Waziri Ndalichako unapata Faida gani Wastaafu kulipwa Kikokotoo?

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,985
2,770
Leo nimesitika Mbunge anachangia Wastaafu walipwe Mafao ya Mkupuo kama Awali. Ndalichako akaInterupt na kusema Watu wanaolipwa pesa nyingi Sana ambazo si zao hivi wanastahili Kikokotoo. Yaani miaka yote hii ndio Ndalichako kaona Waanze 2022 kupunja Wastaafu akidai wataishi miaka 12. Hivyo Kikokotoo kinawatosha.
 
Wanataka wafe ndipo walipe.

Kimsingi mstaafu anapaswa alipwe nusu ya fedha zake akiwa amegawanya nusu ya miaka yake kabla ya kustaafu, ili fedha hiyo imsaidie kwenye maandalizi ya kiuchumi.

Sasa unampa mtu haki yake akiwa na miaka 55/60 maradhi kibao! Sukari yake, presha, Moyo n.k saa ngapi atapambana kujenga maisha yake!!!

Kuweni na huruma, kwa kuwa wao wanapata marupurupu mengi ndio maana hawajali wale wanao tegemea fedha za kustaafu
 
Leo nimesitika Mbunge anachangia Wastaafu walipwe Mafao ya Mkupuo kama Awali. Ndalichako akaInterupt na kusema Watu wanaolipwa pesa nyingi Sana ambazo si zao hivi wanastahili Kikokotoo. Yaani miaka yote hii ndio Ndalichako kaona Waanze 2022 kupunja Wastaafu akidai wataishi miaka 12. Hivyo Kikokotoo kinawatosha.
Anatetea tumbo lake..tu hakuna kingine.

Mtu anastaafu halafu unampa mafao yake 47M halafu zingine unabaki nazo eti mumpe kidogo ndani ya miaka 12 ..akifa ndani ya miaka 3 mbona hamsemi chochote !!!???
 
Anatetea tumbo lake..tu hakuna kingine.

Mtu anastaafu halafu unampa mafao yake 47M halafu zingine unabaki nazo eti mumpe kidogo ndani ya miaka 12 ..akifa ndani ya miaka 3 mbona hamsemi chochote !!!???
HV tangu ln mwanasiasa akawa na huruma na mapenzi KWA mtumishi?wanahisi watumishi NI mazuzu.mbona wap miaka 5 Tu milioni zaidi ya 300.mbn hawazungumzii kujipa robo then nyngne wawe wanpewa kidogokidogo?
 
Hicho kikokotoo cha 33%, ni cha kipumbabu sana. I wish kingewagusa pia na hao wapiga meza baada ya kumaliza miaka yao 5 ya kupiga meza na vigelegele.
Yaani huyu Maza Professor anasiliba utazani hiyo Pesa iliyozulumiwa anapelekewa yeye. Eti Watu wanapewa Pesa nyingi ambazo si zao. Basi Wastaafu Wote warudishwe tangu ilipojulikana Pesa si zao. Amshukuru Magufuli na Wana Jf waliompitisha kuwa Waziri. Leo hii Angekuwa naye anakipata akitokea UDSm. Hana huruma ana Roho ya Kihutu na Kitusi. Mzee amefanya KazI 40 years akiwa Officer eti bila Aibu unampa Mkupuo wa Pensheni 39 Million. Halafu kila Mwezi unampa Laki 3na 50. Iko wapi Ile dhana ya kufaidi Pensheni Uzeeni? Wazee walikuwa na Madeni na ni wale waliokuwa hawana Fursa yeyote Ofisini zaidi ya monthly Salary.
 
Hivi na wao huwa wanalipwa kwa kikokotoo?.
Jibu la swali hili ndio la mhimu kuliko mada ya kikokotoo yenyewe.
 
Hivi na wao huwa wanalipwa kwa kikokotoo?.
Jibu la swali hili ndio la mhimu kuliko mada ya kikokotoo yenyewe.
Heche keshasema 272milioni Kwa miaka 5 tuu. Awamu hii huenda wakapewa 350milioni Kwa miaka 5. Wametumia pesa za Wastaafu kuwekeza miradi Isiyozalisha hata Hilo hawalioni. Majumba Marefu kama lile karibu na Tcra Hq halina Wapangaji pesa irudi. Daraja la Kigamboni, Ubungo Plaza watoke hazarani waeleze wanapata Faida gani kwenye hayo Majengo.
 
HV tangu ln mwanasiasa akawa na huruma na mapenzi KWA mtumishi?wanahisi watumishi NI mazuzu.mbona wap miaka 5 Tu milioni zaidi ya 300.mbn hawazungumzii kujipa robo then nyngne wawe wanpewa kidogokidogo?
Ndio hapo sasa.

Kinachonishangaza au kunisikitisha ni kwa nini Watumishi wapo kimya.

YAAANI HAKUNA KITU MWANASIASA ATAANZISHA KIKAWA NA MASLAHI MAPANA KWA UMMA. HAKUNA.

Mambo yao yote yanamlengo wa kisiasa ILA ifike wakati wananchi tuwe tunaingilia kati japo tumegawanyika kimaslahi.
 
Walimu wetu wakiwa ni kati ya watumishi waliotumikia nchi hii kwa zaidi ya miaka 30 eti walipwe 33%wakati wabunge wenyewe wanapewa zote .Lakini mchawi wa hao walimu ni Cwt ambao kwa kupitia Tucta waliomba watumishi walipwe 25% ya mafao siku ya maadhimisho ya mei mosi yaliyofanyika mkoani Iringa serikali kwa huruma wanaongeza asilimia 8 ikafika 33.Hao Cwt hawana nia njema na watumishi wa nchi hii uwingi wa wanachama wao ambao umewapa mandate ya kusikilizwa na serikali unaadhiri na makundi ya wanachama wengine
 
Huyo mama ni katili. Nitamlaumu sana mwendakuzimu kutuletea watu makatili kama yeye. Natumaini mama atapiga chini masalia yote ya awamu ya 5.
 
Huyooo mama Sijawahi kumuelewa hata siku moja, yupo kwa ajili ya kukandamiza raia tuu, hana lolotee tangu enzi ilee alipokua Elimu
 
Back
Top Bottom