Wazee Kumi na Saba (17) Waliodai Uhuru wa Tanganyika

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
22,124
49,376
Wakuu; kwa kujua au kutokujua, kwa makusudi au kwa bahati mbaya kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu hasa ni akina nani waliodai Uhuru wa Taifa letu Tanganyika.

Mh. Rais Kikwete leo kaweka kila kitu hadharani kumbe ni wazee 17 kutoka pande zote za nchi yetu walishiriki kikamilifu kudai uhuru wetu kinyume na historia inavyopindishwa au kuaminishwa kwamba ni watu wa Kariakoo pekee walifanya hivyo.

Tafadhali, kama kuna mwenye list kamili aliyoitaja Rais pale Uwanja wa Uhuru leo naomba aiweke humu. Hii ni muhimu sana na itatusaidia kuweka historia sawa tofauti na makala fulani iliyomo humu ambayo imejaa upotoshaji wa kutupwa.

Nawasilisha.

UPDATES: Waasisi 17 wa Uhuru wetu kwa mujibu wa alivyowataja Mh. Rais hawa hapa:

Julius Kambarage Nyerere, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes.
 
Kuna tatizo wapi?ina maana JK haitambui historia na michango ya hao wazee???naomba nijue kuna nini kimejificha??maana nadhani anawatambua waasisi wengi sana anashiriki hata kuwajulia hali zao mara kadhaa!!!
 
Katika hotuba inayoendelea sasa hivi Uwanja wa Uhuru, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataja watu 14 Muhimu ambao amesema "bila ya wao leo hii tusingekuwa tunasherehekea Uhuru, labda sisi ndio tungekuwa tunadai Uhuru". Kwa mara ya kwanza nasikia Abdul Wahid Sykes akikumbukwa rasmi kwenye sherehe za Uhuru kwa mchango wake.

Ahsante Kikwete.

Upotoshaji as usual. Yaani wewe umemwona Sykes tu? Mbona kataja wengi tena ni 17 siyo 14! Hebu full list hapa.
 
Katika hotuba inayoendelea sasa hivi Uwanja wa Uhuru, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataja watu 14 Muhimu ambao amesema "bila ya wao leo hii tusingekuwa tunasherehekea Uhuru, labda sisi ndio tungekuwa tunadai Uhuru". Kwa mara ya kwanza nasikia Abdul Wahid Sykes akikumbukwa rasmi kwenye sherehe za Uhuru kwa mchango wake.

Ahsante Kikwete.

kwani hujui leo ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika!
 
Katika wote alowataja Mh. Rais, FF kamwona Sykes peke yake na tayari amemwanzishia thread. Tunaomba full kwa mwenye nayo tafadhali. Hii ni muhimu mno kuweka historia vizuri.
 
Mtoa maada kauliza kama kuna mtu anawajua kwa jina... that would be good to pay tribute.
 
Wakuu; kwa kujua au kutokujua, kwa makusudi au kwa bahati mbaya kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu hasa ni akina nani waliodai Uhuru wa Taifa letu Tanganyika.

Mh. Rais Kikwete leo kaweka kila kitu hadharani kumbe ni wazee 17 kutoka pande zote za nchi yetu walishiriki kikamilifu kudai uhuru wetu kinyume na histori inavyopindishwa au kuaminishwa kwamba ni watu wa Kariakoo pekee walifanya hivyo.

Tafadhali, kama kuna mwenye list kamili aliyoitaja Rais pale Uwanja wa Uhuru leo naomba aiweke humu. Hii ni muhimu sana na itatusaidia kuweka historia sawa tofauti na makala fulani iliyomo humu ambayo imejaa upotoshaji wa kutupwa.

Nawasilisha.

Hakuna upotoshaji hapo leo ndio katajwa Mzee wetu wa Kariakoo Gerezani, Tunashukuru sana Mohamed Said, kwa kuweka historia ya uhuru humu JF
 
Katika hotuba inayoendelea sasa hivi Uwanja wa Uhuru, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataja watu 14 Muhimu ambao amesema "bila ya wao leo hii tusingekuwa tunasherehekea Uhuru, labda sisi ndio tungekuwa tunadai Uhuru". Kwa mara ya kwanza nasikia Abdul Wahid Sykes akikumbukwa rasmi kwenye sherehe za Uhuru kwa mchango wake.

Ahsante Kikwete.

Kwa hiyo unakubaliana na Historia ya Mohammed Saidi. Unajua Uhuru wa Tanganyika halikuwa suala gumu sana kuupigania ukichukulia mantiki kuwa Tanganyika ilikuwa inatawaliwa na Uingereza kwa dhamana ya League of Nations (Sasa hivi UN). Kilichokuwa kinatakiwa ili kupata uhuru ni watanganyika kuonesha kuwa wapo tayari kujitawala. Ninadhani watu hawa akiwapo Julius waliweza kuishawishi UN kuwa watngantyika wapo tayari. Msikilize Mohammedi saidi hapa chini

PodOmatic | Best Free Podcasts
 
Kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za Uhuru Abdul Wahid Sykes amekumbukwa Rasmi. Sijawahi kusikia kabla ya sherehe hizi za Uhuru.

Vp FaizaFoxy...kuna kitu au kulikuwa na something fishy...au ...nisaidie kama vipi ni PM nitashukuru dada...
 
Katika wote alowataja Mh. Rais, FF kamwona Sykes peke yake na tayari amemwanzishia thread. Tunaomba full kwa mwenye nayo tafadhali. Hii ni muhimu mno kuweka historia vizuri.

Mzee wa gerezani huyo mkuu.
Hana shida ya kuwataja wengine. Kitu kingine ambacho kimewavua nguo wamanyema wa gerezani, katika hiyo list ya watu 17 kataja watu toka mbinga, toka kanda ya ziwa, toka kaskazini, toka kanda ya magharibi, toka kanda ya kusini na toka kona zote za Tanganyika.

Sasa wanaojaribu kuipotosha historia kwamba mambo yote ya ukombozi wa Tanganyika yalikuwa gerezani kwisha habari yao.
 
Hakuna upotoshaji hapo leo ndio katajwa Mzee wetu Kariakoo! Tunashukuru sana Mohamed Said, kwa kuweka historia ya uhuru humu JF

lakini wa kwanza kutajwa ni Mwl Nyerere na wa mwisho kutajwa ni Abdulwahid sykes!
 
Hakuna upotoshaji hapo leo ndio katajwa Mzee wetu Kariakoo Gerezani, Tunashukuru sana Mohamed Said, kwa kuweka historia ya uhuru humu JF

Mkuu sina tatizo na Mzee wetu Sykes wa Kariakoo Gerezani. Tatizo langu ni wapotoshaji fulani waliojaa humu kutaka kutuaminisha kwamba hapakuwa na wengine waliochangia uhuru wa taifa letu. Kumbe kwa orodha ya Mh. Rais leo, watu wa makabila na dini mbalimbali walishiriki kikamilifu. Nasema, weka full list hapa kumaliza mzizi wa fitna.
 
Back
Top Bottom