Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu
na David Frank, Loliondo
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Watoto Sophia Simba, ameonja joto ya jiwe baada ya kuzuiwa na wananchi kumfikia Mchungaji Ambilikile Maisapila, kwa madai kuwa alichakachua foleni kumfikia.
Waziri Simba alifika katika kijiji cha Samunge majira ya alasiri (Alhamisi iliyopita), akiwa katika msafara wa magari manne na kutaka kwenda moja kwa moja kumwona Babu eneo alilokuwa akitolea tiba hiyo.
Ghafla waziri huyo alivamiwa na kundi la watu wenye hasira ambao wengi wao walikuwa wamekaa kijijini hapo kwa zaidi ya siku saba, wakisota kumwona Babu.
Mashuhuda wa tukio hilo la aina yake, waliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa Waziri Simba alizuiliwa kwani alitaka kumwona Babu muda mfupi tu baada ya kuwasili kijijini hapo bila kufuata foleni.
Watu hawakujali uwaziri wake, walimzonga na kumhoji imekuwaje amefika na kukimbilia kikombe bila kupanga foleni kama wanavyofanya wao. Uliibuka mzozo mkubwa kati yake na wananchi hao ambao baadhi walikuwa wakisema hovyo kwa hasira, alisema shuhuda wetu.
Wakati tafrani hiyo ikitokea, wasaidizi wa Babu pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji cha Samunge, walikimbia kwa hofu ya kupewa maneno makali na wananchi, hali iliyomlazimu Babu kusitisha tiba yake kwa muda kutuliza hali hiyo.
Wakati akituliza hali hiyo, Babu akiwatahadharisha wananchi waliofurika kijijini kwake kwamba wanapaswa kuwaheshimu viongozi wanaofika hapo kwani mbali ya kupata kikombe, pia wanaratibu shughuli zinazohusiana na tiba hiyo ya ajabu.
Nawaomba muwaheshimu viongozi wanaokuja hapa kwani mbali ya kuja kupata tiba wanafika kuona namna ya kuboresha hali ya mazingira ili tiba hii iweze kuwa endelevu, alikaririwa Babu akisema.
Babu alimwongoza Waziri Simba kwenda kumpa kikombe pamoja na ujumbe wake na baada ya kupata tiba hiyo, waliondoka kurudi Arusha.
Katika hatua nyingine siku chache tu baada ya Babu kusitisha huduma kwa watu na wagonjwa wanaotoka ndani na nje ya nchi, kumeibuka staili mpya ya magari kusafiri na kupeleka watu kwenda kijijiini Samunge kupitia njia za panya.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mbali na barabara zilizowekewa vizuzi, yapo magari yanayotumia barabara ya Longido kupitia Ziwa Natron na kuingia moja kwa moja kijijini Samunge.
Pamoja na kuwepo vizuizi maalumu kama vile vya Arusha, Mto wa Mbu, Babati mkoani Manyara, Mugumu na Musoma mjini mkoani Mara, bado madereva watukutu wanafanya hila na kusafirisha watu na wagonjwa hao kupitia Longido na kuchepukia Ziwa Natron na kuunganisha moja kwa moja kwa Babu, alisema mmoja wa viongozi wa wilaya ya Ngorongoro.
Wakati hayo yakiendelea, magari zaidi ya 300 yamezuiliwa katika kizuizi cha Mto wa Mbu, huku zaidi ya magari 100 yakiwa yamekwama eneo la Melerani wilayani Monduli, yakiwa njiani kwenda Loliondo.
Kuzuiliwa kwa magari hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya mchungaji huyo ambapo aliomba wagonjwa wapya kusitisha kuingia Loliondo katika kipindi cha wiki moja.
Chanzo: Tanzania Daima.
My Take:
Wadau -- hii anavyofanya Babu ni sahihi -- kuwatetemekea wakuu wa siasa na serikali kwa visingizio ya kuboresha mazingira? ya sehemu hiyo
Sasa kila kiongozi wa serikali ataruka foleni kwa kisingizio hicho -- hiyo dawa itawaponyesha?