Financial Intelligence
Senior Member
- Sep 29, 2023
- 113
- 249
Kwa ushirikiano na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, leo tumeianza hatua mpya katika safari ya kuimarisha uchumi wa kidijitali wa Taifa letu
Miongoni mwa mambo ambayo tumeingia makubaliano kushirikiana na Wizara, ni pamoja na:
Uundwaji wa “Jamii Namba” Hii ni namba maalum kwa Mtanzania itakayojumuisha huduma mbalimbali, yaani badala ya kuwa na namba tofauti tofauti, (Leseni, Passport, Nida) tunaweza kuwa na namba moja itakayo tambulika katika nyanja hizi zote.
Jamii Data Exchange Platform
Huu ni mfumo ambao utaundwa kuunganisha mifumo yote ya kiserikali hasa ile ya malipo ili iweze kuwa na mahusiano na uwezo wa kupata taarifa kutoka sehemu moja au nyingine kiurahisi zaidi.
Uundwaji wa mifumo imara zaidi ya malipo mtandaoni ambayo inawezesha huduma salama na rahisi za miamala ya kidijitali kwa wananchi kila wanapo pata huduma sehemu tofauti za serikali.
Kutumia wataalam wa Benki ya NMB katika kuunda na kuboresha mifumo, kwani tunajivunia kuwa na vijana wazalendo wenye utaalamu mkubwa juu ya maswala ya Tehama.
Benki ya NMB itatoa jukwaa la kufanyia majaribio (pilot platforms) ya mifumo itakayoundwa, ili kuhakikisha ubora na ufanisi kabla ya kuanza kutumika.
Makubaliano haya yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari – Mohammed Khamis Abdulla na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB - Bi. Ruth Zaipuna, wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari – Mhe. Nape Moses Nnauye.