Waziri Ngeleja: Serikali imeridhia kuilipa DOWANS Bilioni 95

Sio dharura kabisa, ufisadi tu umewajaa! Rais ni fisadi, the comedy, mshirikina unategemea nini? Anajijali yeye, familia yake, na kikundi cha watu wachache wanaoishi maisha ya anasa huku wakipora bila huruma rasilimali za nchi na wananchi waliomchagua, inatia hasira!!!!!
 
HUYO Jamaa WA DOWANS WAMKABIDHI HUNDI YAKE NA WAKATI WANAMKADHI TAKUKURU, POLISI,TRA NA DPP WAMSUBIRI NJE HUKU RAIS AKIKAA KWENYE TV KUSUBURI ILE ANATOKA TU KUPOKEA CHEQUE YAKE AMTANGAZE MHUJUMU UCHUMI NA KUMUWEKA KIZUINI HUKU TRA, TAKUKURU, POLISI AND DPP WAKIFUNGUA KESI MBALIMBALI KUANZIA YA KUKWEPA KODI, RUSHWA, KUGUSHI, UVUNJIFU WA AMANI N.K. ALL THESE TO MAKE HIM/THEM UNDERSTAND THAT WHAT THEY DID IS ATROCITY!
 
Hili sakata la serikali kuilipa kampuni feki ya Dowans mabilioni ya pesa nafikiri lingewaza kuepukika kama wataaluma wa sheria, wanauchumi na watu wenye taaluma juu ya mambo ya uwekezaji wangejitokeza na kuungana pamoja kila mmoja kwenye fani yake kupinga serikali kulipa Dowans.

Inakuwa ni aibu kubwa kwa Wanasheria (waserikali au wa kujitolea/Binafsi) kukubali uovu huu utendeke.

Lingekuwa jambo la busara sana kama Vyama vya wanasheria vingejitokeza na kupinga jambo hili ikiwa ni pamoja na kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.

Wajipange na watafute hoja na mapungufu yaliyoko kwenye mkataba feki na pia mapungufu yaliyoko kweny hukumu iliyotolewa, wayatumie mapungufu hayo kupinga ulipaji huo.

Zaidi ya hapo, wafungue kesi mahakamani kuwaishtaki wote waliohusika na maovu hayo na wadai fidia kwa usumbufu na kero amboya watanzania wamepata kutokana na RICHMOND na Dada yake DOWANS.

Wajue wasipojitokeza kuwatetea wananchi katika mambo haya, basi taaluma yao itadharauliwa na wananchi watakosa imani nao na pia nchi nyingine zitaona kuwa Tanzania haina wanasheri na wataalam wengine amba kwa fani yao wangeweza kuinusuri nchi na janga hili.

Wajitokeze ili Mafisadi wajue kuwa nchi hii inawenyewe.
 
Hili sakata la serikali kuilipa kampuni feki ya Dowans mabilioni ya pesa nafikiri lingewaza kuepukika kama wataaluma wa sheria, wanauchumi na watu wenye taaluma juu ya mambo ya uwekezaji wangejitokeza na kuungana pamoja kila mmoja kwenye fani yake kupinga serikali kulipa Dowans.

Inakuwa ni aibu kubwa kwa Wanasheria (waserikali au wa kujitolea/Binafsi) kukubali uovu huu utendeke.

Lingekuwa jambo la busara sana kama Vyama vya wanasheria vingejitokeza na kupinga jambo hili ikiwa ni pamoja na kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.

Wajipange na watafute hoja na mapungufu yaliyoko kwenye mkataba feki na pia mapungufu yaliyoko kweny hukumu iliyotolewa, wayatumie mapungufu hayo kupinga ulipaji huo.

Zaidi ya hapo, wafungue kesi mahakamani kuwaishtaki wote waliohusika na maovu hayo na wadai fidia kwa usumbufu na kero amboya watanzania wamepata kutokana na RICHMOND na Dada yake DOWANS.

