Waziri Mansour Yusuf Himid (ambae ni CCM) ambae ni wazir asokuwa na wizara maalum Zanzibar katika kuchangia hotuba ya WIZARA ya Sheria na Katiba ya Zanzibar leo hii jioni amepaza sauti kali kwa Wizara hio kwa kumwambia waziwazi Waziri wa Wizara hio Abubakari Khamis (CUF) kuwa hana haki ya kuifuta Taasisi ya kiislam ya Jumuiya ya MUAMSHO hapa Zanzibar kwasababu wanazungumzia ukweli mtupu ktk masuala ya muungano.
Na amesema kuwa yeye anawaunga mkono ktk harakati zao za uhuru wa Zanzibar bila woga, na ataendelea na msimamo wake huo mpaka Zanzibar itakapo kuwa huru kama ilivokuwa kabla ya muungano huu.
Huku akishangiliwa na wawakilishi wenzake amewakemea baadhi ya wawakilishi kutaka kuisaliti Z'bar na Wazanzibari ktk kuietea nchi yao kwa maslahi yao binafsi.