Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Waziri wa kilimo mwaka jana alikomalia kuuza chakula nje ya nchi. Kitendo hicho kililalamikiwa sana kusababisha bei ya vyakula nchini kupanda zaidi ya maradufu, lakini waziri huyu alikomalia jambo hilo akitoa sababu eti anawatajirisha wakulima, wakati ukweli ni kuwa alikuwa akiwatajirisha wafanya biashara wenzake (middle men) na makangomba.
Alisikika akiapa kuwa katika utawala wake kamwe hatakubali kuzuia wakulima kuuza chakula nje ya nchi. Alisema piga ua hatakubali kwenye kipindi chake cha uwaziri. Tulishuhudia raia wa nchi za nje wakienea kwenye vijiji vyetu wakinunua mchele, mahindi, maharage na kadhalika hadi yaliyokuwa bado yako shambani.
Tulishuhudia maelfu ya ma semi trela yaliyosheneni vyakula kila siku yakipeleka chakula hicho nchini Kenya hadi Somalia. Bei ya vyakula huko Kenya ikawa nafuu sana ukilinganisha na huku kwetu ambako ambako bei zilipaa kwa zaidi ya 150%. Watanzania walio wengi wakawa hawa uwezo wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku.
Ikafika wakati nchi yetu ikawa na upungufu mkubwa wa chakula hadi ikabidi ianze kununua chakula kutoka nchi zingine hususani Zambia kwa kutumia akiba yetu ya pesa za kigeni (USD) na kusababisha uhaba mkubwa wa pesa hizo huko BoT hadi sasa. Hivyo wafanyabiashara wa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi wakawa wanakosa pesa (USD) za kuagizia bidhaa hizo.
Baada ya agizo hilo la leo kutoka kwa Rais Samia kupiga marufuku uuzaji vyakula nje ya nchi, huyu waziri wa kilimo anapaswa kujitathmini na kuachia ngazi kama alivyotuapia katika utawala wake.