Wajue wasipojitokeza kuwatetea wananchi katika mambo haya, basi taaluma yao itadharauliwa na wananchi watakosa imani nao na pia nchi nyingine zitaona kuwa Tanzania haina wanasheri na wataalam wengine amba kwa fani yao wangeweza kuinusuri nchi na janga hili.

Wajitokeze ili Mafisadi wajue kuwa nchi hii inawenyewe.
 
Suala la kuilipa DOWANS linawagusa wananchi wote sio wanasheria pekee.

My friend, instead of wanting to get lawyers to come forward to fix this mess you also can seek a legal advice for the same purpose. We all have a part to play in this saga, how is that??
 
:fish:Waziri amesha sibitisha kuwa wamiliki wa Dowasa ni hao hapo chini kwa mana hiyo basi Dowans si kampuni hewa na wala hakuna sita wala saba au mwakiembe mwenywe uwezo wa kuzuwia malipo kwa kampuni ya Dowans Wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd., ambao ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd. Barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (BRELLA) inawataja wakurugenzi kuwa ni Andrew James Tice - Canada, Guy Picard - Canada, Gopalakrishnan Balachandaran - India, Stanley Munai - Kenya, Hon Sung Woo - Singapore na Sulaiman Al Adawi - Oman.





 
:fish:Waziri amesha sibitisha kuwa wamiliki wa Dowasa ni hao hapo chini kwa mana hiyo basi Dowans si kampuni hewa na wala hakuna sita wala saba au mwakiembe mwenywe uwezo wa kuzuwia malipo kwa kampuni ya Dowans Wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd., ambao ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd. Barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (BRELLA) inawataja wakurugenzi kuwa ni Andrew James Tice - Canada, Guy Picard - Canada, Gopalakrishnan Balachandaran - India, Stanley Munai - Kenya, Hon Sung Woo - Singapore na Sulaiman Al Adawi - Oman.




Hakuna kipya hapo ni changa la macho! Wajinga wanafurahia
 
:fish:Waziri amesha sibitisha kuwa wamiliki wa Dowasa ni hao hapo chini kwa mana hiyo basi Dowans si kampuni hewa na wala hakuna sita wala saba au mwakiembe mwenywe uwezo wa kuzuwia malipo kwa kampuni ya Dowans Wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd., ambao ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd. Barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (BRELLA) inawataja wakurugenzi kuwa ni Andrew James Tice - Canada, Guy Picard - Canada, Gopalakrishnan Balachandaran - India, Stanley Munai - Kenya, Hon Sung Woo - Singapore na Sulaiman Al Adawi - Oman.




Hii sio news tena. Mbona ilishaandikwa kwenye magazeti siku nyingi toka Dr Silaha alipotishia kumlipua JK hapo ndipo wakaziba mashimo. hakuna kitu hapo. Huyo Al ADawi wa Oman hata alishakana siku nyingi kuhusika nao. Wamiliki wako hapa hapa bongo
 
:fish:Waziri amesha sibitisha kuwa wamiliki wa Dowasa ni hao hapo chini kwa mana hiyo basi Dowans si kampuni hewa na wala hakuna sita wala saba au mwakiembe mwenywe uwezo wa kuzuwia malipo kwa kampuni ya Dowans Wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd., ambao ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd. Barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (BRELLA) inawataja wakurugenzi kuwa ni Andrew James Tice - Canada, Guy Picard - Canada, Gopalakrishnan Balachandaran - India, Stanley Munai - Kenya, Hon Sung Woo - Singapore na Sulaiman Al Adawi - Oman.






haya huyo wakala aliyethibitisha wamiliki kutokana na andiko lako ni wakala feki...huyo kwenye red... wakala kama huyu tanzania hayupo labda Afghanistan

crap .....
 
Ngeleja alitumia mkutano huo kuwataja wamiliki wa Dowans baada ya kupata taarifa kutoka Brela kwa barua yenye kumb. namba MITM/RC/58550/22 ya Januari 5, mwaka huu ambao ni Dowans Holdings S.A, yenye hisa 81 ya Costa Rica na Portek System and Equipment PTE Limited hisa 54 ya Singapore.

