Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,433
- 36,070
Ziwa Victoria halikugawanywa sawa saww, Tanzania tuna umiliki wa karibu theluthi mbili ya ziwa lote, wakati Kenya na Uganda wakipata sehemu ndogo.Kwa Mlima Kilimanjaro nitakuelewa lakini si kwa Ziwa Victoria kwani liligawanywa katikati, otherwise useme ulitaka Wakoloni wahakikishe kuwa Wajaluo wote (Rorya) wanakuwa ndani ya mipaka ya Kenya na Baganda wote (Kagera River) wanakuwa Uganda. Je, ungetatuaje mgogoro wa Wakurya ambao wengi wao (asilimia 70%) wako Tanzania? Je, vipi Wamasai ambao wako wengi Kenya (60%)?
Hili suala, Wakoloni walitamani kulitatua lakini lilikuwa ni gumu sana kutokana na mazingira ya wakati ule ambako hakukuwepo miundombinu yoyote ya umma, hivyo walilazimika kutumia natural boundaries katika kuweka mipaka.
Huyo ndio mkoloni, hakuwa fair japokuwa alikuwa na mantiki zake. Hivyo tukubali tu matokeo kuwa kuna mahali mkoloni alitupendela na kuna mahali alitupunja. Ndio ukweli mchungu huo.