Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Waziri wa afya Mh. Ummy muda huu anazungumza na viongozi mbalimbali wa dini juu ya mikakati ya kudhibiti Corona.

--
ALIYOZUNGUMZA WAZIRI UMMY MWALIMU (KWA UFUPI)

Viongozi wa dini mnayo nafasi ya kipekee kutoa taarifa sahihi, kwa weledi na uwazi, hivyo kupunguza uwepo wa taarifa zisizo za kweli zinazoweza kupelekea hofu, unyanyapaa na mashaka miongoni mwa wananchi.

Tunaomba pia ibada ifanyike muda mfupi, pia wekeni utaratibu wa kupunguza msongamano wa waumini wakati wa kuingia na kutoka katika nyumba za ibada.

Nimpongeza mkuu wa mkoa wa Pwani (Everist Ndikilo) kwa kuzuia kongamano la dini lililopangwa kufanywa na madhehebu ya kidini na kuhusishwa watu 3,000 wanaotoka nchi nzima.

Ugonjwa tumeletewa kutoka nje, hivi sasa takwimu za jana, juzi na wiki iliyopita tumeanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe. Ili viongozi wangu wa dini naomba niliweke wazi its no longer imported cases, tumeanza local transmission.

Ndani ya siku chache tutaingia katika community transmission. Maana yake tutapata mgonjwa ambaye hajui ugonjwa ameupata wapi? Sasa hivi amekuja mtu anamuambikiza fulani ndio maana tunafanya contact (muingiliano) kujua.

Lazima niwaambia ukweli nisiwafiche soon (karibuni), tutaingia kwenye community transmission. Bado tunatakiwa kuchukua tahadhari na kuongeza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu

Rais amesema hatuwezi kufunga kazi, kazi lazima tufanye lakini tuweze kudumisha kutokaribiana baina yetu. Hata Baba Askofu unaweza kufanya 'Video Conference' ukiwa na jambo na waumini

Tafiti zinaonesha virusi vya corona pia vinaambukizwa kwa njia ya hewa hivyo baada siku chache Serikali itatoa mwongozo ikiwa ni pamoja na kumtaka kila mtu anapotoka nyumbani awe amevaa barakoa ili kupunguza kasi ya mambukizi.

Mwanzoni kulikuwa na hisia kwamba Afrika hatuwezi kuumwa ugonjwa huu lakini leo kwa mujibu wa takwimu za Africa CDC, tuna wagonjwa takribani 10,000 na vifo vimefikia takribani 500

WHO ilitukadiria kufikia katikati ya Aprili tutakuwa na wagojwa 1000 nchini na katikati ya Mei tutakuwa na wagonjwa 10,000, kufikia sasa tumeruka kiunzi hicho kwa sababu hatuna wagonjwa wengi tunapaswa kumshukuru Mungu

Tunashauri wananchi tujiulize, je ni lazima tusafiri kutoka mijini kwenda vijijini wakati huu wa maambukizi ya corona? Tutafakari tusije tukawapelekea wazee wetu, wazazi wetu, na walezi wetu hivi virusi vya corona.
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiongea na viongozi wa dini, amesema kuwa kwa sasa hali ya ugonjwa wa Korona nchini imebadirika kutoka kuletewa ugonjwa na watu kutoka nje imegeuka kuwa hali ya kuambukizana sisi wenyewe kwa wenyewe.

Wakati huo Waziri Ummy ameonya kuwa ndani ya muda mfupi ujao maambukizi yatageuka kuwa maambukizi ya jumuia(Community Transmission), akawataka watanzania wajiandae kwa hali hiyo.

MY TAKE:
Tuliwaambia mapema kabisa, Fungeni hii mipaka ya nchi mtatuletea janga, lakini tukaendelea kujivutavuta sasa tunakwenda kwenye hali ngumu sana

Tumeona juzi hapa mtu katoka Dubai tarehe 24 March kashuka Dar, kisha tukasikia kaenda mwanza tarehe 29 March alipopimwa na kukutwa na Korona, huyu mtu ilikuwaje hakuwekwa karantini?

Kwa hiyo ina maana Kwenye Karantini hatukuwa serious na pia kwenye kufunga borders hatukuwa serious, sasa matokeo yake huenda tukaingia kwenye hali ngumu

Kiufupi serikali haiwezi kukwepa lawama hali ikigeuka na kuwa mbaya nchini.

Saa hivi hao wachina tuliokuwa tukiwapokea kwa bashasha pale KIA kipindi wapo kwenye hali ngumu sasa hivi wamefuta residence permit na viza za foreigners walio nje ya mipaka ya nchi yao na wanawasumbuasumbua foreigners walio nchini mwao kwa sasa kwa kuwabagua na kuwafanyia kila aina ya ubaguzi kuwa eti ndo wanawapelekea New cases, Wanawanyima hoteli, kuingia kwenye supermarkets,Weusi wakipanda mabasi wachina wanashuka. Sasa najiuliza Je sisi wema wetu wa kufungua mipaka kipindi kile umetuletea nini zaidi ya kuhatarisha maisha ya watu wetu?

Msikilize Ummy Mwalimu hapa akiongea
 
Waziri wa afya mh Ummy muda huu anazungumza na viongozi mbalimbali wa dini juu ya mikakati ya kudhibiti Corona.

Kwa sasa anaongea Shehe wa mkoa wa Dsm slhad Mussa Salumu ambaye anawalaumu baadhi ya viongozi wenzake wa dini wanaoshindwa kutekeleza maagizo ya wizara.
Kwakweli hii hali inakera sana tusije tukaelekea katika hali ya South Africa !Na jirani yetu Kenya
 
Back
Top Bottom