Nape Nnauye: Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi iachwe iwe Huru, isiingiliwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye ameizundua rasmi Bodi ya Tume ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi huku akiitaka kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo iliyowekwa na si kwa Matakwa na Utashi wa watu fulani.

Waziri Nape amesema anatamani kuona tume hiyo inakuwa huru na kutoingiliwa kwa namna yoyote kwani Sheria na miongozo ipo wazi.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa TCRA Jijini Dodoma, leo Januari 19, 2024, Nape amesema "Natamani tume mkahakikishe, mnaanza kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa.

"Kama kuna tume tunataka iwe huru kutekeleza majukumu yake basi ni hii; hii Tume nataka iwe huru mlinde hilo. Tusiiingilie na nyie msikubali kuingiliwa, mlindwe na Sheria - tumezitunga, ziko na Kanuni. Kama kuna shida mahali, ni Bora turekebishe Sheria na Kanuni lakini msiendeshwe kwa Matakwa na Utashi wa watu, tuendeshe kwa mujibu wa Sheria".

Ameongeza “Mmeaminiwa, hamkupewa upendeleo, mchakato ulikuwa mkubwa, mnazo baraka na imani ya Watanzania, tumewakabidhi jukumu la kulinda taarifa zetu, fanyeni kazi kwa kujiamini.”

Amewataka Wajumbe wa Bodi hiyo mpya kuendeleza na kuandika historia ambayo inakwenda kutengeneza jamii ya watu wastaarabu kwa kuanzishwa Tume hiyo.

Ameongeza kuwa ilianza kutungwa Sheria ikazaa Tume na baadaye ikazaa Bodi ambapo lengo kuu ni kuhakikisha Taarifa za Watu Binafsi zinatunzwa.
Snapinsta.app_419536894_280484974701055_3944591058807001307_n_1080.jpg

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye
Snapinsta.app_419766178_327111526965614_6385735360174570483_n_1080.jpg

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Ukumbi wa TCRA, Jijini Dodoma, leo Januari 19, 2024.

Amesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za Watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni Taifa salama kwa huduma za Kidigitali.

"Tume hii ni mpya wenzetu huko Mataifa mengine walishaanza, ndio maana sisi hapa Tanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akaamua ianzishwe na amefanya kwa imani," amesema na kuongeza:

"Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato ulikuwa mkubwa kuwapata ninyi na kuipata tume hii na ukweli kutoka moyoni ninatamani kuja kusikia tume hii ya Taarifa Binafsi Nchini ni bora kuliko tume nyingine Duniani," amesema Nape.
Snapinsta.app_419540884_393870619703052_6641231005312064566_n_1080.jpg

Snapinsta.app_420329714_894344262163505_5223678645655638413_n_1080.jpg

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Balozi Adadi Mohammed, Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Fatma Mohammed Ali na baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya kuzindua Bodi hiyo katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma, leo Januari 19, 2024.

Amesema matumaini ya Taifa ni kuona faragha zao zinalindwa nchini kwani kuanzia sasa taarifa za watu zinakusanywa, zinachakatwa na kutuma sehemu sahihi ambapo misingi mikuu inazingatiwa ya kikanda na kimataifa.

"Nina matumaini baada ya muda watu watakuja kujifunza kwetu juu ya tume hii kwani nchi ya Tanzania ni Mwanachama kwa Nchi mbalimbali imeanza vizuri, hivyo tume kuhakikisha inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na msikubali kuingiliwa na badala yake mlindwe na sheria msiendeshwe.
Snapinsta.app_419818213_217324418121163_7786116553969904853_n_1080.jpg

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa TCRA, Jijini Dodoma leo, Januari 19, 2024.

"Utoaji wa huduma uhakikishe unaendana na Huduma za Kidigitali pia mifumo isomane na iwepo kila mkoa ili watu watumie mifumo kuliko watu kutoka mikoani kuja Dodoma au Dar es Salaam kutafuta mifumo nasisitiza muweke mifumo inayisomana," amesema.

Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah alikuwepo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi na mkakati huo ulikuwa unalenga mikakati mitano.

Amesema hayo ni Matokeo ya siku 100 ambapo wamefanikiwa kwa asilimia 90 kwani wameweza kujenga taasisi yenye sura nzuri inaonekana kujenga utambulisho anuani pamoja na logo na wako kwenye kutengeneza mpango mkakati.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi, Balozi Mohamed Adadi Rajabu amemshukuru kwa uteuzi wake kwa kuwaaminiwa na kuteuliwa kwenye tume hiyo na ahadi yao ni kufanya kazi kwa weledi unaotakiwa ili kuhakikisha tume inafanya kazi vile inavyotakiwa.

Amesema "Kikubwa ni kuelewa Sheria Namba 11 inaeleza majukumu ya tume inataka nini, majukumu ya tume inawataka kutunza Siri za watu taarifa za watu binafsi zinatunzwa.

"Kupitia maelekezo ya Waziri tutafanya kazi vile atakavyoelekeza bila kusahau kutoa uelewa kwa umma ili kujua kazi na majukumu ya tume.”
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye ameizundua rasmi Bodi ya Tume ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi huku akiitaka kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo iliyowekwa na si kwa Matakwa na Utashi wa watu fulani.

