Mtumishiwetu

Senior Member
Jul 13, 2022
187
334
Tangu Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kuzungumzia suala Tozo la miamala naona kampeni kubwa inafanyika ndani ya CCM kutaka kumfukuza uwaziri Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kile kinachoonekana kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.

Kwanini iwe Mwigulu Nchemba peke yake, Je ni kweli katika Serikali hii ni Waziri Mwigulu pekee aliyefanya mambo mabaya na kusababisha wananchi kupata shida? Kwanini wengine hawatajwi kuna nini?

Kwanini Januari Makamba hatajwi?
Kwanini Hussein Bashe hatajwi?
Kwanini Nape Nnauye hatajwi?

Auhao Wizara wanaziziongoza hazijawakosea watanzania?
 

Attachments

  • 287203992_5118088714936890_1078514186751471247_n.jpg
    287203992_5118088714936890_1078514186751471247_n.jpg
    130.3 KB · Views: 5
Impact kubwa kwa watanzania inayotokana na incompetence ya hawa watu ni (wizara ya fedha na Nishati) kwahio binafsi naona wote hawafai..., ila mbaya zaidi ni kauli za huyu Bwana kana kwamba anachofanya kipo sahihi na ataendelea kukifanya (hence bora aondoke kabla huu mchicha haujageuka kuwa mbuyu)
 
Wote hao kila mmoja kwa wakati wake walitukashifu sisi wananchi.

Hatutasahau kamwe namna tulivyowapa hayo madaraka ili waje kutudhalisha.
 
Serikali yote ni wizi tuu. Chanzo cha upotevu wa mapato ni matumizi mabaya ya serikali. We mkurugenzi au katibu wizara anatembelea miradi kwa kutumia ndege kuhama mikoa huku gari zinapita chini kumfata na kumpokea.

Jambo dogo la uzinduzi kuna timu ya watu zaidi 20 posho, gari kuanda tukio na unakuta mradi wa billion 1

Kwa nini tusione tozo ni wizi
 
Tangu Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kuzungumzia suala Tozo la miamala naona kampeni kubwa inafanyika ndani ya CCM kutaka kumfukuza uwaziri Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kile kinachoonekana kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.

Kwanini iwe Mwigulu Nchemba peke yake, Je ni kweli katika Serikali hii ni Waziri Mwigulu pekee aliyefanya mambo mabaya na kusababisha wananchi kupata shida? Kwanini wengine hawatajwi kuna nini?

Kwanini Januari Makamba hatajwi?
Kwanini Hussein Bashe hatajwi?
Kwanini Nape Nnauye hatajwi?

Auhao Wizara wanaziziongoza hazijawakosea watanzania?
Mwigulu ni kinyesi katika kauli na kiburi na dharau na mdomo wenye matamshi na jeuri ya uumbwa, kila mmoja Abebe mzigo wake, Huyu hasira zetu kwake sio tozo Bali alichonena na hatasamehewa mshamba huyu. Labda aombe radhi
 
Baadhi ya viongozi wetu wana lugha chafu na za kuudhi. Hawa ni wa kupigia kelele hadi kieleweke. Jamaa kasema twende Burundi, mwingine kasema tutakula nyasi na KIBOKO ni yule aliye waambia jamaa wapige mbiki etc.
 
Tunapolalamika kuwa Tozo zinabana na kuumiza unasema "Hamieni Burundi kweli..." UTU uko wapi?
 
Taasisi ya urais imechafuka sana Kwa wananchi, mwigu lazima atolewe kafara kuisafisha.

By the way nani alimwambia aje na msururu mkubwa bungeni kama kiongozi mkuu??

Nani alishauri kununua V8 ktkt ya maumivu ya tozo?

Nan alimpa kiburi kurudia mara mbili kuwambia watz kuhamia Burundi???
 
Labda kama hua husomi humu, Mawaziri wote hutajwa humu, wengine kwa mabaya wengine kwa mazuri, lakini Mwigulu kwa kauli yake ya "HAMIENI BURUNDI IMEWAUDHI SANA WATANZANIA"
Jamaa ana roho mbaya sana, hivi alishindwa hata kusema tuende Denmark, Norway, Canada n.k.

Mtu akikuchukia hataki hata kuona unapata raha....hata kukutajia sehemu yenye neema anahofu isije ikatokea kweli.
 
Back
Top Bottom