Nimekuwa nikifuatilia utendaji wa TCU na hasa baada ya Magufuli (RIP) kuwapokonya kazi ya kudahili wanafunzi waliyojipachika. Kwa ufupi hapo Magufuli alishauriwa vizuri maana walishaanza kufanya biashara na vyuo vikuu na hasa vyuo binafsi (private).
Sasa yaonekana hawana mwongozo wa kazi zao za kila siku ukiacha ile ya kufungia vyuo binafsi wakati vya serikali viko hoi kwa miundombinu. Wameanza kazi ya kubadilisha muelekeo wa mitaala ya vyuo vikuu bila kuelewa wanachokifanya jambo ambalo linaleta usumbufu bila manufaa. Nitaeleza.
Kuna mkumbo wa kujidai vyuo vikuu vyote vifuate mitaala, wanaita ni competence based badala ya mpangilio uliovianzisha, yaani knowledge based. Uelekeo huu naomba niuite ni wa "Kijinga" kwa sababu hakuna nchi duniani iliyo na vyuo vikuu vyote ambavyo ni competence based.
Kila nchi ina mchanganyiko wa vyuo. Tanzania tayari tuna mchanganyiko huo. Wahitimu wa digrii ambazo ni competence based wako chini ya NACTE. Vyuo chini ya TCU vilistahili kubaki kwenye mfumo wa knowledge based na ndivyo nchi zote zinavyofanya. TCU sasa wanajidai ni wataalamu sana, wanaleta usumbufu kwa vyuo na kwa hili, nafahamu wazi vyuo binafsi vitasumbuliwa sana bila sababu.
Tuwaombe TCU wajifunze mifumo ya dunia kabla ya kutuharibia mfumo wetu wa elimu kwa uelewa wao mdogo. Kama wamepewa pesa na hawajui nini wakifanye, ni bora wakaziachia ziingie kuwasaidia vijana wanaotafuta ada za vyuo.