Wazee Kumi na Saba (17) Waliodai Uhuru wa Tanganyika

Kumbuka Abdul Wahid Sykes ndio alimkaribisha Nyerere alipotoka Pugu, au hujui hilo?

Kwani pugu sio dar es salaam?
Hatahivyo ukweli ni kwamba sykes alimkaribisha kwake Nyerere. Baadae wazee wa gerezani wakagundua kwamba hawakuwa na uwezo wa kumshawishi mwingereza awape uhuru isipokuwa Nyerere. Wakamkabidhi uongozi wa TAA na baadae Nyerere akai transform TAA toka kuwa social club na kuwa TANU chama cha siasa na hatimaye Tanganyika ikapata uhuru chini ya uongozi shupavu wa Nyerere.
 
Katika hotuba inayoendelea sasa hivi Uwanja wa Uhuru, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataja watu 14 Muhimu ambao amesema "bila ya wao leo hii tusingekuwa tunasherehekea Uhuru, labda sisi ndio tungekuwa tunadai Uhuru". Kwa mara ya kwanza nasikia Abdul Wahid Sykes akikumbukwa rasmi kwenye sherehe za Uhuru kwa mchango wake.

Ahsante Kikwete.

wewe na wewe tabula rasa kweli kweli mwenzio kaomba listi yote na wewe unarudia kumtaja Abdul Wahid Sykes ambaye ameshatajwa au hukuelewa kilitakiwa nini?? au ni ushabiki?? au udini hasa baada ya kusikia jina la kiislamu?? funguka!!!!
 
Kumbuka kuwa hii haijawahi kutokea, tulikuwa tunaaminishwa kuwa ni Nyerere tu, mwanzo na mwisho. Leo Kikwete kakata mzizi wa fitina, tunataka historia za hao wazee, mimi naijuwa ya Sykes kama nilivyoisoma kutoka kwa Mohamed Said, hapa JF:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wananchi-miaka-50-ya-uhuru-wa-tanganyika.html

Hapo kwenye red; nakataa katakata! Kwamba Nyerere peke yake ndiye aliyedai uhuru? How? Basi kwa kuwa wewe uliamini sahihi to be fair kwenye "hadithi" au "masimulizi" yenu na Mohamed Said mngewataja/kumbuka na hao wengine! Vinginevyo na nyie mnaingia kwenye mtego uleule wa "waliowaaminisha watu kuhusu Nyerere" kama kweli imani hiyo ilikuwepo.
 
Sana tena, wacha mimi hata Kikwete anaikubali na leo amedhihirisha. Huyo ndio Jakaya, unaijuwa maana ya Jakaya?

Sifahamu maana ya jina hebu nijuze!,

Ila ninavyojua historia huwa haiandikwi na marais bali Historians, si Nyerere wala JAKAYA wanaoweza kuaminika katika historia. Ninaweza kukubaliana na Mohamed Said kwa kuwa ni Historian na si kwa sababu JAKAYA anamkubali.
 
Katika hotuba inayoendelea sasa hivi Uwanja wa Uhuru, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataja watu 14 Muhimu ambao amesema "bila ya wao leo hii tusingekuwa tunasherehekea Uhuru, labda sisi ndio tungekuwa tunadai Uhuru". Kwa mara ya kwanza nasikia Abdul Wahid Sykes akikumbukwa rasmi kwenye sherehe za Uhuru kwa mchango wake.

Ahsante Kikwete.

Kwanza kabisa napenda kuishukuru sana Serikali ya JMTz kwa kunialika japo nimekuja jana tu kwenye maziko lakin usiku ule ule nilipewa kadi ya kuhudhuria Uwanja wa taifa leo (Japo swala ya ijumaa imenikosa) na vile kunipa kadi ya kuhudhuria dhifa ya Taifa jioni leo Ikulu. nashukuru sana kwa kunikirimu.

Katika Hotba yake amewataja watu mashuhuri 17 na kubainisha katika hao ni watatu tu ndio wapo hai. Na akaanza kuwaita kuanzia Mzee Ally Sykes na wengine wawili. lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufika kiwanjani.

Ndipo akataja waliosalia 14 kwa majina. lakini hao ndio walikuwa ni TAA ambao baadae walipobadilisha mtazamo wao na kutaka kuingia kwenye siasa ndipo walianzisha TANU.

TUKUMBUKE PIA taa KILIKUWANI UMOJA WA WALE WALIOPIGANA VITA KUU AMBAO WALIKUWA WANAKUTANA DAR KATIKA KUBURUDISHANA NA KUKUMBUSHANA. hAKUNA HATA mWANAMKE mmoja. Vile vile hakutajwa Mze kawawa sababu yeye alikuwa mcheza sinema ya Muhogo mchungu na katibu wa chama cha wafanyakazi. Bibi Titi na wengine hawakutajwa.



 
Una haki ya kukataa, wala hunipeleki huko, lakini leo mzizi wa fitina umekatwa, ulishawahi kusikia Abdul Wahid Sykes akitajwa kwenye kumbukumbu za Uhuru na Nyerere, Mwinyi, Mkapa kabla ya leo?

Kwani wewe ulishawahi kusikia majina ya Lameck wa Usukumani, Cuthbert wa Mbinga, n.k. wakitajwa kabla ya leo? Hivyo, Sykes, kama kweli hakuwahi kutajwa haikuwa ajabu, wako wengi!
 
