Waziri Ngeleja: Serikali imeridhia kuilipa DOWANS Bilioni 95

Nimechoka kudanganywa na kila siku sielewi,sasa tabu ilikuwa ipi kuwataja tokea mwanzo???hadi Dr aseme fulani ndo anahusika ndo watuambie???What is wrong with our leaders,do they need that much pressure kuwapa wananchi majibu kwa maswali yao??
 
ukitaka kuamini rostam anaongoza nchi angalia draft lilivyo chezwa kaanza rostam kuropoka kisha kafuatia mfanyakazi wake ngeleja. mipango hiyo..
 
NGELEJA = VODACOM = ROSTAM'S LIL BYAAAATCH!..... Asitake kufanya watanzania majuha. N'gombe.
 
Kitendawili kimeteguliwa kwa waziri Ngeleja kuwataja wamiliki wa Dowans na Wakurugenzi wa Dowans. Mbona jina la Rostam Aziz halipo katika wamiliki na hata wakurugenzi?

Ukweli umedhihiri, je uzushi utakwisha??
Unaamin kwa kufanya ivyo Ngeleja katuliza hasira ya watanzania?
 
Hivi Sheria za nchi na kimataifa zinasemaje kuhusu mtu binafsi kuamua kufungua mashitaka kupinga jambo fulani linalohusu maslai ya nchi yake?katika hili nazungumzia kupinga malipo hewa yanayotaka kufanywa kwa Dowans? Nasema hivi kwani naamini kati yetu kuna wenye ushahidi wa kulitetea taifa hili. kwa mfano Bubu Ataka kusema na ushahidi alionao. Zipi ni faida na hasara za kufanya au kutokufanya hivyo kama sheria inaruhusu?
 
Yaani wewe unaamini serikali inayoundwa na wahujumu uchumi??
Ulitegemea wamtaje Rostam halafu iweje?
 
Kitendawili kimeteguliwa kwa waziri Ngeleja kuwataja wamiliki wa Dowans na Wakurugenzi wa Dowans. Mbona jina la Rostam Aziz halipo katika wamiliki na hata wakurugenzi?

Ukweli umedhihiri, je uzushi utakwisha??

kwenda zako.
 
Kitendawili kimeteguliwa kwa waziri Ngeleja kuwataja wamiliki wa Dowans na Wakurugenzi wa Dowans. Mbona jina la Rostam Aziz halipo katika wamiliki na hata wakurugenzi?

Ukweli umedhihiri, je uzushi utakwisha??

Wewe ndio walewale 'mawazo mgando'. Unaweza kumchukua mtanzania gani umwulize unalohoji asijue jibu lake?

Wewe serikali ilishawahi kukupa jibu lenye mwanga pale maswali muhimu yanayotafutiwa majibu yenyewe inahusika?

Usiwe kipofu mno maana hata kipofu siku akifumbuliwa macho akikuta dunia yote imepakwa rangi ya nyekundu, hata ukimwambia awali ilikuwa tofauti mtauna kuliko akubali.

Nawe yaelekea upo ktk leve iyo hiyo. Pole sana. Saa na mda wa kudanganya umma ulishatoweka. Labda ubakie mwenyewe ulipo.
 
Sina la kuongeza, nimeingia nchini nina wiki mbili tu, niko full hapa
 
Kitendawili kimeteguliwa kwa waziri Ngeleja kuwataja wamiliki wa Dowans na Wakurugenzi wa Dowans. Mbona jina la Rostam Aziz halipo katika wamiliki na hata wakurugenzi?

Ukweli umedhihiri, je uzushi utakwisha??

Jee, wewe una ushahidi kuwa Rostam ni mmoja katika wamiliki? Kama unao si uweke hapa, ya nini blah blah blah, siku zote mlikuwa mnataka kujuwa wamiliki, ingawa kuna sehemu za kwenda kisheria kujuwa wamiliki, mlishindwa kufanya hivyo, leo Ngeleja kawarahisishia kazi, sasa kama hamkubaliani nae, prove him wrong.
 
