Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii Gervas Mbassa akomalia mgomo wa madaktari bungeni kwa kutaka Bunge lieleze ni kwanini taarifa ya serikali haipo kwenye ratiba ya bunge. Mbassa aliomba muongozo huo kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Spika kufuatia hoja ya dharura iliyoanza iliyotolewa na Zitto Kabwe naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Katika maelekezo yake Spika alielekeza kwamba kabla ya hoja hiyo ya Zitto tayari Spika alishakubaliana na serikali iwasilishe kauli kuhusu mgomo wa madaktari. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge akitoa maelezo ya nyongeza kufuatia maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alisema kwamba serikali itawasilisha kauli yake katika siku itakayopangwa na Spika. Mfululizo huu wa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kuhoji kuhusu suala hilo kunaelekea kuwa ni utekelezaji wa tamko lilotolewa na CHADEMA kwamba Chama kimewasiliana na kimeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu maelezo hayo na kutumia njia za kibunge katika kuisimamia serikali kushughulikia migogoro kati yake na madaktari, maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na sekta ya afya nchini.