Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Hongera kwa hiyo picha ya Master Sgt Thomas Sankara, mkuu. Unanikumbusha mbali.Back to the issue, jambo hili la Maige kumsimamisha Mkurugenzi ni maigizo tu kwani kiutawala Maige ni Waziri, a mere politician, Hana mamlaka ya kumteua au kubatilisha uteuzi achilia mbali kumsimamisha MKURUGENZI YEYOTE KATIKA WIZARA NZIMA. HE IS NOT THE APPOINTING AUTHORITY. Tunayo mifano mingi tuuuu hapa hapa Danganyika ya waliowahi kujidai eti wanayo mamlaka ya kusimamisha watendaji lakini Amri zao Ziliishia
kuwa nguzo za mipapai! Mkumbukeni Lowassa na issue ya maghorofa feki/fake chang'ombe, Diallo Anthony Ng'wandu akiwa hapo hapo Maliasili ya Yule jamaa sijui yuko wapi siku hizi. Wenye mamlaka hula ni Katibu Mkuu Luhanjo kwa mjibui wa ofisi yake na jakayaa mrishoo kikwete kwa mjibu wa ofisi yake
Mkuu hapo kwenye wekundu usije ukawa unachanganya na Master Sgt. Samwel Doe!! Turejee. Umenikumbusha habari za Tsere na Diallo. Diallo Alimsimamisha lakini Tsere akasema mimi na wewe ni wateuliwa wa Rais na huna mamlaka ya kunitimua. Tsere alibaki ila Diallo akang'oka. Nashangaa wabunge wetu walikuwa wakishangilia wakati Maige anasema amemsimamisha kazi Mkurugenzi. Hivi wabunge wetu hawajui nani ana mamlaka ya kumsimamisha mkurugenzi hadi washangilie uongo wa waziri? Pole pole ndio mwendo na hakika tutafika tu.
Wanyama hai 116 wanaibwa lakini waziri hachukui hatua za kinidhamu hadi bunge limkabe koo. Kumbe na Mkurugenzi alikuwepo Bungeni. Hii inaonyesha kwamba hana taarifa ya kusimamishwa kwake!!