Briefcase Company hiyooo na mabilioni ya Watanzania huku wakitoa kicheko cha kutukejeli :angry:


Serikali yasalimu amri Dowans

• Ngeleja atangaza rasmi kulipa mabilioni ya fidia

na Betty Kangonga

HATIMAYE serikali imetangaza rasmi uamuzi wa kuridhia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuilipa fidia ya shilingi bilioni 94 Kampuni ya Dowans Holdings.


Msimamo huo rasmi wa serikali unaotokana na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICC) ulitangazwa mbele ya waandishi wa habari na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.


Akitangaza uamuzi wake huo, Ngeleja ambaye alisahihisha taarifa za vyombo vya habari kuhusu kiasi halisi kinachopaswa kulipwa badala ya kile cha shilingi bilioni 185 zilizokuwa zikitangazwa awali, alisema wanasubiri kusajiliwa kwa uamuzi huo wa ICC katika Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya utekelezaji wa malipo kufanywa.


Ngeleja alisema uamuzi huo wa kuilipa Dowans umezingatia ushauri wa kisheria uliotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wanasheria wa TANESCO.


Alisema serikali imeamua kutekeleza uamuzi huo wa mahakama hiyo ili kuepuka gharama zaidi za tozo iwapo itashindwa kutekeleza uamuzi wake kwa wakati.


Habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kuwa mara tu baada ya hukumu hiyo kusajiliwa Mahakama Kuu, iwapo serikali itashindwa kulipa itakuwa ikitozwa kiasi cha ziada cha shilingi milioni 25 kila siku.


"Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO ilishauriwa na wanasheria wake wa Kampuni ya Rex Attorneys Advocates pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali tukubaliane na hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo bila kupinga endapo itasajiliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania," alisema.


Alisema kutokana na hukumu hiyo Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC haitalipwa kiasi chochote cha fedha kama ilivyokuwa ikidai fidia ya dola milioni 169 kutokana na kashfa iliyofanywa na TANESCO.


Ngeleja alisema kuwa ni vyema wananchi wakaendelea kuheshimu na kuthamini matumizi ya sheria za nchi na za kimataifa na kuamini kuwa mgogoro wa Dowans na TANESCO ni suala la kisheria na si vinginevyo pamoja na kuwa matokeo hayo yamelitia hasara taifa.


"Wakala wa usajili wa Makampuni na Biashara nchini (Brela) ndio wenye kumbukumbu za makampuni yote yaliyosajiliwa, hivyo suala la kujua wamiliki au wakurugenzi wa kampuni si hisia wala kuzusha, ni jambo linaloweza kuthibitishwa na wakala huo," alisema.


Ngeleja alitumia mkutano huo kuwataja wamiliki wa Dowans baada ya kupata taarifa kutoka Brela kwa barua yenye kumb. namba MITM/RC/58550/22 ya Januari 5, mwaka huu ambao ni Dowans Holdings S.A, yenye hisa 81 ya Costa Rica na Portek System and Equipment PTE Limited hisa 54 ya Singapore.


Alisema wakurugenzi wa Dowans wa hapa nchini ni Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenyan).


Wakati Ngeleja akitaja majina hayo, wiki moja iliyopita Tanzania Daima ilikwisha kuwataja wanaomiliki kampuni hiyo.


Alisema hakuna sheria inayowataka wawekezaji wakitaka kuanzisha kampuni nchini ni lazima awepo mbia wa ndani, wanaweza kuanzisha wenyewe ikiwa wamefuata taratibu na sheria za nchi.


Alisisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ulipwaji fidia wa sh bilioni 94 kwa Dowans na TANESCO kupandisha bei za umeme kama ilivyoamriwa na Ewura.


"Ni upotoshaji mkubwa kuhusisha mambo mawili tofauti... migogoro ya Richmond na Dowans ilipelekwa ICC mwaka 2008, sasa kwanini watu wanaunganisha haya? Labda hii inatokana na watu kupenda kuchakachua maneno," alisema.


Alisema kuwa kuna bidhaa mbalimbali zimekuwa zikiongezeka bei lakini wanashangazwa na hatua ya Ewura kupandisha gharama hiyo kwa asilimia 18.5 na kusababisha baadhi ya makundi kutaka kuandamana wakati ongezeko la bei ya umeme ni suala la kiuchumi na kibiashara kwa shirika hilo.


