Waziri Kivuli wa Afya Mbassa akomalia mgomo wa madaktari bungeni

Serayamajimbo

Senior Member
Apr 15, 2009
191
38
Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii Gervas Mbassa akomalia mgomo wa madaktari bungeni kwa kutaka Bunge lieleze ni kwanini taarifa ya serikali haipo kwenye ratiba ya bunge. Mbassa aliomba muongozo huo kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Spika kufuatia hoja ya dharura iliyoanza iliyotolewa na Zitto Kabwe naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Katika maelekezo yake Spika alielekeza kwamba kabla ya hoja hiyo ya Zitto tayari Spika alishakubaliana na serikali iwasilishe kauli kuhusu mgomo wa madaktari. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge akitoa maelezo ya nyongeza kufuatia maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alisema kwamba serikali itawasilisha kauli yake katika siku itakayopangwa na Spika. Mfululizo huu wa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kuhoji kuhusu suala hilo kunaelekea kuwa ni utekelezaji wa tamko lilotolewa na CHADEMA kwamba “Chama kimewasiliana na kimeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu maelezo hayo na kutumia njia za kibunge katika kuisimamia serikali kushughulikia migogoro kati yake na madaktari, maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na sekta ya afya nchini.”
 
Mwenyekiti ameipotezea hasa Lukuvi amesema sio Taarifa ila ni Kauli ya Mawaziri ndo itatoka na kutoa Tamko
 
ITAZAA MATUNDA HIYO AU??MAANA NAONA SERIKALI ISHAKATA TAMAA WANAFANYA BORA LIENDE TUU

nchi kusha uzwa hii
 
Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii Gervas Mbassa akomalia mgomo wa madaktari bungeni kwa kutaka Bunge lieleze ni kwanini taarifa ya serikali haipo kwenye ratiba ya bunge. Mbassa aliomba muongozo huo kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Spika kufuatia hoja ya dharura iliyoanza iliyotolewa na Zitto Kabwe naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Katika maelekezo yake Spika alielekeza kwamba kabla ya hoja hiyo ya Zitto tayari Spika alishakubaliana na serikali iwasilishe kauli kuhusu mgomo wa madaktari. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge akitoa maelezo ya nyongeza kufuatia maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alisema kwamba serikali itawasilisha kauli yake katika siku itakayopangwa na Spika. Mfululizo huu wa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kuhoji kuhusu suala hilo kunaelekea kuwa ni utekelezaji wa tamko lilotolewa na CHADEMA kwamba "Chama kimewasiliana na kimeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu maelezo hayo na kutumia njia za kibunge katika kuisimamia serikali kushughulikia migogoro kati yake na madaktari, maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na sekta ya afya nchini."

Hapo ndio penye mashaka............Spika yuko upande wa serikali na chama twawala.........
 
Serikali ya wajanja imejaa ujanjaujanja kama wa kina Lukuvi, kukwepesha mambo na changamoto za msingi za nchi si njia ya kutatua matatizo ni bora masuala haya yangejadiliwa wazi na kwa mapana yake ili kufikia ufumbuzi kamili, ukimya, ukwepaji wa changamoto si njia sahihi kutatatua masuala kama haya. JK shtuka, ngoma inazama mkuu........:hatari:
 
...hatutaki kusikia kauli zenu za kinafiki,tunakata madaia ya madaktari yapatiwe ufumbuzi wa haraka kumaliza mgomo...
 
Taarifa itatolewa wakati wa kufunga mkutano huu wa Bunge,serikali haina dhamira ya dhati katika kumaliza tatizo hili la madaktari.
 
af tunasema tuna utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka ktk mihimili mitatu ! Serikali inaingilia uhuru wa bunge!
 
Hivi huu upole wa kondoo utakwisha lini? Senegal wanaandamana sisi tumebaki na kusema eti tuna aman!! Ni aman gani hiyo ya wenzetu wanadai haki yako na serikali haitaki kuwapa?! Huku ndg zetu wanakufa hovyo kwa uzembe wa hao mafisadi. Kazi ni kujiongezea posho tu. Muda wa mapinduzi ndo huu, na si kesho!
 
suala ni sensitive lakin wawailishi wanakubali kukaa kitako wakti watu wanakosa huduma za afya na wengi kufariki.

Kazi ipo
 
suala ni sensitive lakin wawailishi wanakubali kukaa kitako wakti watu wanakosa huduma za afya na wengi kufariki.

Kazi ipo

Haya mambo yanakera ajabu,hapa wangeacha siasa na kutafuta ufumbuzi!!eti watu wanakufa maswali yanayoulizwa ni ya ajabu!!mtu anauliza minara ya simu,hivi kweli minara ya simu ni muhimu na roho zinazoangamia,ehee mungu tunaomba uwape hekima viongozi wetu.
 
Nchii hii hatuna Bunge, ila tunakundi la wanasiasa wa chama tawala na waupinzani wakiwa pamoja.

Hakuna cha upinzani wala nini lao moja tu ni kula,mbona mswada wa katiba walijifanya wana uchungu sana na kukataa kushiriki au uchungu uliokuwepo walikuwa wanaona wanazidi kubanwa kisiasa,kama wanaburuzwa kwa suala hili ni kwa nini wasiangalie njia mbadala au wanaona watapoteza 330,000/=??
 
Nchii hii hatuna Bunge, ila tunakundi la wanasiasa wa chama tawala na waupinzani wakiwa pamoja.

Kweli mkuu maana tungekuwa na bunge naamini moto ungelikuwa umeshawaka maana kuna kanuni inayozungumzia jambo la dharura ambalo linaweza kusababisha kusitisha shughuli za kawaida za bunge na kuanza kulijadili,sasa hapa napata picha ya kwamba mgomo wa madaktari sio jambo la dharula na wala halina madhara kwa taifa.
Ila time will tell
 
Back
Top Bottom