Waziri wa Kilimo, mifugo na Uvuvi tatua matatizo ya wastaafu waliokua Mashirika ya Utafiti TARO na T

Ukiwa

Member
Jul 12, 2016
61
28
Mashirika haya mawili yaliundwa kwa mujibu wa sheria mnamo tarehe 01/07/1982 kwa nia ya kuongeza ufanisi kwa kuwahamisha wafanyakazi wa kitengo cha utafiti wa iliyokuwa Wizara ya Kilimo na Mifugo wakati huo na kuwapeleka kwenye mashirika hayo mawili.Hata hivyo mnamo tarehe 30/06/1989 ajira za wafanyakazi zilirejeshwa waizarani.

Kwa bahati mbaya wafanyakazi hawa wanapofikia kustaafu wanakatwa kipindi chote cha miaka saba ambayo wamekua wakitumikia haya mashirika inagawaje walifanya kazi kwa uadilifu hadi kustaafu. Pamoja na miongozo iliowekwa na SSRA kuhusu majumuisho ya mafao lakini ukifika PSPF ambao ndio mfuko wa mwisho, na walitakiwa kuwasaidia hawa watu utapigwa danadana mpaka unapata kizunguzungu haswa ikizingatiwa umri umeenda. Kuna baadhi ya wafanya kazi pale (si wote) wanakutafutia visingizio likuki ili tu mradi usilipwe badala ya kukusaidia. Inafikia mahali unajiuliza hivi hizi fedha ni za kampuni binafsi au nia za mfuko ambao unachangiwa na wafanyakazi. Mbona wanakopesha watu fedha hizo bila marejesho kama inavyosemekana kwenye bunge?

Kwa heshima na taadhima Mheshiwa waziri wa Kilimo wewe ndio mwenye dhamana na mashirika haya tunakuomba ulitazame tatizo hili kwa jicho la huruma ili hawa wazee wasiendelee kunyanyaswa. Na tunaomba uwasiliane na waziri mwenzio mwenye dhamana na mifuko ya jamii maana yaelekea kua hii mifuko inafanya kazi kama hamna mamlaka nyingine juu yake ili mtatue tatizo hili ambalo limekua mwiba kwa wanaotarajiwa kustaaafu na ambao wamestaafu halafu hawajalipwa hadi sasa na wameshakata tamaa.
 
waziri wa ccm, may be atoke nje ya nchi

Back
Top Bottom