BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Sisi Wananchi wa Mtaa wa Agape, Kata ya Muriet Mkoani Arusha tuna changamoto ya kukosa maji kwa muda wa miezi miwili sasa.
Licha ya kufanya jitihada za kuwasiliana na mamlaka ya Maji (AUWSA) hatujapata majibu ya kueleweka, hali hiyo imekuwa ikisababisha kero kubwa kwa wakazi wengi wa Agape.
Kuna Injinia wa AUWSA ambaye tulimtafuta akasema kuwa kuna mradi unaendelea unasimamiwa na Wachina lakini hakuna maelezo ya kueleweka.
Tukienda ofisi za AUWSA napo hakuna majibu ya maana tunayoyapata, tunaomba mamlaka za juu ai ikiwemo Waziri wa Maji, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya watusaidie kwa kuwa Muriet tupo Mjini kabisa Arusha kukosa huduma ya maji sio haki na sio salama kwa afya