Waziri Jenister Mhagama: Serikali Kuzingatia Mafungu Maalum ya Fedha kwa WAVIU Katika Utekelezaji wa Bajeti 2023/2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946

WAZIRI JENISTER MHAGAMA - SERIKALI KUZINGATIA MAFUNGU MAALUM YA FEDHA KWA WAVIU KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amesema utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na vipaombele vingine inazingatia pia mafungu ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika kila Wizara na Taasisi.

Ameyasema hayo mapema leo 25 Mei 2023, katika Ukumbi wa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA).

Mhe. Mhagama, aliendelea kusema kuwa hii ni namna ambavyo Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kwa dhati kusaidia utekelezaji wa Afua za masuala ya UKIMWI nchini, kwa kuzingatia maeneo muhimu ikiwemo masuala ya lishe bora, dawa za kupunguza makali ya virusi na kuhakikisha mambo mengine yanayochangia ustawi wao kupatikana.

Akizungumzia suala la Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 Mhe. Mhagama alisema kuwa kuna kila Sababu ya Sera hiyo kufanyiwa mapitio na maboresho kwani ni ya muda mrefu na kuona, namna gani sekta zote zinaweza kushiriki katika suala hili ili kuweza kuyafikia malengo ya dunia ya kupunguza vifo, maambukizi na unyanyapaa ifikikapo 2030.”

Niwahakikishie kwamba sisi kama Serikali tunaweza kusimamia kufikia malengo haya ya dunia.”Alisisitiza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA Mwalimu Leticia Mourice alimpongeza Mhe. Waziri Jenista kwa uteuzi wake na pia kumshukuru kwa juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, aidha aligusia kuhusiana na maandalizi ya Mdahalo wa Kitaifa kuhusu uhimilivu wa mwitikio wa jamii katika mwitikio wa Taifa wa UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Sambamba na hilo alizungumzia kuhusu, uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa, ambao unalenga utekelezaji wa NMSF5 (Mpango Mkakati wa Tano wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI) na alisisitizia umuhimu wa ushirikiano, katika kujenga mwitikio wa kijamii katika mapambano dhidi ya UKIMWI, akitolea mfano maeneo kadhaa muhimu ikiwemo Uhimilivu wa Kisera.

FxB324tWAAAAOCS.jpg
FxB9_N_WcAInwbe.jpg
FxB36vcWAAAHhPK.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom