi na uaskari!!?Nchemba hapo kama unajiosha tu.
Isiishie kwa kuwaagiza polisi, inatakiwa uwape masaa wakuletee ripoti, huyo ni nani na kwanini alifanya vile na kama ni askari nani alimpa amri ile, chain of command iliyofanya yale ijulikane, tuone hiyo chain ya command kama ilianzia tokea kwako au ilianzia kati kati.
Bila kufanya hivyo basi wewe ni Waziri husika wa usalama wetu na inabidi ufanye wajibu wako ili tuelewe kuwa na wewe huhusiki kwa Nape kuwa harassed namna ile.
Nnawaza tu, ikiwa mtu kama Nape anafanyiwa vile, sisi wenzangu na mie si tupo mashakani.
Mbwa wa polisi hakamati mtu bila ya kupewa amri, hali kadhalika kwa polisi mwenyewe kama ni polisi.
Tunataka mizizi ya huo ujinga ing'oke.
You can do much better than that kama hautaki nafsi yako ikusute. Otherwise utakuwa ni mnafik tu.
Kwa ujumla ni tukio lililoleta udhia kwa watu wengi, na tumejeruhiwa nyoyo zetu