Waziri Nape amesema anatamani kuona tume hiyo inakuwa huru na kutoingiliwa kwa namna yoyote kwani Sheria na miongozo ipo wazi.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa TCRA Jijini Dodoma, leo Januari 19, 2024, Nape amesema "Natamani tume mkahakikishe, mnaanza kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa.

"Kama kuna tume tunataka iwe huru kutekeleza majukumu yake basi ni hii; hii Tume nataka iwe huru mlinde hilo. Tusiiingilie na nyie msikubali kuingiliwa, mlindwe na Sheria - tumezitunga, ziko na Kanuni. Kama kuna shida mahali, ni Bora turekebishe Sheria na Kanuni lakini msiendeshwe kwa Matakwa na Utashi wa watu, tuendeshe kwa mujibu wa Sheria".

Ameongeza “Mmeaminiwa, hamkupewa upendeleo, mchakato ulikuwa mkubwa, mnazo baraka na imani ya Watanzania, tumewakabidhi jukumu la kulinda taarifa zetu, fanyeni kazi kwa kujiamini.”

Amewataka Wajumbe wa Bodi hiyo mpya kuendeleza na kuandika historia ambayo inakwenda kutengeneza jamii ya watu wastaarabu kwa kuanzishwa Tume hiyo.

Ameongeza kuwa ilianza kutungwa Sheria ikazaa Tume na baadaye ikazaa Bodi ambapo lengo kuu ni kuhakikisha Taarifa za Watu Binafsi zinatunzwa.
View attachment 2876506
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye
View attachment 2876507
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Ukumbi wa TCRA, Jijini Dodoma, leo Januari 19, 2024.

Amesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za Watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni Taifa salama kwa huduma za Kidigitali.

"Tume hii ni mpya wenzetu huko Mataifa mengine walishaanza, ndio maana sisi hapa Tanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akaamua ianzishwe na amefanya kwa imani," amesema na kuongeza:

"Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato ulikuwa mkubwa kuwapata ninyi na kuipata tume hii na ukweli kutoka moyoni ninatamani kuja kusikia tume hii ya Taarifa Binafsi Nchini ni bora kuliko tume nyingine Duniani," amesema Nape.
View attachment 2876508
View attachment 2876509
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Balozi Adadi Mohammed, Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Fatma Mohammed Ali na baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya kuzindua Bodi hiyo katika ukumbi wa TCRA, jijini Dodoma, leo Januari 19, 2024.

Amesema matumaini ya Taifa ni kuona faragha zao zinalindwa nchini kwani kuanzia sasa taarifa za watu zinakusanywa, zinachakatwa na kutuma sehemu sahihi ambapo misingi mikuu inazingatiwa ya kikanda na kimataifa.

"Nina matumaini baada ya muda watu watakuja kujifunza kwetu juu ya tume hii kwani nchi ya Tanzania ni Mwanachama kwa Nchi mbalimbali imeanza vizuri, hivyo tume kuhakikisha inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na msikubali kuingiliwa na badala yake mlindwe na sheria msiendeshwe.
View attachment 2876510
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa TCRA, Jijini Dodoma leo, Januari 19, 2024.

"Utoaji wa huduma uhakikishe unaendana na Huduma za Kidigitali pia mifumo isomane na iwepo kila mkoa ili watu watumie mifumo kuliko watu kutoka mikoani kuja Dodoma au Dar es Salaam kutafuta mifumo nasisitiza muweke mifumo inayisomana," amesema.

Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah alikuwepo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi na mkakati huo ulikuwa unalenga mikakati mitano.

Amesema hayo ni Matokeo ya siku 100 ambapo wamefanikiwa kwa asilimia 90 kwani wameweza kujenga taasisi yenye sura nzuri inaonekana kujenga utambulisho anuani pamoja na logo na wako kwenye kutengeneza mpango mkakati.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi, Balozi Mohamed Adadi Rajabu amemshukuru kwa uteuzi wake kwa kuwaaminiwa na kuteuliwa kwenye tume hiyo na ahadi yao ni kufanya kazi kwa weledi unaotakiwa ili kuhakikisha tume inafanya kazi vile inavyotakiwa.

Amesema "Kikubwa ni kuelewa Sheria Namba 11 inaeleza majukumu ya tume inataka nini, majukumu ya tume inawataka kutunza Siri za watu taarifa za watu binafsi zinatunzwa.

"Kupitia maelekezo ya Waziri tutafanya kazi vile atakavyoelekeza bila kusahau kutoa uelewa kwa umma ili kujua kazi na majukumu ya tume.”
Shida je wanaaminika?
 
Okay. Hongera Mr Melo.

Lakini usifurahie saana kuwa miongoni mwa hao watu. Lengo lao sio Watanzania wawe huru, lengo ni kupata taarifa za watu wengi kadiri iwezekanavyo. Kvp? Pindi mtu atakapoenda kulalamika kwao, wao watakuwa wakiulizq maswali ambayo yatawafavor, na mlalamikaji kwasababu ana imani nanyi atajimwaga akijua yuko safe.
 
Naomba kueleweshwa,taarifa zangu zipi zitalindwa na tume? kwanini lazima kuwe na tume ili kulinda taarifa zangu? hao tume wanalindaje taarifa zangu? Wanalinda taarifa zangu dhidi ya nani?
 
Back
Top Bottom