Waziri wa Malawi kasema haya...!

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
Serikali ya Malawi imepuuza tishio la Tanzania kuhusu mzozo wa mpaka kwenye ziwa Nyasa na kusisitiza kwamba ziwa lote ni la Malawi hivyo utafiti wa Mafuta utaendelea.

Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa Malawi Uladi Musa amekaririwa akiongea na radio moja na kusema watanzania hawana mamlaka ya kuzuia utafiti wa mafuta uliokua ukifanywa kwenye ziwa hilo, na kama shinikizo litaendelea watawasilisha hiyo ishu kwenye mahakama ya kimataifa

Gazeti la habari leo limeandika kwamba waziri huyo amesema serikali ya Malawi ina ushahidi kabisa kuthibitisha kwamba ziwa nyasa ni lao na kuna mikataba inayoonyesha, hivyo hoja ya Tanzania haina mantiki.
 
mimi nasema hivii waje tuu wafanye huo utafiti wa mafuta tuatawapiga na kuwasambaratisha watafiti wote wa hayo mafuta!
 
Who is that big Chimp behind this little monkey??

Au wanajua tumeishiwa budget ya Vita na mabomu yote yametulipukia wenyewe?

hivi Shimbo kanunua mabomu mapya !? maana yale mengine walisema yame-expire, au kajiungezea matrilion ? daaah isije ikawa tuna mabomu ya kichina ndo maana madogo wanatuchokoza !
 
Tutaipiga Malawi kwa mkwara kutumia picha za Uganda mwaka 1978-79 hakuna cha ziada mkwara unatosha sana kuwakimbiza wale wa nyasa ...sisi mabingwa wa propaganda na bla bla tutawashinda tu
 
Hawaijui TZ wale wanyasa:
Sisi tumepigana, usheli sheli mara kadhaa na tukamweka Albert Reneè
Tumepigana Angola, Namibia, Msumbiji, Zimbabwe, Comoro, Uganda tukaiteka yote na kuidhibiti, kufundisha na kuwasaidia Polisario(Sahara Magharibi) kuwafundisha na kuwasaidia 'Umkhonto we Sizwe' kuwafundisha na kuwasaidia Congo ya Kabila.
hivi wanaijua hii CV ?
 
wanataka tuichukue malawi kwenye imaya yetu kijanja mana wao wenyewe imewashinda!
 
Tusiombe vita wakuu. I know there are big nation (s) behind this!!! Wanataka kuwekeza pale kwe mafuta na inasemekana yapo mengi!! watalipia vita at any cost!! Tutaisha maana kina Vasco Da Gama watapanda ndege watatuacha tukifa, Liwalo na Liwe.
 
Tusiombe vita wakuu. I know there are big nation (s) behind this!!! Wanataka kuwekeza pale kwe mafuta na inasemekana yapo mengi!! watalipia vita at any cost!! Tutaisha maana kina Vasco Da Gama watapanda ndege watatuacha tukifa, Liwalo na Liwe.

Labda waje wao, mbona Afghanistan wanachemsha huko na wanapigana na wavaa vikoi na kanzu !
 
haka kaNCHI kasitusumbue ni sawa na kelele za mlango mbovu hazimsumbui mwenye nyumba kulala, pale kn kuna askari mgambo wanaweza tangulia, maana ni wa akiba wakifuatiwa na Sungusungu.
Hii kitu lazima tuwashtue kuwa sisi ni wababe na hatuna ugomvi nao ila haki itendeke kwani Raia wetu walioko hapo Ziwani waende wapi?
 
Huyo Waziri ana "test". Apeleke videge vyao kule aone, tunakwenda kwanza kwa Mheshimiwa Zitto atuazimie radi kule kwa wataalam wa kijijini kwao. Halafu ndio watajuwa kuwa hatuchezewi.
 
Last edited by a moderator:
Gazeti gani? Acha uchochezi wewe! Kama gazeti moja limesema hivyo; gazeti mbili limekataa
 
Back
Top Bottom