Alisema wakurugenzi wa Dowans wa hapa nchini ni Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman),Jakaya Kikwete (Tanzania )na Stanley Munai (Kenyan).

 
Kikwete aamsha hasira za wabaya wa Dowans
Send to a friend
Sunday, 06 February 2011 22:30


MBOWE, KAFULILA WAMSHANGAA KUTOFAHAU WAMILIKI WA KAMPUNI HIYO
Boniface Meena naRaymond Kaminyoge
HOTUBA ya Rais Jakaya Kikwete imeibua mjadala mpana baada ya baadhi ya wanasiasa, wasomi na wanaharakati kumpongeza huku wengine wakimkosoa kutokana na kile walichokiita ni kauli yake tata ya kutowafahamu wamiliki wa Dowans na kutaka aitishe kikao cha Baraza la Mawaziri na kutangaza kutoilipa kampuni hiyo tata.

Juzi akizungumza na wana-CCM wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa chama hicho kikongwe Afrika, pamoja na kuelezea mlolongo mrefu kuanzia Richmond aliyoiita "Phantom Company,' Rais Kikwete aliweka bayana, "Sina hisa Dowans, wala wamiliki wake siwajui na hawajawahi kuniita kwasababu hawanihitaji."

Hata hivyo, msimamo huo wa Rais kujivua tuhuma hizo za kuwa mmoja wa wamiliki wa Dowans zilizoelekezwa kwake na Dk Willibrod Slaa, bado haujamnasua baada ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kushangaa kauli hiyo wakati Serikali ya Awamu ya Nne ndiyo iliyoingia mkataba na kampuni hiyo.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, alifafanua kwamba kitendo hicho cha Rais Kikwete ni hadaa kwa wananchi akifikiri wanataka kujua uhusiano wake na wamiliki hao.

"Ni kazi ngumu sana kulinda uongo, Rais anasahau kwa jinsi gani Richmond na Dowans zilivyoisumbua Serikali yake hivyo kama anasema hajui basi hafai kuwa Rais wa nchi,"aliweka bayana Mbowe.

Mbowe alisisitiza kwamba, Rais wa nchi si mtu anayepaswa kulalamika bali ni mtu wa kuchukua hatua.

"Ni aibu kwake kunung'unika badala ya kuchukua hatua, ni lazima ajue anapozungumza kwenye vikao vya CCM ajue bado ni Rais wa nchi,"alisema Mbowe.

Kuhusu onyo la Rais kuhusu wanaochochea migomo na maandamano kwa kudai kile alichokiita madaraka waliyokosa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Mbowe alisema mkuu huyo wa nchi aache madai hayo akimtaka atambue kila mtu ana haki ya kudai kile anachoona ni haki yake.

Mwenyekiti huyo wa Chadema aliongeza kwamba, kuandamana ni haki ya watu hivyo kama Rais hataki kuwepo kwa maandamano afute haki hiyo ili wananchi wajue haipo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCID), Deus Kibamba alisema kauli aliyoitoa Rais Kikwete juzi ilikuwa ni maoni yake binafsi.

“Tunataka Rais Kikwete aitishe kikao cha Baraza la Mawaziri, ili kitoe msimamo mmoja wa Serikali wa kukataa kuilipa kampuni ya Dowans,” alisema.

Alisema kauli ya Rais kwamba, ni mmoja kati ya watu wanaotaka Tanesco isiilipe kampuni ya Dowans, ilikuwa ni maoni yake binafsi.

“Tunataka msimamo wa Serikali, tunataka uamuzi wa Baraza la Mawaziri, mawaziri wamepingana kuhusu Dowans kwa sababu hakuna kikao kilichowahi kufanyika,”alirejea kauli na msimamo huo uliowahi kutolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Kibamba alifafanua kwamba, baada ya kikao hicho, ndipo mawaziri na wanasheria wanatakiwa kuweka mikakati ya namna wanavyoweza kuinusuru nchi na ulipaji wa fidia hiyo.

