Waziri Mansour Yussuf Himid asema Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar hana haki ya kuifuta MUAMSHO

mkataba

Senior Member
Jul 6, 2012
147
37
uamsho02.png
Waziri Mansour Yusuf Himid (ambae ni CCM) ambae ni wazir asokuwa na wizara maalum Zanzibar katika kuchangia hotuba ya WIZARA ya Sheria na Katiba ya Zanzibar leo hii jioni amepaza sauti kali kwa Wizara hio kwa kumwambia waziwazi Waziri wa Wizara hio Abubakari Khamis (CUF) kuwa hana haki ya kuifuta Taasisi ya kiislam ya Jumuiya ya MUAMSHO hapa Zanzibar kwasababu wanazungumzia ukweli mtupu ktk masuala ya muungano.

Na amesema kuwa yeye anawaunga mkono ktk harakati zao za uhuru wa Zanzibar bila woga, na ataendelea na msimamo wake huo mpaka Zanzibar itakapo kuwa huru kama ilivokuwa kabla ya muungano huu.
znz02.png

Huku akishangiliwa na wawakilishi wenzake amewakemea baadhi ya wawakilishi kutaka kuisaliti Z'bar na Wazanzibari ktk kuietea nchi yao kwa maslahi yao binafsi.
 
Tanganyika bado wamelala, wanataka wazanzibar wawasaidie kupigania haki zao.
 
Watuache tupumue na tutapumua mwaka huu inshallah. kwa sasa zanzibar hakuna cha ucuf wala uccm bali kuna uzanzibari hata wakinuna na kusema tumeoana ila ukweli ndo huo
 
My foot! Nape atampa onyo huyo Waziri

Hapana Mkuu yeye anasema hakuna wa kumfundisha na wakumuelewesha kuhusu ccm, kwa7bu anaijua ccm kuliko yyte, na zaidi kwake yeye ASP ndio muhimu zaidi kuliko ccm.

Kwa hio hana haja ya kushauriwa kuhusu muungano kamalizia kwa kusema "kwa muungano huu sebu (siutaki)"
 
Tusitishane amueni mtakalo maana tumeshawaambia hicho Kisiwa hakikutoka Arabia kijiografia / Kijiolojia ni kutoka Bara la Afrika. Sasa kama mnataka kuwakaribisha Waarabu wawatawale kuliko kujitawala wenyewe mlikoshindwa karne iliyopita haya? VUNJENI MUUNGANO HATA KESHO KULIKO KUPOTEZA FEDHA ZA BAJETI YA SERIKALI YA MUUNGANO
 
amani karume juzi aliapa kuulinda muungano, mama yake anaonekana kutokuukubali, mansoor ambae niliwahi kusikia ni ndugu wa mke wa karume(sina uhakika ) aliupinga siku nyingi tu. hawa wote ni makada wa ccm. kiukweli tulipofikia kama taifa kwa kuzingatia usalama wa raia ni heri tukagawana mbao bila ya machafuko wala uhasama.
 
Tusitishane amueni mtakalo maana tumeshawaambia hicho Kisiwa hakikutoka Arabia kijiografia / Kijiolojia ni kutoka Bara la Afrika. Sasa kama mnataka kuwakaribisha Waarabu wawatawale kuliko kujitawala wenyewe mlikoshindwa karne iliyopita haya? VUNJENI MUUNGANO HATA KESHO KULIKO KUPOTEZA FEDHA ZA BAJETI YA SERIKALI YA MUUNGANO
ukiongea taratibu watakuelwa si lazima ufoke, na kwa nini ulie? tuseme ndo unawatakia mema saaana au?
 
Wazanzibar wote wanaunga mkono UAMSHO.Hata huku bara wengi tu,tunawaunga mkono! Haya wenye chuki mezeni wembe mfe!
 
Shida ni kwamba wana dai talaka, wakipewa hawanyooshi mkono kuipokea.WANAJUA FIKA faida ya muungano kwao ila tatizo ni kwamba ili wabaki kwenye politics za ZANZIAR ni sharti waonekane hawaupendi muungano.
 
Wakati akichangia hakuna aliyeomba mwongozo au taarifa ya kutaka wawakilishi hao kupiga kura ya either kuwa na muungano au lah? Kama hawakufanya hivyo jua ni siasa ya kuteka akili za wazanzibari tu.
 
Hapo patamu sana ,na panahitaji uelewa aidha ni kuiteka sera ya CUF kwa upande wa Zanzibar au ndio GNU inataka kukatika ,huyo ni CCM anaepingwa ni CUF. Au tuseme Waziri Yusuf ameokoka.

Hongera wapemba machogo watatuelewa tu !
 
Wakati akichangia hakuna aliyeomba mwongozo au taarifa ya kutaka wawakilishi hao kupiga kura ya either kuwa na muungano au lah? Kama hawakufanya hivyo jua ni siasa ya kuteka akili za wazanzibari tu.

Zinedine,

..mansour ni kati ya wale wanaoogopa kura ya maoni.

..wanadai kuna waznz 350,000 wanaishi D'Salaam na uwezekano mkubwa wanaunga mkono muungano.
 
Zinedine,

..mansour ni kati ya wale wanaoogopa kura ya maoni.

..wanadai kuna waznz 350,000 wanaishi D'Salaam na uwezekano mkubwa wanaunga mkono muungano.

Haya naiitishwe hiyo kura ya maoni !
 
Wazanzibar wote wanaunga mkono UAMSHO.Hata huku bara wengi tu,tunawaunga mkono! Haya wenye chuki mezeni wembe mfe!

hata mimi nawaunga mkono walipo ni uzi nikuingiza udini na kuanza kuchoma makanisa kama ni wao kweli walio choma mana tiss hawashindwi kuchoma ili tuamini UAMSHO ndiyo walio choma.
 
hata mimi nawaunga mkono walipo ni uzi nikuingiza udini na kuanza kuchoma makanisa kama ni wao kweli walio choma mana tiss hawashindwi kuchoma ili tuamini UAMSHO ndiyo walio choma.

Nyinyi ndio mnaoitwa kutoa ushahidi mkaishia jela !Naona hata maandishi yako yanajikanyaga.Inawezekana umekatika akili.
 
Kesi zake nyingi za watu aliowapora ardi zao kwa jeuri ya Karume shemeji na hatimae watu kukimbilia mahakama lakini huko pia wapo wanasheria wa ukoo kina Fatma Karume na kesi zake babaake huwatisha kwanza majaji ili ashinde. Mansour ni Form 4 na ni mwizi wa kutisha licha ya kuwa basha wa wengi wa mawaziri wenzake. Ni uozo kwa mkoa wa Zanzibar! Liwalo na Liwe
 
Back
Top Bottom