Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

Wadau juzi tarehe 5/3/2011 mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika alifanya ziara jimboni kwake na kuzungumza na wananchi waishio kandokando ya Barabara ya Morogoro,kuhusu kuvunjiwa nyumba zao na hatma ya malipo yao.Walikubaliana na wakazi waishio pembezoni mwa barabara ya morogoro kuwa mapema siku hiyohiyo kumpelekea azma Waziri mkuu Pinda amwamuru Waziri wa Ujenzi Magufuli asitishe zoezi la bomoa bomoa,Nimetahamaki Leo Asubuhi Nasikia kuwa Magufuli Kaamrishwa asimamishe Zoezi la bomoa bomoa.Jamani Hv Nyie Chadema Kwani Nyie ndo wenye Nchi?Mbona kila kulicha matamko yenu ndo yanafuatwa kila siku?
 
Sasa angekulaje huu ujiko wa kuzima kauli ya Magufuli? Ukiangalia kwa jicho la tatu kuhusu hili utaona kuna hoja zaidi ya hii ndani yake!

Kama mimi ningekuwa Pombe, ningejiuzulu!

Mie sishangai kabisa kuona viongozi wenye mamlaka kisheria kutoa kauli zinazohitilafiana mbele ya vyombo vya habari na umma kwa ujumla.Hili ni ombwe ktk serikali ya jk,na kama magufuli anatambua maana ya dhamana aliyopewa,tunataraji atachukua maamuzi magumu.
 
Na pia huyu anayejitutumua na kujiita mtoto wa mkulima ni msanii mkubwa.bado ameendelea kuwa kama "shock absorber" wa mafisadi.
 
Wakimbana bungeni atatoa 'mchozi' tena kama ilivyokuwa kwenye issue ya 'maalbino'. By implication PM anaruhusu watu wajenge ndani ya hifadhi ya bararabara! Hii ni hatari sana hasa linaposemwa na mtu ambaye aliapa kufanya kazi kwa kufuata sheria!
 
Hili la Pinda ni agizo la kisiasa wala halitengui sheria husika. Sana sana watau watapata muda wa kutafuta mahala pengine pa kufanyia shughuli zao vinginevyo kama ukibaki ndani ya road reserve ukasingizia PM Pinda alisema usibomoe, yakija matingatinga hatakuwepo kukutetea.
 
Akili ya Magufuri huwasiielewi inashangaza sana aina ya Wataalam tulionao, wanawaza kuumiza wananchni tu!
 
Mie sishangai kabisa kuona viongozi wenye mamlaka kisheria kutoa kauli zinazohitilafiana mbele ya vyombo vya habari na umma kwa ujumla.Hili ni ombwe ktk serikali ya jk,na kama magufuli anatambua maana ya dhamana aliyopewa,tunataraji atachukua maamuzi magumu.
Kweli kabisa,ni sawa na mbowe/slaa hatujui yupi anamtambua rais na yupi hamtambui!
 
Acheni kujadili hili swala kisiasa, hili ni swala la kitaalam; Magufuri hajui analofanya.
 
Picha nyingine kama ya magufuli na mwandosya inakuja sasa ni magufuri na pinda
 
Hapa kweli ipo kazi. Halafu mbona mabasi mengi yana spidi 120 km/hr:hand:, hii kasi haitoshi?

Kasi haimaanishi ni speed 100km/hr au zaidi. Mabasi yataedna kwa speed ya 40km/hr kinachofanya yaitwe mabasi yaendayo kwa kasi, ni kwamba hayakaa kwenye foleni na magari mengine, yatakuwa na njia yao, na yatapewa upendeleo kwenye junction.
 
mwanawane imeniwia vigumu kukuelewa unataka kueleza nini katika post yakop maana kichwa cha habari hakiendani na kitu unachokizungumzia na pia unamalizia kwa kutoa ushauri, au ulitaka kutoa mapendekeza kwa watu kuwekeza kwenye hii barabara ili na wewe ufaidike au
 
Endeleeni na maandamano au maandalizi hayajakamilika na mnamsingizia Pinda kuyaahirisha?
 

Huyu Babu +CCM yake, wote Wanazeeka vibaya.
It is just the same old politics !
 
Ninachosema Magufuli ni mchapakazi lakini "at the same time" ni mtu wa media sana na media pia itamuumbua. Mimi nauliza tangu ateuliwe leo siku ya ngapi? je zile siku sitini za kumaliza traffic jam Dar es salaam hazijatimia bado? Kuna miundo gani imeimarishwa au kuibuliwa? traffic jam imepungua kwa kiasi gani? Tunahitaji tuone utendaji unaolandana na maneno yake. Hata media yetu yenyewe ni ya kibababaishaji pia maana sijawahi kuona media house yoyote iliyohoji hiyo ahadi yake. Unaweza ukawa mzuri sana kuibuibua issues ambazo zitakufanya uwe kwenye news kila wakati as if wewe ni model wa kiutendaji lakini ukawa one of worst kama ukiangaliwa katika jicho la tatu. Mimi sioni kama Magufuli anatimiza ahadi zake ambazo amezitoa lakini ni mzuri tu kutaja takwimu ambazo hata wakati mwingine "you can't confirm". Si mbaya kihivyo lakini si mzuri kihivyo pia!!!
 
Back
Top Bottom