Tayari kauli ya Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa na kusimamia Serikali kuwaadhibu waliohusika Richmond na kisha kuvunja mkataba wa Dowans, inapingana na msimamo wa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliyetangaza kwamba, Serikali lazima iilipe kampuni ya Dowans fidia ya Sh 94 milioni.

Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG) Frederick Werema, naye aliangukia katika kundi hilo la Ngeleja akisema deni hilo halikwepeki kauli ambayo ilipingwa si tu na Sitta, bali pia Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe huku wanaharakati kwa upande wao wakifungua kesi Mahakama Kuu kutaka shauri hili litolewe uamuzi nchini na kuanisha hoja 16 za kwanini kampuni hiyo isilipwe.

Kafulila adai JK hawajui Dowans, Ngeleja anawajua

Kwa upande wa mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, David Kafulila, alimshangaa Rais Kikwete kusema hawajui wamiliki wa Dowans wakati waziri wake Ngeleja alikwishawataja.

“Ngeleja alikwishawataja wamiliki wa Dowans, inakuwaje Rais anasema hawafahamu..., suala hili linazidi kuwachanganya wananchi, inabidi likajadiliwe bungeni,”alirejea msimamo wa hoja yake anayotarajia kuiwasilisha bungeni kama ikikubaliwa.

Kafulila alifafanua kwamba, suala hilo likijadiliwa bungeni ndipo linaweza kutoa majibu sahihi kwa wananchi.

“Kwa ujumla Rais Kikwete kusema hawajui wamiliki wa Dowans ni kielelezo kuwa wale tuliotangaziwa na Waziri Ngeleja sio wenyewe kwani wangekuwa wamiliki Rais angewajua,” alisema Kafulila na kuongeza:

Je waziri wake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliposema lazima tulipe Dowans hawakumwambia wanamlipa nani?

Alisema katika sakata hili ataendelea kupigana hadi ijulikane nani amefikisha taifa katika hali hii. “Serikali ilipe isilipe ni lazima iwajibike maana hoja ya msingi hapa tumefikishwaje hapa hadi kushindwa kesi,” alihoji Kafulila

Mwanasheria maarufu, Profesa Abdallah Safari alisema Serikali inazidi kuwachanganya wananchi kwa namna vigogo wanavyotofautiana kuhusu suala hilo.

“Rais kuwa upande wa wanaopinga kuilipa kampuni hiyo ni jambo jema, lakini inasikitisha kuona mawaziri wanapingana hadharani, hakuna msimamo wa pamoja, Baraza la Mawaziri likae ili kutoa msimamo wa Serikali.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema ni jambo la busara kutafuta njia mbalimbali za kisheria ili fidia hiyo isilipwe.

“Kuna mambo mawili ya kuangalia tunapojadili suala hili..., ni vizuri tukitafuta njia za kutuokoa kulipa fedha hizi, lakini tukumbuke tukishindwa tutatozwa fedha zaidi ambazo ni asilimia 7.5,”alisema.

Kuanzia siku hukumu ilivyotoka, faini ya Dowans imeongezeka hadi kufikia Sh97 bilioni kutokana na riba ya Sh20milioni kwa siku.


Mkataba wa Dowans na Tanesco ulivunjwa Agosti 31 mwaka juzi, baada ya Bunge kuagiza uvunjwe baada ya kuibuka sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Richmond mwaka 2008, l ililomfanya Edward Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu na Baraza la Mawaziri likavunjwa.
 
[h=2]Dk. Slaa: Kikwete ajiuzulu:ASISITIZA ANAHUSIKA NA DOWANS, AAHIDI KUTOBOA SIRI [/h]
na Janet Josiah




KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, sasa amekuja na hoja mpya ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kutokana na kuhusika moja kwa moja na sakata la Dowans iliyorithi mikoba ya Richmond.
Dk. Slaa ametoa kauli hiyo nzito jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, ikiwa ni siku moja baada ya Ikulu kutoa taarifa ya kejeli na vijembe vya mitaani dhidi yake kuhusu sakata hilo.

