The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 7,382
- 8,437
Hongera Serikali Kwa kupunguza mzigo wa misumari Kwa walipakodi.
Hata hivyo Bado Kuna Utitiri wa mashirika, taasisi na wakala ambazo hazina maana zaidi ya kuleta usumbufu.
Mfano sijasikia mlipounganisha au kufuta kina Sido,Temdo,Tirdo,TanTrade,Mbrela na mizigo mingine kama hiyo..
Hayo 20 yawe ya kuanzia tuu ,Kuna mengi ya kufutwa na kuunganishwa maana yamekuwa mzigo sana Kwa walipakodi na hayana Tija
======
Pia soma Kongole kwa Serikali kwa kuondoa muingiliano wa kazi za TFDA na TBS, ikiwapendeza sasa muitazame RITA na NIDA
Serikali ya Tanzania imetangaza kufuta, kuunganisha na kuvunja mashika na taasisi za umma 20, ili kuongeza ufanisi wa utendaji na tija serikalini.
Uamuzi huo umetangazwa jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa Desemba 15, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alipozungumza na waandishi wa habari.
Ameyataja mashirika yanayounganishwa ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na Wakala wa Udhamini, Utambuzi na Ufilisi (Rita).
Mengine yanayounganishwa ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo.
Profesa Kitila amesema Bodi ya Chai itaunganishwa na Wakala wa Wakulima wa Chai, huku Bodi ya Nyama ikiunganishwa na Bodi ya Maziwa.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), amesema kitaunganishwa na Mamlaka ya Maeneo ya Uchakataji Mauzo ya Nje (EPZA), kadhalika taasisi za utafiti za Chai, Tumbaku na Kahawa zinaunganishwa kuwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari).
Hata hivyo, ameyataja mashirika yatakayovunjwa ni Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPSCF), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Bodi ya Pareto na Shirika la Elimu Kibaha.