Abdul Wahid Sykes, unaongelea muasisi wa TAA na TANU na mtu aletoa jina la TANU, hao uliowataja waliasisi nini?

Kwani mada inazungumzia nini bibie? Tunazungumzia Uhuru wa nchi iliyoitwa Tanganyika au Tanzania Bara kwa sasa. Hatuzungumzii uhodari wa kutunga majina hapa!
 
Una haki ya kukataa, wala hunipeleki huko, lakini leo mzizi wa fitina umekatwa, ulishawahi kusikia Abdul Wahid Sykes akitajwa kwenye kumbukumbu za Uhuru na Nyerere, Mwinyi, Mkapa kabla ya leo?

Kwani FF, nini kilimzuia Kikwete kumtaja Sykes kwenye sikukuu zilizopita na akamtaja leo? Huu si mwaka wake wa sita? Hoja ni nini, Sykes hakuwahi kutajwa mahali popote kuanzia vitabuni hadi shereheni au shereheni tu?
 
mbona mi nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi kwenye somo la historia kulikuwa na mtu anayeitwa ALLY SYKES na kina SYKES wengine ambao siwakumbuki vizuri na ambao walishiriki kiikamilifu katika harakati za kudai uhuru.Huyu Ally sio ndugu moja na Abdul Sykes? Na kama ni ndugu mbona historia yao ipo wazi kabisa na hawakusahaulika?
 
Kama upo kama kwenye avatar yako, InshaAllah ntakustuwa kwenye dhifa leo usiku.

Ndivyo nilivyo kabisaaa na ni picha yangu halisi . Na nimevaa vazi langu hilo hilo la Taifa langu Oman kama linavyojionyesha kwenye Avatar.

Lakini pia unaweza nipigia simu namba ya Dereva wangu 255 777 420000. Ninapatikana. Kesho naenda Tabora insh'Allah

 
Ndivyo nilivyo kabisaaa na ni picha yangu halisi . Na nimevaa vazi langu hilo hilo la Taifa langu Oman kama linavyojionyesha kwenye Avatar.
,
Lakini pia unaweza nipigia simu namba ya Dereva wangu 255 777 420000. Ninapatikana. Kesho naenda Tabora insh'Allah

duuh barubaru pm kazi yake nini?? mbona yakhe unaleta za kama mtu anayebahatisha maisha!!!!!!!!
 
WHO CARES!
Thanks God nshamaliza historia ya shule ya msingi na sikuwasoma hao wazee wenu.
Nitahakikisha wanangu hawasomi hiyo historia kwa kuwapeleka wasome IB lol
Kwani inasaidia nini?
 
Inasaidi kujuwa wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunaeleke, Huku pwani tuna msemo, "mkataa asili ni mtumwa".
Unajua FF, Mi nilikua napenda sana kujua history ya Tanzania
kama ninaivyopenda ya nchi zingine.
Kitu kilichonifanya niichukie ni haya
malumbano yasoisha JF kuhusu mara
wazee wenu mara sijui nini?
Mnatuchanganya sana kwa kweli.
Wengine tunashindwa kuona objectivity kwenye hii mijadala
hadi tumeamua ku switch off kabisa.
Bora niwe "mtumwa" kuliko kupotezewa
muda na malumbano ya maisha ya watu!

 
Dereva wako? Hivi unakiwango gani cha elimu kabla sijaendelea?

Ni vizuri ukajuwa kuwa sina namba ya Tz. Natumia namba yangu ya Oman kwa kitu kinachoitwa Roaming. Hivyo inakuwa si rahisi kwa mtu wa Tz kuweza kunipigia kwani inakuwa kama unapiga simu za kimataifa japo mimi nikikupigia kutoka hapa ninakuwa napiga sawa na local.

Hiyo ni namba ya Kijana wangu ambaye kila pahala nipo naye ambaye kwa urahisi unaweza kunipata kwa local number.

Elimu yangu ni PhD. (Bcom- UDSM Tz), MBA (Carleton univ- Canada) na PhD (Sofia Univ -Japan).

Jina langu ni Dr Hamza Yousuf Al- Naamani. Je una la ziada?

 
Unajua FF, Mi nilikua napenda sana kujua history ya Tanzania
kama ninaivyopenda ya nchi zingine.
Kitu kilichonifanya niichukie ni haya
malumbano yasoisha JF kuhusu mara
wazee wenu mara sijui nini?
Mnatuchanganya sana kwa kweli.
Wengine tunashindwa kuona objectivity kwenye hii mijadala
hadi tumeamua ku switch off kabisa.
Bora niwe "mtumwa"
kuliko kupotezewa
muda na malumbano ya maisha ya watu!



Pole sana. Ni kweli inaboa na inakera! Lakini hata hivyo ni heri kupotezewa muda kwa kuweka historia vizuri kuliko kujifanya huna time na kuiacha hii mijitu iendelee na upotoshaji wao - itafika mahali utapotezwa jumla! Cheza na haya magaidi mabingwa wa propaganda za kizushi na chuki katika jamii.
 
Hakuna upotoshaji hapo leo ndio katajwa Mzee wetu wa Kariakoo Gerezani, Tunashukuru sana Mohamed Said, kwa kuweka historia ya uhuru humu JF
Usisahau kumlaani sana MS kwa kunyapalia udini na kutaka waislamu wajione wanyonge na wanaoonewa daima. Mzee huyu ni mtu hatari kuliko ukimwi.
 
Back
Top Bottom