Akizungumza kwa utulivu na umakini mkubwa, Dk. Slaa alisema Rais Kikwete alipaswa kujiuzulu kabla ya aliyekuwa Waziri Mkuu na swahiba wake mkubwa, Edward Lowasa, kuchukua hatua hiyo Februari 7, mwaka 2008, mjini Dodoma.

Mawaziri wengine waliojiuzulu kutokana na sakata la Richmond lililozua mjadala mkali nchini ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha ambaye alikuwa waziri wa wizara hiyo kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC).

Akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa juzi na Kurugenzi ya Mawasiliano, Dk. Slaa alisema mkuu huyo wa nchi hawezi kukwepa kuhusishwa na sakata la Dowans, kwani alilijua hata kabla mitambo yake haijaingizwa nchini.

"Nataka niwatoe Watanzania wasiwasi kwamba ingawa kurugenzi ya mawasiliano imetoa taarifa ya kumsafisha Rais Kikwete na kunikashifu mimi kwa lugha ya mtaani, nawaambia alipaswa kujiuzulu kabla na anatakiwa ajiuzulu sasa, kwani anahusika moja kwa moja na uingiaji wa mkataba wa Kampuni ya Richmond na baadaye na Dowans" alisema Dk. Slaa.

Alimtaka Rais Kikwete kutambua kuwa hawezi kukaa kimya kwa kisingizio cha kuhatarisha amani na utulivu wakati wananchi wanaibiwa mabilioni ya fedha na mafisadi wachache kupitia kampuni feki ya Dowans.

Akirejea historia ya vita dhidi ya ufisadi aliyoiasisi bungeni, Dk. Slaa aliwataka wananchi wakumbuke kuwa taifa lilipokumbwa na tatizo la umeme kabla ya mitambo ya Richmond kuingia nchini, Rais Kikwete alikwenda Marekani kwa ziara ya kikazi.

Alisema aliporejea nchini, alizungumza na waandishi wa habari kuhusu tatizo hilo na kuahidi kuwa serikali yake inalifanyia kazi na siku chache baadaye, rafiki yake wa karibu, Rostam Azizi, Mbunge wa Igunga (CCM), naye alikwenda Marekani.

"Rostam aliporejea kutoka Marekani baada ya siku chache tukaanza kusikia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond inatarajiwa kuwasili. Kweli ilitua nchini katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere na shughuli nyingine zilifungwa uwanjani hapo kupisha ushushaji wa mitambo ya Richmond" alisema Dk. Slaa.

Huku akisisitiza kuwa ana ushahidi wa anachokisema, Dk. Slaa alisema hata baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme na kusababisha mawaziri kujiuzulu, serikali ya Kikwete iliamua kuingia mkataba na Dowans iliyorithi shughuli za Richmond na hatua hiyo Rais Kikwete pia aliijua.

"Dowans nayo ikashindwa kuzalisha umeme, mwisho Bunge katika moja ya maazimio yake liliridhia uamuzi wa kuvunja mkataba huo, lakini leo Serikali inadaiwa fidia ya sh bilioni 185, je, Rais Kikwete anaweza kukwepa kwamba hana mkono wake hapo?  alihoji.

Kutokana na hayo, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete amtaje mmiliki halali wa Dowans ili kuwatoa kiu Watanzania wanaohitaji kumjua.

"Sitaacha kuzungumzia masuala yanayowagusa Watanzania na mali, hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanataka kuibiwa fedha zao, wakati wa kukaa kimya umekwisha" alisema Dk. Slaa.

Alisema hashangazwi na kejeli za Ikulu na kuwataka Watanzania kukumbuka alipoanza kuwalipua mafisadi, Rais Kikwete aliwahi kutamka kwamba kelele za mlango haziwezi kumnyima mwenye nyumba usingizi na kamwe kelele za chura hazimzuii ng ombe kunywa maji.

"Lakini baada ya sisi kuamua kupambana na Richmond, Rais Kikwete alikiri linamnyima usingizi na hili la Dowans litamnyima usingizi zaidi katika kipindi hiki cha mwisho cha uongozi wake" alisema Dk. Slaa.