Alisema wananchi hawana budi kuhakikisha wanasonga mbele na si kuangalia nani aliyeliingizia taifa hasara ili achukuliwe hatua, bali ni kujua hiyo ni sheria na itabaki kuwa historia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando, alisema kuwa mgawo wa umeme bado utaendelea katika maeneo mbalimbali kutokana na kupungua kwa gesi inayosababisha kuwa na upungufu wa megawatts 50 katika grid ya taifa.

Alisema serikali hadi sasa inadaiwa deni la umeme kiasi cha sh bilioni 70, ambapo Waziri Ngeleja aliahidi kufuatilia madeni hayo na kuyakata moja kwa moja kutoka Hazina ili kuyapunguza.
 
We Kaumza kama huyo **** ni baba yako endelea kumtetete lakini nilifisadi la kwanza... limemaliza mali za nchi hii sasa bado wewe lazima akunyonye ubongo

Mambo ya kusikiliza sana hisia za watu wenye chuki ya rangi na dini ndio yanakufikisha kuwa na Jazba namna hii, leo kuna matajiri wengi sana hata kupita huyo Rostam, ambae ni mfanya biashara halali na mwanasiasa mzuri sana , kama unabisha tazama nyanja za biashara na tazama kule jimboni kwake, leo wewe unasikiliza maneno ya wabaguzi wachache ambao kila ukiwaambia walete ushahidi wa madudu ya Rostam wanashindwa kuleta.

Tatizo letu waTanzania ni kufata mkumbo ndio maana jana watu wakafa kwa sababu tu, wanafata mkumbo.

Hivi nakuuliza, hujawahi kusikia dhambi za huyu kijana wenu Mbowe? Jee hujui kama baba yake alikuwa katika Serikali? Jee hiyo mali ya utajiri wa kupindukia aliichumaje? mfanya kazi wa serikalini leo ghafla awe bilionea? Hujiulizi ilikuwaje?

Sasa tazama cha kustaajabisha, unamshutumu Rostam ambae vizazi vyake vyote ni wafanya Biashara, ana asili ya mali toka alikozaliwa. On the other hand, hakuna asili ya mali kwa kina Mbowe, ni mfanya kazi wa Serikalini. Hiyo mali aliyorithi huyu mbowe Jr. ilitoka wapi? Naomba usiwe biased na ujibu kiuungwana.
 
we acha undundu huo. Jk mwenyewe kadanganywa mara kibao. Nchi hii uliwah kuambiwa kipi cha ukweli.?a/c ngapi zinafunguliwa skukuu?
 
yaan mwenyewe kakiri kushawish dowans waje kuwekeza tz. Means bila kuwashawishi tusingewajua na wala tucngeuvaa mkenge.
 
Briefcase Company hiyooo na mabilioni ya Watanzania huku wakitoa kicheko cha kutukejeli :angry:

Ebu nijibu post yangu hapo juu mkuu.kwani nafikiri kuna nafasi ya kufanya kitu kuliko kulalamika

Ni kweli ukifuatilia details za case hii tangu Richmond na sasa Dowans ni utapeli mtupu lakini mafisadi ndiyo wameshaamua kulipa tena haraka sana. Yule Valambhia alishinda case miaka mingi iliyopita lakini hadi hii leo Serikali imegoma kumlipa. Wale wastaafu wa EAC hawajalipwa mafao yao ya EAC na Serikali inawazungusha zungusha tu kwa zaidi ya miaka 30 sasa, lakini cha ajabu hii pesa ya Dowans inalipwa haraka sana pamoja na ushahidi chungu nzima wa kuonyesha utapeli mkubwa uliofanywa na kampuni hi(z)i Richmond/Dowans.

Nwaigwe ushahidi huu si wa BAK bali umepatikana kupitia kwa Watanzania mbali mbali ambao walifanya juhudi kubwa katika kupinga malipo ya aina yoyote kwa kampuni hiyo ya kitapeli.

 
Back
Top Bottom