Ili kumaliza kelele za Dowans, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumtaja mmiliki wake ambaye anataka kuwaibia Watanzania mabilioni ya fedha.

Wakati Dk. Slaa akimkaba koo Rais Kikwete, mjadala wa Dowans hivi sasa umewavuruga hata viongozi wa serikali tangu ilipoamriwa ilipwe sh bilioni 185.

Aliyekuwa Spika wa Bunge lililopita, Samuel Sitta, hivi karibuni alikaririwa akiitaka serikali iache kuilipa Dowans kwa madai kuwa ni mradi wa mafisadi watatu.

Kauli hiyo ilipingwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alisema kuwa suala la malipo ya Dowans lipo kisheria na ikithibitika serikali haiwezi kukata rufaa, italazimika kulipa mabilioni hayo.

Juzi Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Dk. Slaa kumtaja Rais Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa Kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.

Taarifa hiyo kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu aliyechanganyikiwa na mzabinazabina ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu, ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji, aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha.

Rweyemamu katika taarifa yake hiyo iliyoonyesha waziwazi kuandikwa na mtu mwenye hasira, chuki na dharau ama kwa Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima, alikwenda mbali na kumwita kiongozi huyo wa kisiasa kuwa ni mtu hatari.

Katika mahojiano maalumu na gazeti la Tanzania Daima Jumapili, mwishoni mwa wiki, Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala la Dowans kutakiwa kulipwa fidia limetokana na uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe anahusika kuileta Kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.

Chanzo:Tanzania Daima
 
Inauma lakini jamani inauma sana. Hivi kun watu wenye akili bdo hawaoni wizi huu!!!!!!!!!. Jamani nchi yangu Tanzania, E Mungu tulikufanyia nini sisi wajawako. Tuokoe na hili genge la majambazi wa ccm, wafedheheke, waaibike.
Unamlilia Mungu kafanya nn?katupa rasilimali mpaka zinatuua..ni sisi kuchukua hatua..mungu ana kazi nyingi za kufanya..hili la Tanzania ni upuuzi wetu wananchi wenyewe
 
Tafakuri Yangu Ya Leo: Ya Kakobe na TANESCO mwogopeni Mungu tujaribu kwa Mafisadi




KAMA kuna jambo linalowakera watanzania basi ni hili la Ufisadi miongoni mwa baadhi ya viongozi wetu. Watanzania wanajiuliza, iweje wao waendelee kuwa masikini ilihali wachache wanazidi kuneemeka huku wakikodi ndege kwenda kutumbuliwa vipele huko Berlin Ujerumani? Sasa mimi nina pendekezo binafsi mkiona linafaa tulifanyie kazi wadau.

Hivi mnakumbuka enzi zile za mgogoro kati ya Askofu Zakaria Kakobe na TANESCO? , Kakobe aliendesha harakati zisizo na umwagaji damu akazipachika jina la TANESCO Mwogopeni Mungu !! na fulana za njano alichapa tunazikumbuka, Sasa kwa nini na sisi tusitumie mbinu hii kuwashughulikia Mafisadi?

Na hii iwe Tafakuri yangu ya leo jamani

Nova Kambota Mwanaharakati
Kitendawili sio deni ukishindwa nipe mji
0717-709618 au 0766-730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com
10 Machi 2011
Njombe , Tanzania.
 
Hii kasi zaidi ya kukimbilia kulipa hela kwa wamiliki wa dowans hewa ni kiashiria kuwa serikali haina mpango wa kukata rufaa na pia ni kuwa wanajua kwa vile ni kampuni hewa ,hela hizo zinakwenda mifukoni kwa vigogo.
Tunazungumzia shamba la bibi, that is a proof!

Nashangaa hatukuwa na kasi yeyote kwenye kudai chenji ya rada mpaka wakoloni wetu wakasimamia kidete huku sisi tukiwa fofofo sitashangaa. Hii nayo ikiunganishwa kwenye episodes za radar comedy ni rahisi sana. Ni kiasi cha kui direct cash ya radar kuelekea kwenye korongo la Dowans kwisha kazi
 
Back
Top Bottom